ππππππππ: πππππππ π ππ ππππππ πππππ ππ.....23
πππππ ππππ....
nilihisi huenda yupo bize na nitamtafuta baadae nimsalimie tu kisha nimwambie nipo Tanzania japo yeye pia hakupaswa kuniona au kunijua hadi nitakapo maliza kazi zangu..
Asubuhi hiyo hiyo niliingia Mitaa ya Posta na kwenda hadi kwenye Mgahawa wa wahidi na kuagiza Supu ya kuku na Bagia..
Nilimiss sana kula vile...
Lakini nikiwa nakula alipita bwana mmoja akiwa anauza magazeti..
Nilimuhurumia tu kwajinsi alivyo vaa na alionekana amechoka sana..
japokuwa sikuwa mpenzi wakusoma magazeti lakini niliamua kumuungisha angalau apate hela ya kula..
Nilichukua gazeti na kumwachia chenchi.. nilimpa shilingi elfu tano..
Nikiwa naendelea kupata Supu Nilikuwa naiperuzi ile gazeti..
Lakini nilishangaa sana kuona Picha ya mkuu wa mkoa wa Morogoro na kichwa cha habari kimeandikwa..
"MKUU WA MKOA DSM ACHARUKA.. BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA YAZIDI KUSHIKA KASI DSM"
inamaana Huyu jamaa kahamishiwa dar.?? Sasa baba atakuwa amebaki na nani kule kama rafikiake mkubwa hivi yupo huku....
nilikuwa nikiwaza huku namtazama mkuu wa mkoa aliewahi kunisaidia miaka kadhaa nyuma nikiwa kichaa dodoma...
Nilitikisa kichwa tu na kwenda kulipia Supu na kutoka pale..
Nilinyoosha njia hadi nyumbani kwa Amir na kupaki gari langu nje ya nyumba yao...
Niliingia ndani nikiwa sina hofu kabisa kwasababu najua amiri atakuwa kazini..
Nilimkuta mke wake yupo na mtoto mchanga na Msichana wa kazii
"Mambo zenu wadada... samahani kuna dada Anaitwa Hajraa alikuwa ni nesi nimekuja kumuulizia.
niliongea kama mgeni wa heshima kweli..
" Hajraa alishaondoka mda mrefu sana uliopita.. yupo kwao morogoro...
Maana kuna tatizo lilitokeaga Baba yake Hajra alimuua kaka mmoja anaitwa nic ni mjombaake na mume wangu...
Baada ya kuua alikimbilia morogoro na kuuliwa na mkuu wa mkoa baada ya kukutwa na madawa ya kulevya kwenye gari lake...
Aliongea mke wa Amir kwa msisitizo...
"Unasemaje wewe mama.????? niliuliza kwa ukali hadi yule mama akaikumbuka sauti yangu..
'Heeeeehh dada unaongea kama Hajra kabisa...
Pia mke wake yule mzee yaani Mama yake Hajra aliuwawa na baadae mke mdogo wa yule mzee nilisikia aliuliwa pia na mali zake zote kubinafsishwa serikalini...
"Kwahiyoo unasema kweli NiC amekufa.????
Ndio na tayari tulishaenda kwenye Mazishi Mrijo Kondoa..
Nilibaki nimechanganyikiwa nisijue nini chakufanya..
jasho lilikuwa likinitoka hadi mikono yangu ilikuwa imeloa tepetepe.
Ahsante dada.. niliaga na kwenda hadi kwenye jumba la Uasherati..
Nilikuta ukuta wa nyumba ile umesogezwa juu na kufanya mtu wa njee asijue chochote kinachoendelea mule ndani..
kulifumgwa na nyaya za umeme kama ulinzi ili mtu akitaka kuruka apigwe shoti...
Nilifika na kwenda kuipaki gari yangu umbali mrefu sana kutoka pale ilipo nyumba na haikuwa rahisi kwa mtu yeyete kujua kama nipo na gari..
Nilisogea hadi kufika kwenye duka la mangi..
"Mangi naomba maji madogo..." nimwambia Mangi kisha kukaa kwenye Fomu njee ya duka lake..
mangi pia baada ya kuona nimekaa na yeye alikuja kukaa karibu yangu kabisa..
"Nambie Mangi.. hivi ile nyumba sikuizi watu hawaishi Mule.????
nilimuuliza Mangi kichokozi..
'Lile ni Jumba la uasherati dada..
kwasasa ni danguro la vigogo tu..
wanaingia Wabunge na watu wenye pesa zao..
wapo wanawake warembo wa kila namna..
Bikira na wanawake wa kawaida..
Kwasasa mule ndani kuna vyumba vya wageni.
Bar kwaajili yakulewa.. na swiming pool..
vyakula na kamari za kila aina..
Yaani hilo eneo lote humo ndani limejengwa..
Kuanzia saa 11 jioni utaona Magari ya kifahari yavyopaki hapa njee na wao wanaingia nda kupata starehe za kila aina..
Aliongea Mchaga huku anacheka..
"Kwahiyo mimi nikiingia naweza pata bwana mwenye Mali zake etieee...
'Weeehhh inabidi upendeze.. wasichana humu ndani ni wazuri weee.. kwanza kila kitu ni mamilionea tu ya pesa..
Niliinamisha kichwa chini na kuwaza dakika. kadhaa. nilimlipa mangi na kuondoka..
Nilikuwa nina nguo za kutosha nilizo ninia kwa wazungu..
Nilipita saluni na kutengeneza Nywele zangu vizuri kisha kwenda hoteli nilipochukua chumba na kupumzika.. Jioni nilioga na kuvaa vizuri sana..
Nilivaa simple tu.. Ilikuwa ni bukta fupi nyepesi na blauzi nyeupe huku nywele nimeziacha zimelalia mgongoni..
nilivaa sendels na saa kisha kuwasha gari kuelekea kwenye Jumba la UASHERATI..
Sikutaka kubeba silaha kwasababu nilikuwa najiweza sana kwa upande wa ngumi..
nilikuwa na uwezo mkubwa ila kuutumia uwezo wangu ni hadi inapohitajika na sio vinginevyo..
Nilifika na kukuta ulinzi mkali sana..
nilielekezwa wapi nipaki gari langu.. niliweka kama watakavyo..
Niliingia ndani na kwenda hadi kwenye kaunta wanapouzaga vinywaji..
Niliagiza GRAND MALT na glass kisha kukaa kwenye kona huku naangalia wadada waliovalia bikini ty wanavyo tumbuiza..
Lakini kwa mbali sana nilimuona Mkuu wa mkoa Yupo kwenye meza moja Upande wa magharibi wanakunywa na kula... kwa mbele zaidi watu walikuwa wakicheza kamari..
Kweli lilikuwa JUMBA la UASHERATI..
Niliendelea kumtazama mkuu wa mkoa sehem walipokaa lakini Moyo wangu uliniuma sana Kwanini aniulie baba na mama.?? hatakama wanauza madawa kwanini asiwafunge.???
Niliinuka na kwenda kukojoa..
njia ilikuwa ni mbele kidogo tu ya walipokaa akina Mkuu wa mkoa, Nilivyopita tu nilimuona mkuu kamtonya Askari wake akaja kunifuata Chooni.,
Niliingia chooni na kukojoa.. Lakini wakati namalizia kunawa mikono nilimuona askari wa kiume nyuma yangu...
"Kaka nidhamu gani hiyo hatakama ni Askari hupaswi kuingia kwenye vyoo vya wasichana sawa ..
Niliongea lakini yule askari alinitazama kwa muda na kuja kuninyanyua na kuelekea walipokaa akina Mkuu wa Mkoa.....
- Alinibeba kama karatasi fulani hivi..
- sikutaka kuleta fujo yeyote pale...
- Alinifikisha na kuniweka jirani kabisa na Mkuu wa mkoa..
- Who are you..? (wewe ni Nani.?) aliongea mkuu wa mkoa kwa sauti ya kilevi kwa kiasi fulani...
- naitwa Melania
- unakaa wapi na huku umekuja kufanya nini binti.??
- Nakaa kinondoni. nilikuwa napita tu nikaona magari mengi hapa njee na watu wengi humu ndani nikaambiwa ni Bar naweza pata kinywaji na ndio maana nilikuwa nimekaa kule kwenye kona nakunywa...
- mkuu wa mkoa alitoa ishara wakaja askari wawili na kunibeba kuniingiza kwenye chumba kimoja lililokuwa nje kidogo na ule ukumbi wa starehe.
walinitupa kitandani nakuniambia nisithubutu kuongea chochote hadi mkuu aje..
Kweli baada ya kama Nusu saa Mkuu wa mkoa alikuja chumbani na kuwatoa wale askari kisha kufunga mlango..
"Melania.. Yale maswali niliokuwa nakuuliza ilikuwa kukufaham tu...
Mimi ni Mkuu Wa mkoa wa hapa DSM..
Binti nimependa umbo laki sana...
kiukweli nilikuwa ninamke lakini alipata ajali ya gari na kufariki yeye na Mwanangu mdogo..
Sina mke wala mtoto hapa nilipo ndio maana unaniona nashangaa tu hapa bar usiku huu..
Aliongea mkuu wa mkoa kwa hisia sana huku akintazama machoni....
Nilijikuta namhurumia sana pia kwakupoteza mke na mtoto..
"Melania.. nakuomba uwe mke wangu..
nitakupenda sana na nitakupa utakacho..
na ili kukuthibitishia hilo tunaweza kulala hapa hata wiki nzima na nisikubake..
Naomba utambue naKupenda na ninakuheshim... Nakupenda melania..
nihurumie na ninaomba upokee moyo wangu..
"I need a time Mr..." Nahitaji muda bwana..
naomba nifikirie kuhusu hili na akili yangu ikiwa sawa nitakujibu..
Namba zangu ni Hizi hapa.. ukinihitaji mda wowote nipo hewani..
baada ya wiki nadhani nitakuwa sawa kabisa...
Kama itawezekana nitakujuza na kama haitawezekana nitakujuza..
Naomba uniache niende nyumbani..
pia waambie askari wako wasinifanye mimi kama mtoto kunibeba na kunitupa tu hovyo..
Niliongea na kubeba pochi yangu kisha kuelekea ulipo mlango..
Mkuu wa mkoa hakuwa mbishi..
aliinuka na kunifungulia mlango kisha kunipa mkono na kuniaga..
Nilifurahi sana kwa wema alio nifanyia lakini huruma juu yake ilizidi kuniingia japokuwa nilipata habari kuwa yeye ndio alihusika kumuua baba yangu na mama..
Nilifika hotelini na kuoga kisha kulala usiku ule..
Lakini kabla sijapata usingizi vizuri nilisikia kama kitu kimeniminya kifua changu na kunikamata shingo kama jinamizi vile..
Nilihangaika kurusha miguu lakini wapi..
nilijitahidi kutoa sauti lakini haikutoka..
Kwambali nilianza kusikiasauti kama ya mtu ikiniita kwanguvu sana..
"Hajraaaaaa...!!!!
Niliitika kwa sauti pia lakini haikutoka..
Nilizidi kuhisi nanyongwa na mtu nisiye muona.. hadi fahamu ikaanza kunipotea...
- " Hajraaa.. Mkubalie mkuu wa mkoa awe mumeo..
anakupenda kwa dhati.. atakupa kila utakacho..
- Itoe Damu ya bikira yako kwaajili ya kuliokoa Taifa lako..
Biashara hii ni kubwasana na inaua nguvu kazi kubwa sana bila watu kujielewa..
- Ukisema ukurupuke kumuua huyo mkuu wa mkoa utakuwa haujafanya chochote kwasababu watu ni wengi kwenye hili kundi..
- Lakini ukiwanae karibu atakupa siri zoye na njia zote za madawa utajua..
Mfumo mzima utautambua. wauzaji na wasambazaji wote utawajua na itakuwa rahisi kukamilisha kazi yako..
- Itoe damu yako Hajraa ulikomboe Taifa lako...
ITAENDELEA.....
Bikira ya hajra ndio hivyo jamani inatoka.. karibuni group...
No comments: