ππππππππ: πππππππ π ππ ππππππ πππππ ππ.... 44
πππππ ππππ....
Nilishangaa nimefunikwa kitambaa kizito usoni na gari likawashwa na kuondolewa mbio sana..
Gari liliende umbali mrefu kiasi na kufika sehemu fulani ikasimama.
Nilibebwa na kuingizwa kwenye chumba funani chenye ubaridi kiasi nadhami ikuwa AC ile..
Nilikalishwa kwenye kiti na kutolewa kile kitambaa kichwani..
Nilishtuka sana kumuona yule Mkuu wetu alietufundisha kule urusi akiwa amekaa mbele yangu..
Nilitazama kulia na kushoto na kuona wanaume kama sita hivi wananishanga huku wote wanatabasam na kupiga makofi kama kunipongeza.
"Hajraa.. Umefundishwa kwa muda mrefu kuliko wenzio lakini nakuona unatoka njee kabisa ya mafundisho yako..
Nakuomba uwe makini sana na majukumu uliyoagizwa..
Bado nina imani na wewe na ninaamini siku moja Tanzania itakuwa salama..
Chukua hii karatasi. Inayo ramani ya majumba yote ya wauza madawa. Picha zao na majina yao yamo humo.
Narudia tena kukwambia..
"Hajraa. Tunakuamini na kila hatua upigayo tupo nyuma yako...
Nenda walipo wenzio na ukae siku kadhaa tu..
Waache huku wale wameshapata dili la maisha yao.. Wewe kafanye maandalizi ya kurudi tanzania.. PASPOT hii hapa..
Nakutakia kazi njema..
Alimaliza kuongea yule mzee nakunikabidhi bastola kisha nikafunikwa tena lile gunia usoni na kurudishwa kwenye gari..
Safari ilianza na kurudishwa hadi waliponichukua...
Wale wakaka waliniacha na kuniaga kisha wao wakaondoka...
Nilitembea kurudi ndani nikiwa na mawazo sana...
Niliingia na kuwakuta wale mapacha wamekumbatiana tu kwenye kochi wanaangalia Tv..
"Shosti.. Mlikuwa mnaongea nini masaa yote hayo..?? Sema yule kaka hensam.. Kama anataka mzigo mpe tu..
Aliongea Omera na kufanya wote tucheke...
Mmmmhhhhh. Kumbe hata hawajui kuwa nilitekwa na kurudishwa hapa.. Niliwaza kimya kimya na kushusha pumzi kisha kupita kuingia ndani kwangu..
Niliweka mezani kwangu zile ramani na picha za wahusika na kuanza kutazama kwa umakini sana..
Baada ya hapo niliamua kulala tu kwasababu nilikuwa nimechoka sana..
Asubuhi Omera alikuja kuniamsha tukanywe chai.. Tulienda lakini tulikuwa tukijadiliana kuhusu dili la mapacha wale njia nzama.
"Nyie kubalini ndio mwanzo wa kutusua maisha.. Mnatakiwa mrudi tanzania mkiwa matajiri bana..
Niliwapa ushauri na kukaa kimya. Niliona wameangaliana na kutabasam.. Baada ya muda walikubali na kuniomba tukitoka kwenye chai tuende nyumbani kwa INI..
Tulipata chai upesi na safari ikaanza..
Tulifika hadi pub na kumuulizia lakini tuliambiwa kama yupo katikati Lagos kwenye maduka yake ya nguo..
Tulipewa namba zake na kuwasiliana nae ili kumpa tarifa zile za kuwa tupo tayari na kazi zake....
INI alifurahi sana kupata habari zile.. Mda huo huo alituma tax itupeleke mjini..
Tulipelekwa hadi kwenye duka lake kubwa..
Duuuhhhh... Kuna watu wanamaisha jamani... Ojala aliongea..
Tulicheka tu na kuendelea kuingia ndani hadi alipo Ini..
"Your welcome My dear.. Karibuni sana wapendwa..
Aliongea Ini na kumshika mkono Omera na kutuambia tuwafuate nyuma..
Tuliingia chumba fulani dogo lenye nguo nyingi tolea jipya na kulikuwa na wadada kama 6 mule ndani..
"Dada unaweza kutupisha kidogo..
Aliongea Ini kuniambia mimi.. Nilikuwa nikimchukia sana yule dada kwasababu alinitenga sana.
Nilitoka na kuwaacha wajaribu zile nguo..
Baada ya Muda nilimuona ini akitoka kwenye kile chumba akiwa anachekacheka tu..
Alienda hadi mapokezi na kukaa kwa mda kidogo kisha akarudi na kunishika mkono pia kuelekea ndani walipo akina Ojala..
Jamani kwasasa mnaelekea saluni.. Mkatengenezwe nywele vizuri na kusafishwa kwa scrub nziri kwaajili ya maonyesho ya Mavazi yake mapyaa yatakayo fanyika usiku wa siku hiyo hiyo..
Mimi nilikuwa nawafuata tu kama mchungaji na mbuzi wake...
Walifikishwa kwenye saluni moja na kuingizwa.. Nilibaki kwenye gari nikiwa nachati tu na kusikiliza redio..
Tangazo kuu ilikuwa ni kuhusu maonyesho ya mavazi mapya yaliyotoka kwenye maduka ya INI..
Niliigia mtandaoni pia yalikuwa ni hayo tu..
Comment zilikuwa nyingi sana kwenye zile picha..
Kila mtu aliahidi kuwepo kwenye hayo maonyesho..
Walitoka akina Omera wakiwa wamependeza sana kisha tukapelekwa hadi kwetu kujiandaa na maonyesho ya usiku wa siku hiyo..
Tulifika tukiwa na furaha sana. Muda ulikuwa hauendi kabisa..
Tulikaa tunaangalia TV na kila baada ya madakika zilikuwa zikipita picha zaakima Omera kwenye TV.
Ilikuwa burudani ila iliniuma kwanini mimi tu sijaonekama kwenye TV
Jioni ilifika na kuanza kujiandaa.. Jua lilivyozama tu.. Alikuja INI na watu wake.. Walitupakia kwenye gari na kuelekea pub.. Mimi nilikuwa msindikizaji tu..
Tulifia na kuingizwa kwenye chumba fulani. Omera na ojala walianza kuvalishwa vazi la kwanza na wakati huo watu walikuwa ni wengi sana njee kwenye ukumbi kusubiri maonyesho....
Baada ya muda walifika na kupigiwa shangwe sana.. Walipigwa picha nyingi sana..
Baada ya mda walirudi ndani wakiwa sare.. Hapo mwenyewe nilichanganyikiwa nilikuwa simjui Omera ni nani na Ojala ni nani...
Walivua zile ngo ila bado walinichanganya. Walivaa zingine na kurudi ukumbini..
Walishangiliwa sana.. Yalikuwa ni mavazi kama matano hivi..
Waliiingia na kutoka hadi wakamaliza..
Baada ya lile zoezi la mwisho kukamilika niliona kimya na akina Omera hawakurudi ndani..
Ghafla nilisikia simu yangu inaita .
Alikuwa ojala kanipigia..
"shost tupo kwenye gari twarudi home.. Panda bajaji utatukuta .
"hahahahaha... Nishatengwa hapa hadi lift nanyimwa....
Nilitoka na kupanda bajaji kuelekea nyumbani...
Lakini nikiwa njiani nilishanga kuona kuna magari kama manne yamezingira gari moja na kushuka vijana kama kumi..
Baadae alishuka mzee mmoja.. Nilimwangalia vizuri na kugundua ni yule mzee ambaye alikuwa anasema aliibiwa na Ojala siku kadhaa zilizopita na kusababisha Omera aende polisi..
Walienda hadi kwenye gari na kuwashusha Omera na ojala kisha kuwapakia kwenye gari lao na kuondoka
Nilihisi kuchanganyikiwa.. Nilimwambia jamaa wa bajaji afuate yale magari hadi yatakapoingia...
Nilifika hadi hapo na kuanza kuangalia yele mazingira.. Ilikuwa ni nyumba kubwa sana..
Nilimlipa jamaa wa bajaji kisha nikaendelea kuangalia...
Niligundua nyumba inao ulinzi mkali sana.. Niliwaza kwenda home kuchukua bastola lakini moyo uliniuma sana...
Niliita tax na kukimbia upesi.. Nilichukua bastola yangu yapili niliyopewa na yule mzee kwasababu yakwanza nilinyang'anywa na Renatusi na kumuulia mwanangu..
Nilirudi na kuruka ukuta kisha kuingia hadi ndani..
Niliingia kwenye kila chumba kwa siri bila mafanikio..
Niliichungulia kwenye chumba fula kwa dirisha na kuona wapo wanaume kama sita wapo matumbo njee na wanavuja jasho..
Nilijua huenda walikuwa wapo kwenye mazoezi...
Lakini haikuwa hivyo... Nilichungulia vizuri na kumuona Omera sijui ni Ojala yule yupo pale chini anavuja tu dam sehemu za siri na amelegea kama mtu aliekufa ..
Nilizunguka haraka na kuuvunja mlango na kuingia hadi ndani... Alikuja kaka mmoja na kunirushia ngumi..
Nilimdaka mkono na kuuvunja.. Wenzie baada ya kuona vile walikuja wote huku wanapiga kelele...
ITAENDELEAA..

No comments: