ππππππππ: πππππππ π ππ ππππππ πππππ ππ.....22
πππππ ππππ....
"Mama hajra.. Ni wewe.???? Hapana mke wangu.. Nisamehe mimi.. Aliongea husein huku analia...
kwa hasira Husei aligeuka nyuma kumtazama Nic lakini alishangaa Kumuona Nic Kamnyooshea Bastola....
Kwa hofu kubwa huku jasho linamtoka husein aliruka na kumuwahi nic kabla hajafyatua Risasi...
Nic na mafunzo yote alijikuta anazidiwa nguvu na jibaba lenye kitambi..
Nic alidondoka chini kama gunia na kujigonga kichwa kwenye ukuta....
Sehemu moja ya kichwa chake kilikuwa kimebondeka sana jambo lililo pelekea damu nyingi kumtoka puani na mdomoni na kupoteza maisha..
Husei kwa haraka alimkagua mke wake na kuona anaendelea vizuri Kwasababu alishashonwa na kupakwa dawa kwaajili ya kukausha kidonda..
Husein alikwenda kumuita mlinzi wa geti na kusaidia kumpakia Arafa kwenye gari lake..
bila kuchelewa alifunguliwa geti na safari yakurudi morogoro ilianza..
Usiku wa majira ya saa nane na madakika walikuwa wamefika morogoro mjini..
aliwahi mapema kumpeleka mkewe kwenye hospitali ya rufaa ili apate huduma zingine..
Lakini ile anaingia tu kwenye geti la hospitali alishangaa gari lake linashambuliwa kwa kupigwa risasi.
Aliingiza ndani haraka bilakujua waliokuwa wanashambuli walikuwemo mule mule ndani ya hospitali...
Husein baada ya kuona anazidiwa ilibidi awashe taa zote za ndani ya gari lake na kushuka akiwa amenyanyua mikono juu..
Walikuwa ni askari polisi wakiwa wameongozana na mkuu wa mkoa wa morogoro...
kumbe mkuu wa mkoa baada ya kusika Rafikiake na mfamya biashara mwenzie mkubwa kauliwa aliamua kuja kumtege Husein Morogoro pia ili kulipa kisasi..
alijua hakuna sehem nyingine ambayo angeweza kwenda husei zaidi ya kumleta mkewe hospitali..
Husein alisogea hadi karibu na mkuu wa mkoa ambaye alikuwa ni rafiki yake mkubwa.
"Mkuu.. umeamua kunisaliti leo hii.??? Urafiki mimi nawewe ulianza miaka mingi sana na tumesaidiana kwa mengi sana...
Nashukuru na ninakuomba uniue tu ili nisiongeesiri zako mimi nawewe...." aliongea husein huku amepiga magoti analia...
HUSEIN.. Huna haja ya kuishi kwa ukatili wako.. Umemuua Nic.. nic ni ndugu yangu mimi na siwezi kuvumilia katika hili.. naomba unisamehe.. tutakutana Akhera.., KWAHERI KAKA....
Aliongea mkuu wa mkoa kwa hasira sana na kutoa Amri kwa askari wamshambulie Husei kwa kumpiga risasi...
Husein alipigwa risasi nyingi sana hasa sehemu za tumboni na kifuani na kupoteza maisha palepale hospitalini..
Askari walingia kwenye gari na kukagua na kumkuta Arafa akiwa kwenye hali mbaya sana..
walimmalizia pia na kuchukua baadhi ya pakiti ya Madawa ya kulevya kama uthibitisho...
Kesho yake asubuhi Mji mzima na tanzania nzima kwa ujumla ilitapakaa habari na sifa kedekede kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro pamoja na jeshi la polisi kwa kukamilisha mpango wa kudhibiti wauzaji wa madawa ya kulevya..
Mh Raisi alitoa pongezi zake na kumtoa mkuu wa mkoa wa morogoro kumhamishia Dar Es Salam baada ya kumuona ni kiongozi jasiri na anaeweza kudhibiti madawa, Raisi alifanya hivyo bila kujua kuwa mkuu wa mkoa mwenyewe ni nguli wa uuzaji wa madawa..
Mkuu wa mkoa aliona ni kama fahari kwake kusogezwa jirani kabisa na Lango la kuingilia madawa ya kulevya...
- Alihama na jeshi lake la polisi la morogoro kuja kuish nao dar es salam..
Aliwagawa kwenye maeneo muhimu yote kama bandarini na kwenye kiwanja cha ndege ili aweze kupitisha mizigo kwa urahisi...
Wiki mbili zilipita Hajra akiwa URUSI akiendelea na mafunzo yake yakiusalama.. Ni siku 14 tu zilipita lakinin kwao ilikuwa ni kama Miaka 14.. walikuwa wameiva hasa. walikuwa majasiri hasa.. na walikuwa wenye nidhamu kupita maelezo..
Hawakuwa na uhuru wa kuwasiliana na njee hivyo ilikuwa ni vigumu sana kwa Hajra kujua kama MAMA na BABA yake wameuliwa...
Hajra aliishi kwa amani sana pia IRENE alikuwa na furaha wakiendelea na Mafunzo bila kujua kama Mume wake aliuliwa tena aliuliwa na baba yake Hajraa ambaye wanashinda nae mda wote..
Laiti IRENE angetambua kuwa baba yake hajra ndio alimuua Mume wake sijui ingekuwajee...
Mazoezi yalizidi kuwa magumu siku hadi siku na baada ya miezi mitatu walianza kuingia kwenye madarasa kufundishwa mbinu mbali mbali za kumchunguza mtu na kufanya upelelezi bila kujulika.
walizidi kupata mafunzo hayo na baadae waluanza kutolewa pale kwa awamu na kwenda kwenye majeshi ya Umoja wa mataifa kupewa changamoto kubwa ya nchi yao na kitu gani cha kuanza kushughulikia...
ALIANZA T-3035 ambaye alikuwa ni IRENE. jukumu lake kuu alilopewa lilikuwa ni kwenda kufanya upelelezi kuhusu UFISADI na RUSHWA.. ilikuwa ni miongoni mwa changamoto kuu iliyokuwa ikiikabili Tanzania kwa wakati ule..
Baada ya kumaliza kupewa kazi yake na kukabidhiwa fedha za kutosha kutoka WORLD BANK alisafirishwa kwenda CANADA kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa Sura ili kuwa na muonekano tofauti na mwanzo...
Haikupaswa warudi na Sura zao za mwanzo kwasababu ingekuwa rahisi kujulikana.. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kukusanya taarifa na kupeleka umoja wa mataifa kisha umoja wa mataifa ndio inaagiza nchi ikabiliane na mtu fulani na fulani..
Baada ya kumaliziwa upasuaji IRENE alirudi tanzania akiwa kama mwananchi wa kawaida tu asiejulikana na mtu yeyote...
*
Baada ya IRENE alikwenda mwenzie mwenye namba T-3036 pia alielekezwa sehemu zake za kazi na kupewa fedha za kutosha kwaajili ya kazi na matumizi yeke.. alipelekwa Canada pia na kufanyiwa upsuaji wa sura..
huyu wa sasa alipaswa kwenda kusimamia mipaka ya nchi na uhamiaji.. alikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wakimbizi wanaishi salama pia kukabiliana na Ujambazi kwenye mipaka...
Watatu na Wamwisho alikuwa ni HAJRA T-3037 ambaye alikuwa na jukumu la kwenda kukabiliana na biashara ya madawa na usafirishaji wake.. hii ilikuwa ndio kazi kubwa kuliko zote.. walimkabidhi hajra kwasababu ya nidhamu kuu aliyo ionyesha wakiwa kambini na uongozi mzuri kwa wenzie..
Hajra alitumia muda mrefu sana kupewa maelekezo na mafunzo zaidi kwasababu wengi wanaofanya kazi hizi ni wasomi wakubwa na niwatu wenye uwezo mkubwa sana kifedha...
Ilikuwa ni kazi ngumu ila hakuwa na namna yeyote kuitekeleza kwaajili ya TAIFA LAKE...
Baada ya hapo alipewa fedha nyingi sana, na Umoja wa mataifa ulimwongezea pesa na ulinzi mkubwa sana kwasababu ilikuwa ni biashara yenye kuangamiza vizazi na vizazi..
Hajra alisafirishwa Canada kufanyiwa upasuaji wa sura na kusafirishwa kurudi Tanzania...
Walifika Tanzania kila mmoja kwa awamu yake na sura yake ya pekee sana tofauti na mwanzo..
ambayo hata wao kwa wao hawawezi kujuana... kilichobaki kilikuwa ni kazi tu...
Nilivyoshuka dar siku hiyo nilikuwa na furaha sana... nilikuwa nina fedha za kutosha..
nilitoka na kwenda hadi kinondoni na kuchukua chumba kwenye hotel moja kubwa iitwayo KILIMANJARO HOTEL..
nililala usiku huo na kesho yeke asubuhi nilitafuta mtu anipeleke hadi sehem wanayouza magari..
Nilinunua RAV4 new model ya kisasa kabisa ambayo ilikuwa imekamilika kila kitu hadi usajili..
Niliilipia kwakupitia Chec na kupewa funguo tayari kwa matumiazi..
Nilianza kuzunguka mjini nikiwa na usafiri wangu binafsi na kwamara yakwanza namiliki gari yangu..
Nilienda kununua Sim Mlimani City na kusajili lain mpya kisha kumtafuta baba kwasababu nambazake zilikuwemo kichwani..
Nilikuwa nimekariri namba ya baba kuliko kitu chochote..
Niliipiga lakini haikuwa hewani..
nilihisi huenda yupo bize na nitamtafuta baadae nimsalimie tu kisha nimwambie nipo Tanzania japo yeye pia hakupaswa kuniona au kunijua hadi nitakapo maliza kazi zangu..
ITAENDELEA...
Je.! nini maoni kwa mwanadada hajraa.??? ametua tanzania akiwa na muonekano tofauti.. hajui kama baba na mama yake wameshauliwa... Na kazi kuu aliyopewa anatakiwa kuanza kukabiliana nayo......
Jeee.. Bikira ipo au imemshinda na kuamua kuitoa.???
No comments: