ππππππππ: πππππππ π ππ ππππππ πππππ ππ.... 43
πππππ ππππ....
Hapo ndio nilianza kutambua kuwa Ojala huenda usiku wa jana alivyojiuza alimuibia mtu.. Na kesi yeto ikahamia kwa Omera asiejua kitu ila kwasababu tu wamefanana sana..
Niliguna na kwenda mbio hadi kwenye ile hoteli niliyomwacha Ojala..
Nilimkuta Ojala anaongea na sim.. Nilikaa na kumsubiri amalize maongezi yake...
Lakini alikuwa bado anabebika sijui alikuwa anaongea na nani.!!
Nilikuwa nikiahangaika kutoka na kuingia...
Baada ya ojala kuona nahangaika sana alikata simu na kuja kunifuata nilipokaa..
Vipi mama.. Kuna tatizo.?? Where is Omera? "omera yupo wapi.?
"She has been arrested by police' Amekatwa na polisi..
Nilimjibu na kuendelea kukaa kwa kuhangaika kwa msongo wa mawazo..
Basi Hajra usiwaze mamy... Hili linaisha mda huu huu..
Ojala alishika sim yake na kumpigia mkuu wa kituo na kumwambia kuwa ndugu yake kakamatwa..
Alimaliza kuongea nae na kukata sim akiwa anatabasam tu...
Kumbe ojala alikuwa akiliwa hadi na mkuu wa kituo cha polisi cha jirani na mitaa ambayo tulikuwa tunakaa..
Nusu saa baadae Omera aliletwa akiwa na furaha.. Hatukuamini.. Kumbe ojala alikuwa na urafiki na maaskari karibu wote..
Tulifurahi na kula pamoja kisha kuoga na kumwambia ojala anielekeze ilipo "international bank" benki ya kimataifa..
Aliita tax anae muamini na kumwambia anipeleke..
Account yangu ilikuwa na pesa za kutosha nilizopewa na world bank kipindi cha nyuma kwaajili ya kupambana na wauzaji wa madawa..
Pesa zilikuwa nyingi sana...
Nilitoa karibu milion 30 naira za nigeria na kumwambia tax anipeleke mtaa wanao ishi washua tu.. Yaani maeneo ya kifahari...
Kwa dar es salam tunaweza kusema Masaki vile..
Tulifika na dereva tax akanionyesha sehemu panapo pangishwa apatments (nyumba) na kwenda kukodi..
Ilikuwa tayari na vitu vya ndani kama kitanda na makochi.. Mahitaji ilikuwa ni vitu vya jikoni kama gesi na mengine madogomadogo..
Ilikuwa ni mtaa wa kishua sana..
Baada ya kumaliza mambo yangu yote nilirudi hotelini na kuwafuata akina ojala kama sapraizi vile..
Sikutaka wajue chochote.. Niliwapeleka hadi nilipochukua nyumba na kumpa kila mmoja chumba chake ili tuanze maisha mapya..
Hawakuamini kabisa..
"Ndugu zangu... Hapa nimelipia miezi miwili tu.. Siku 60.. Tuhakikishe ndani ya huo mda tumepata muafaka wa kurudi tanzania au ikishindikana tuwe na kazi inayoeleweka..
Tuliweka mizigo yetu na kutoka kuanza mizunguko jioni ile japo nilikuwa nimechoka sna..
Mitaa ilikuwa ni tulivu sana.. Ni ubaridi wa vivuli vya miti mikubwa na milio ya ndege mbalimbali ulipendezesha mtaa.. Ulikuwa ni mtaa mmoja tulivu sana ulio jaa nyumba za kifahari na mtaa msafi kupita kiasi .
Babara hazikuwa na misongo ya magari wala watu wasio eleweka..
Tulikuwa tukipishana na wazungu na wahindi wakiwa mazoezi wanakimbia pembezoni mwa barabara..
"asante shost hii mitaa ningeishia kuona kwenye movie za kinigeria tu..
Aliongea Omera na kufanya wote tucheke..
"we siulikuwa jini ukashindwa kutumia nafasi yako vizuri.. Ungekuwa unaenda hata NewYok kidogo na kurudi.. Ulikuwa huhitaji viza wala nini..
Alidakia omera akimchamba dadaake..
"Hivi unadhani mda ule unakuwa na hizo akili basi.. Yaani ni sawa na ukipata hela za haraka, unasahau kabisa kama ulitakiwa kujenga... Ila ikiisha ndio unaanza kuwaza..
Yaani natamani ningerudia kuwa jini saivi ningekuwa Tanzania tu.. Hichi kiherehere kimeniisha..
Aliongea Omera kama utani lakini kwa msisitizo kiasi fulani kama anamaanisha vile..
Tulizidi kutembea ile mitaa na kufika sehemu kuna kama pub.. Magari yalikuwa ni mengi sana ya kifahari na kulikuwa na mziki wa polepole sana..
Tulijisogeza na kukuta kama swiming pool kubwa sana.. Watu walikuwa wengi kupita kiasi na kulikuwa na pub kwa ndani.. Watu walikuwa wakifurahia tu maisha yao..
Niliingia nikiwa naongozana na wenzangu kwa madaha na kwasababu tulikuwa na fedha za kutosha haikuwa ngumu kwa sisi kuagiza chochote..
Tulipita na wanaume karubu wote maeneo yale walikuwa wakitukodolea macho uwembamba wetu na nywele zetu zenye matunzo zilizolala mgongoni zilikuwa ni miongoni mwa sababu ya kuwafanya watushangae..
Ila kubwa zaidi ilikuwa ni kufanana kwa Omera na Ojala ambao hata mimi mwenyewe walikuwa wakinishinda kuwatofautiaha.. Kilichokuwa kikinisaidia ni mavazi yao tu..
Omera alipenda kuvaa kwa heshima sana ilia Ojala ndio alikuwa kivuruge nadhani kwasababu ya ukahaba aliokuwa akiufanya Lagos..
Tulifika kaunta na kuagiza wine.. Tulishangaa sana kukuta hadi red wine za Dodoma zipo kule nigeria..
"mmmhh kweli TZ ni nchi kubwa ndugu zangu.. Huu mzigo hadi huku upo..
Tulicheka na kuionea fahari nchi yetu kwa kutoa bidhaa ambazo zilikuwa zikikidhi viwango..
"Tunyweni hii moja tu ndugu zangu... Mkizidisha hapa tutatafutana.. Tutashindwa kujua hata tunarudi vipi geto...
Aliongea Omera..
Omera ndio alikuwa na busara sana kuliko sisi wote pale..
Tulikunywa kistaarabu na kuagiza chipsi na kuku kisha kwenda sehemu na kuhifadhi nguo zetu kisha kwenda kuogelea..
Omera na ojala walikuwa kama kivutio cha utalii kwenye lile swiming..
Hadi alikuja mdada Nadhani ndio alikuwa mmiliki wa ile pub..
"habari zenu warembo.. Naona leo mmelichangamsha pub yangu na kufanya watu wote wawashangae nyie..
Aliongea yule dada kwa lugha ya kiingereza hukua anawashangaa akina Ojala..
Mimi naitwa INI EDO.. Ni mwigizaji wa filamu za Nollywood pia ni mmiliki wa hii pub na zingine nyingi hapa mjini lagos.
Nawaomba warembo muwe sehemu ya wana mitindo wangu kwa kunisaidia kutangaza biashara zangu hasa mavazi na bidhaa za juice kutoka kwenye viwanda vyangu.
Alizidi kuongea yule dada..
Nilifurahi kuona dili limepatikana lakini yule dada hakuwa na habari na mimi hata kidogo.. Mda wote alikuwa akiwashangaa akina Omera na mwenzie..
Waliomba wapewe mda wakujadili na kama ikiwezekana kesho yake atapewa majibu..
Tulimaliza kuogelea na kutoka kurudi nyumbani..
Nilikuwa naaibu sana kupita na chupi mbele ya macho ya watu..
Nilijikaza hadi kwenye vyumba vya kuvaa nguo na kuoga vizuri kisha kutoka..
Tulifika nyumbani na kupumzika tukiangalia TV..
Lakini baada ya muda tulisikia mlango umegongwa.
Omera aliinuka na kwenda kuufungua mlango..
"Habari yako.. Naitwa Otien.. Niliwaona kwenye INI pub jioni hii ya leo nikaona nije kuwafuata..
Kuna dada mmoja nina shida nae kati yetu..
Aliongea yule kaka,
" dada yupi.??
Kuna mmoja ambae hamjafanana nae.. Namuomba mara moja..
"HAAAJRAAAA. Unaitwa huku njoo upesi...
Aliita Omera.. Nilisogea hadi mlangoni na kumkuta huyo kaka..
" Samahani dada. Naomba tukaongelee hapo njee kwenye gari kama huto jali..
Alisema yule kaka..
Omera aliniangalia na kwaishara aliniambia niende tu baada ya kuona ni mkaka mwema na mtanashati..
Omera alirudi ndani na sisi tukaelekea hadi ilipo gari na kuingia ili tuongeaa...
Kabla ya kuanza kuongea nilimuona yule kaka akichungulia mlango wetu na kuona Omera amesharudi ndani na mlango umefungwa..
Nilishangaa nimefunikwa kitambaa kizito usoni na gari likawashwa na kuondolewa mbio sana maeneo yale..
ITAENDELEA..

No comments: