π’πˆπŒπ”π‹πˆπ™πˆ: ππˆπ“π€πŠπ”π…π€ 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ππ†π” 𝐄𝐏.....27





π’πŽππ†π€ ππ€π˜πŽ....
Aliongea mkuu wangu mara tu baada ya mimi kupokea simu na kunitia moyo..

Nilikata simu na kutoka chumbani kwa hasira sana..

Nilifika njee lakini sikuwaona.

Nilirudi ndani na kuchukua noti ya elfu kumi na kumpa msichana wa kazi kisha kumtuma sokoni.. sikutaka aone kinachoendea mule ndani....

Nilizunguka nyumba nzima lakini sikuwaona..

Kwa haraka nilianza kuingia kwenye vyumba ambovyo kwa namna yeyote wanaweza kuwemo..

Nilianza na ndani kwao.. sikuwakuta..

Kwaharaja niliingia jikoni ila bado sikuwaona..

Nilianza kupata hofu..

Nilikimbia hadi stoo na kuwakuta wamekaa wanapiga story..

Nilinyata hadi nyuma ya mmoja wao..

Nilimvunja shingo na kumlaza chini taratiibu bila mwenzie kujua chochote..

Nilirudi nyuma na kujificha pembeni ya gunia la mkaa.

"Mwanangu hili dili litatiki nakwambia.. hii picha ni mke wa boss kabisa navyomuona..

Ila usoni kavaa ngozi nyembamba ya bandia..

Yule jamaa alizidi kuongea bila kujua kama mwenzake ameshakufa..

nilizidi kumsikiliza lakini baadae aligeuka nyuma na kugungua mwenzie yupo chini na kuongea hawezi..

Alishtuka sana na kuanza kutetemeka..

Wakati huo mimi pia nilijitokeza nikiwa namuita majina yake..

"Khalfani.. khalfani.... khalfani..

Niliita nikiwa naipiga piga kisu niliyoibeba kwenye mkoni wangu.

"Samahani ndugu ushahidi utaenda kuutolea mbinguni..

Niliongea na kuruka hadi alipo kisha kumvunja shingo pia...

nilitoka njee upesi na kuchimba shimo ndefu nyuma ya nyumba..

Ardhi ya dar haikuwa ngumu kiasi cha kunishinda mimi..  ndani ya dakika thelathini tu nilikuwa nimechimba na kuwafukia wote wawili na kupanda maua pamoja na nyasi juu yao..

Nilimwagia maji yakutosha kisha nikarudi chumbani kwangu.  nilijiamini kwasababu mume wangu hakuwa na tabia ya kwenda nyuma ya nyumba mara kwa mara..

Dada wa kazi alirudi na kupika chakula cha jioni..

Nilitoka na kutulia sebuleni nikiangalia TV hadi mume wangu akarudi kutoka kazini..

Alipiga sana honi na mimi nikafanya makusudi bila kumfungulia...

Ila baada ya dakika kama nne au tano hivi nilitoka na kumfungulia..

Alipaki gari na kushuka..

"Ooohhh samahani mune wangu.. nilijua halfani yupo getini kunbe hajarudi na mwenzie.. niliwaagiza sokoni wakanunue vyakula niliwakodia tax lakini hadi sasa siwaoni..
Niliongea na kumpokea mume wangu bahasha yake. 

"Usijali mke wangu.. mwenyewe nilihisi wametoka maana siyo kawaida yao..

Kwani umewapa bei gani?? maana wale ni walevi sana.. ukiwapa hela kubwa hawawezi kurudi...
Aliongea mume wangu..

" Niliwapa laki mbili kwasababu unga wa chapati ulihitajika.. sukari na mafuta ndoo moja kubwa.. pamoja na usafiri..

" Daaaahh mke wangu umewapa pesa nyingi hawawezi kurudi tena wale..

Aliongea mume wangu na kuanza kupanda ngazi kwenda chumbani..

"Nilimfuata na kumfuta jasho kisha kumvua nguo na mimi kuvua ili tukaoge..

Tulioga na kurudi sebuleni kula huku tunapiga story..

mmewangu alishika sim yake na kumpigia mkuu wa kituo kuagiza aletewe askari wawili kwaajili ya ulinzi usiku ule...

Tulimaliza kula na baada ya mda walikuja askari wawili na kuachwa getini..

Tuliingia ndani kwetu na kulala usiku huo...




Asubuhi na mapema mume wangu alienda kazini.. alishaanza kusahau matukio yaliyopita..

nyumba ilikuwa na amani sana pia.. jioni yake Walikuja ndugu zake na mkuu wa mkoa kutoka bukoba na vijana wawili wa kazi.

ilikuwa kazi zao ni njee tu bustanini..

Nilifurahi kidogo kupata watu washamba kidogo kutokea bukoba nilijua hawataniumiza akili...

Siku zilienda sana na miezi miwili iliisha hadi matukio yaliyo tokea yakasahaulika kabisa..

Mimi pia kitumbo kichanga kilianza kujitokeza na kunifanya niwe na hofu na hata kutoka kutembea ikawa ngumu sana kwa aibu niliyo nayo...

RC baada ya kugundua mke wake ni mjamzito alizidisha sana mapenzi na kunifanya niwe bize na yeye hadi kusahau kazi yangu iliyonileta..

kutoka Out ilikuwa ni kila siku.. vyakula vizuri na ziara za njee ya nchi viliongezeka..

Nilijikuta na mhurumia sana RC hadi kuanza kuwaza siku nikimuua huyu bwana nitapata wapi tena mume mimi..

Mapenzi yalikuwa yadhati sijawahi kuona..

Ndugu zake walinipenda sana kuanzia mama mkwe hadi wifi zangu..

ile hali ilikuwa ikinifanya nijione fahari sana na mwenye bahati kuliko msichana yeyote..

**

Msimamizi wangu alikuwa akinipigia simu kila siku na kunigombeza sana ila sikumuelewa..

nilibaki kujisemea kimya kimya tu. "Mkuu hajui nini napewa ndio maana anaropoka..

ilifika hatu hata simu za Mkuu wangu nilikuwa sinzipokei..

Miezi ilikata na baadae kujifungua mtoto wa kiune alieitwa JUNIOR..

lilikuwa jambo jema sana kwangu na kuniongezea mapenzi kwa mune wangu kwasababu ya kupata mtoto tena alie fanana nae..

Wanaume wengi hujiona fahari kupata mtoto alie fanana nae..

*
*

Siku moja nikiwa sebuleni alikuja msichana wangu wa kazi na kuniambia..

"Boss... Muda nikiwa naangalia TV kuna wavulana wawili nimewaona wakiingia chumbani kwangu ila nilivyoenda ndani sikuwaona tena."
aliongea Msichana wa kazi kwa hofu sana..

"huku ndani kuna wanaume gani wakuingia mwanangu hadi ndani kwako.. wakati hata wale wafanya usafi njee hawajui sebule ipoje.. Niliongea huku namtazama kwa umakini

" Mama jana nimeamka nimeloa kwenye sehem zangu za siri.. leo nimeona watu nakwambia hutaki.  au hutaki niendelee na kazi hapa kwako.?? inamaana kunasiku ninewahi kukupa malalamiko yoyote mama kuhusu humu ndani. ni miaka mingapi nimekaa hapa bila tatizo.????
aliongea mdada wa kazi na kulia kuelekea jikoni..

. uuuhhhh... nilishusha pumzi na kunyamaza kimya.. kweli maneno aliyoyaongea yalikuwa na nguvu sana..

Ghafla nilisikia mwanangu chumbani akilia kwanguvu utadhani amefinywa lakini nilivyoingia nilimuona anacheka tu..

Niliingia na kumsogelea..

 nilijitahidi kumshika ila alikuwa anaangalia upande mmoja tu huku anacheka utadhani kuna mtu upande ule anamchekesha..

Nilishtuka sana na kuanza kutetemeka baada ya kusikia watu kama wananong'onezana wakiambiana

"Ni huyu hapa hajraaa.. muangalia shingo yake.. amevaa ngozi ya bandia sema boss hajui tu angesha muua...
hahhaahaahahahhaha....

Nilisikia sauti kama ya wale watu wawili nilio waua nyumbani kwangu mwaka mmoja uliopita.. walikuwa wakiongea vilevile huku wanacheka lakini nilikuwa siwaoni.....

ITAENDELE....




No comments: