π’πˆπŒπ”π‹πˆπ™πˆ: ππˆπ“π€πŠπ”π…π€ 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ππ†π” 𝐄𝐏.... 45






π’πŽππ†π€ ππ€π˜πŽ....
Nilizunguka haraka na kuuvunja mlango na kuingia hadi ndani... Alikuja kaka mmoja na kunirushia ngumi..
Nilimdaka mkono na kuuvunja.. Wenzie baada ya kuona vile walikuja wote huku wanapiga kelele...

Nilikuwa nimechafukwa.. Nilikuwa nikiwashika wawili wawili na kuwapiga kama vile napigana na watoto.. Hawakuamini nini kilitokea pale..

Baada ya dakika kama tatu tu wote walikuwa chini wanaugulia maumivu.. Nilikuwa nikiwapiga sehemu muhimu tu....

Kama vile sehemu za Kwenye viwiko na kwenye joint na misuli ambayo nilikuwa nikijua maumivu yake hawawezi kuyamudu..

Nilienda hadi alipo rafikiangu na kumuona kwa haraka alikuwa amepoteza maisha....

Sikujua ni nani kati ya Omera au Ojala nsio kafa kwasababu nguo walivaa sare...

Niliinuka na kumfuata jamaa mmoja aliekuwa akiugulia sana kwa maumuvi na kuanza kumminya sehemu aliyokuwa akiishika hasa..

Nilikuwa  nimempiga teke ya korodani.. Kwahiyo mda wote alikuwa amejikunja analia..

Niliyashika yale magololi na kuyaminya zaidi..

"Yupo wapi yule mwanamke mwingine.. Au mmemuua.?  Niliuliza kwa ukali sana kwa lugha ya kiingeeeza...

I don't know where she is" aliogea yule jamaa akiniambia hajui yupo wapi..

Nilikuwa nimechukia sana.. Niliendelea kumminya lile koridani kwa nguvu hadi akanionyesha chumba cha tatu kutokea pale kwa ishara...

Nilicheka na kumwambia.. "I am coming back soon. Narudi mda si mrefu...

Nilitoka na kaenda hadi kwenye hicho chumba na kumkuta mwenzangu  amekaa tu chini...

"Omera yupo wapi.???
Alidakia yule dada baada ya kuniona nimeingia mule ndani...

Hapo ndio nikatambua yule aliopo ni Ojala na Omera ndio hivyo hatunae tema..

Nilishusha kilio kwa kwikwi sana nikimkumbuka rafikiangu..

Nilikumbuka mangi sana nikiwa na Omera.. Yeye ndio alinitoa Tanzania kunileta huku..

Yeye ndio alinisaidia siku nataka kuuliwa na RC .

Yeye ndio alinisaidia baada ha kunikuta nahangaika sokoni..

Nitamwambia nini mama yake omera mimi jamani..??

Nilijikuta naropoka na kuanza kulia..

Ojala aliinuka pale chini na kunisogelea hadi niliposimama.. "We Hajra.. Unamaanisha dada kauliwa.????

Omera alilia sana na kunikumbatia...

Tukiwa bado tunalia nilisikia minong'ono ya watu wanakuja tulipo..

Nilimshika Ojala mdomo na kumbana kwenye kona.. Alikuja mzee mmoja na askari kama watatu...

Nilimtazama na kumtambua ni yule mzee aliewahi kumuweka jela Omera na usiku huo ndio alihusika na kuwateka rafiki zangu..

Niliinuka na kupaa kwa spidi sana na kutua kwenye kifua cha yule mzee.. Nilimkanyaga na moja kwa moja alidondoka chini..

Nilimshika kichwa na kumvunja shingo..

Niligeuka nyuma sikuwaona tena wale askari... Ojala akiwa analia alikuja kunishika akiwa hana nguvu kabisa..

Nilimshika mkono na kuelekea chumba nilichomwacha Omera.. Alimwangalia ndugu yake na kujiridhisha kuwa kweli ameshakufa .

Ghafla simu yangu iliita.. Ilikuwa ni namba ya Mkuu wangu..
"Njoo hapa njee upesi Hajraaa..
Ilikuwa sauti imesikika baada ya kupokea tu simu..

Nilichungulia na kuwaona wamesimama kwenye gari njee..

Nilimshika Ojala na kutoka upesi.  Tulipanda gari na safati ikaanza.. Nilifika hadi kwenye nyumba ambayo walinipeleka juzi...

Tuliingia hadi ndani pia.. Kulikuwemo na wanajeshi wengi sana pia... Tulienda kwenye chumba cha siri sana..

"Hajraa.. Kama nilivyokwambia Kajiandae na kesho utarudi Tanzania.. Huyu mwenzio atabaki hapa kupata mafunzo kwasababu tulihamishia kambi zetu huku afrika..

Kule urusi eneo  ni ndogo pia palitokea mkwaruzano kati ya Urusi na marekani...
Tukaamua kurudi afrika..

Ojala wewe utabaki hapa na kuanzia leo unaanza mafunzo.. Baada ya miezi sita utaenda Tanzania kumuongezea nguvu mwenzio...

***
***

Kweli kesho yake nilianza safari kutudi Tanzania kwasababu nilikuwa na mahitaji yote..

Nilingikia Tanzania majira ya saa 12 jioni.. Nilikodi Tax hadi kinondoni na kuchukua chumba... Nilioga na kwenda kutafuta chakula usiku ulee..

Kidogo nilikuwa nimebadilika kwani mavazi ya kujisitiri nilikuwa nikishindwa kuvaa kwasababu ya kazi zangu.. Mda mwingi nivaa suruali...

Na jioni ile kweli nilikuwa nimevaa suruali nyeusi na blauzi nyepesi ya kahawia.. Blauzi ilikuwa kama chekecheke vile.. Nikikaa kwenye mwanga mtu alikuwa akiniona hadi tumbo..

Kwasababu maziwa yalishaanza kudondoka niliamua kuvaa Braa nyeupee ambayo ilinipa sapoti kuyainua maziwa yangu na kuyaweka sawa...

Niliingika sehemu na kula chakula.. Sikujua hata ile bar ilikuwa inaitwaje.

Yaani kwajinsi nilivyovaa nilikuwa nipo kimalayamalaya tu... Hata mtu angenikuta pale asingeweza kunitofautisha na makahaba..

Niliagiza kuku na grand malt na kutulia kwenye kona nakula.. Kile kilikuwa ndio chakula changu kikuu..

Nilimaliza kula na kumuita mhudumu... Nilifungua pochi ili nimlipe lakini aliniambia kuwa kuna kaka ameshanilipia..

Niligeuka na kutazama upande nilioelekezwa na kumuona mkaka fulani ananichekea . Alikuwa na kitambia sana hadi nikajikuta namcheka lakini yeye alihisi huenda mimi nimefurahia alivyonilipia..

Aliinuka na kuja kunifuata akiwa na majamaa fulani wawili nadhani ni mabaunsa wake wale..

"Daada mambo.. Aliongea yule kaka..
Tayari nimekulipia.. Pia kama hutojali naomba nikupeleke kwako.. Mimi ndio RC mpya.. Mr RENATUS aliacha kazi na kuamua kuwa mlokole na sasa analo kanisa lake kubwa sana..

Nijikuta nacheka kusikia jamaa ni amekuwa Nabii sasaivi na analo kanisa..

Baada ya kusikia kuwa yule kaka ndio mkuu wa mkoa kwa sasa niliamua tu kujilainisha..

Tulikubaliana na kuongozana hadi kwangu nikachukua begi langu na kwenda nae mikocheni kwenye nyumba yake

Alikuwa na nyumba kubwa sana pia..

Tulipaki gari na kushuka kuelekea ndanii.. Kulikuwa na magari mengi sana pale nyumbani kwake...

Katiaka kupitapita niliona Gari langu la miaka kadhaa nyuma niliyoinunuaga lakini niliiachaga nyumbani kwa Renatus..

Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio sana.. Niliamini Renatus anaweza kuwepo yale maeneo.. Na nilikuwa nikimwogopa sama tangu alivyonipiga..

Nilitembea kwa mwendo wa haraka sana kwa kujifichaficha ilimradi tuingie tu chumbani..

Kweli tulifanikiwa na kufika hadi sebuleni.. Kulikuwa kumetulia sana.. Hapakuwa na mtu..

"Baby.. Naomba tukawasalimie wageni wangu wapo hapa kwenye glosery wanakunywa.. Yupo na mkuu wa mkoa mstaafu .. Siunajua ameokoka kwahiyo anakunywa kwa kujificha sana..

Duuuhhhh.. Nilishusha pumzi kidogo na kumwangalia yule jamaa.

"Hapana kwasasa nimechoka na sana. Naomba nipeleke tu chumbani nioge nipumzike alafu wewe utaenda kuongea nao tu...
Nilimwambia yule kaka.

Tulifika chumbani na kuweka begi langu kitandani.. Nilitazama meza ya yule jamaa ilikuwa imejaa pakiti ya madawa ya kulevya..

Mmmhhh.. Hii ndio meza ya mkuu wa mkoa.. Niliguna kidogo na kujifanya kama sijaona kitu..

Alinionyesha bafu na namna ya kufungua maji..

"haya baby.. Wewe oga acha mimi nikashtue kidogo.. Au nikuletee na wewe ushtue..??

Aliongea yule jamaa na kuja kunishika kiuno.. Nilimtazama na wakati anatoka tu nilimfinya kidogo mgongo..

Ile anageuka  alikutana na ngumi zito kwenye taya akadondoka chini..

Nilimfuata na kumvunja shingo.. Nilimpandisha kitandani na kumlaza kisha kumfunika...

Nilitoka na kwenda hadi sebuleni sikuona mtu.. Niliona kuna miwani ya tinted pale mezani na kuivaa... Niliweka vizuri begi mgongoni na kuanza kutoka..

Nikiwa napiga hatua za haraka na kufungua mlango.. Kabla sijamalizia kutoka nilisikia mtu nyumaangu...

"we dada njoo hapa..' ikikuwa ni sauti ya renatus kabisa..

Niliwaza sana nafanyaje.... Nilitamani kugeuka nyuma ila angenitambua.. Alizidi kunisogelea kwa mwendo wa kunyata akiwa kashika bastola.. Nilikuwa nikimuona tu kwenye kivuli alichokuwa akimulikwa na taa .

ITAENDELEA...






No comments: