ππππππππ: πππππππ π ππ ππππππ πππππ ππ.... 46 & 47
πππππ ππππ....
Niliwaza sana nafanyaje.... Niliwaza kugeuka nyuma ila angenitambua.. Alizidi kunisogelea kwa mwendo wa kunyata akiwa kashika bastola.. Nilikuwa nikimuona tu kwenye kivuli alichokuwa akimulikwa na taa .
"Mkuu.. Samahani wale wageni wanataka kuondoka... Nilisikia sauti ya mhudumu wa pale akimwambia RC..
Rc aligeuka nyuma na kabla hajanigeukia tena nilipo nilishapaa na kuuruka ule ukuta..
Nilikimbia mwendo sana.. Na baada ya umbali fulani nilipanda Tax hadi hotelini...
Niliweka sawa mabegi yangu na kuoga kisha kulala..
Asubuhi niliwasha TV na kuangalia habari kuu kwa asubuhi ile na baadhi ya uchambuzi wa magazeti..
Moja ya habari iliyosumbua ilihusu kifo cha mkuu wa mkoa..
Nyingene niliona imeandika kuwa..
"NABII RENATUS APOKEA KWA MASIKITIKO KIFO CHA MKUU WA MKOA...
nilicheka na kuzima TV
Nilitoka na kwenda kutafuta chai asubuhi ile lakini kwa umakini sana kwasababu kulikuwa na askari wengi mjini..
Nilikunywa chai na kurudi kulala ili usiku nikaendelee na majukumu mengine..
***
***
UJININI..
Mama Omera.. Wanaetu wanarudi lini.?? Karibu mwezi watatu huu siwaoni..
Na ulisema umewaagiza duniani...
Aliongea baba yake Omera..
"mama yake omera alinyama kimya kidogo na kumwambia mme wake kuwa asubuhi atasafiri kwenda kuwaleta.
Walilala usiku ule lakini wakiwa na mawazo sana..
Kweli palivyokucha tu yule mama alifunga safari hadi Nigeria kuwatafuta wanae..
Alitumia nguvu ya kijini kujua walipo lakini hakuweza kupata mawasiliano nao..
Inamaana wamekufa wanangu.??..
Aliongea yule mama...
"mbona siwapati...??
Mama hakuwa na mawazo hata kidogo kuhusu wanae kuwa wanadamu..
Moja kwamoja alihisi wamekufa
Mama alikaa tu chumbani akiwa analia lakini ghafla alisikia harufu za marashi na nguvu kubwa inaenda kumkaba..
Kwa uzoefu wake mama alitumia nguvi nyingi sana kujinasua kwasababu alishajua michezo yote..
"Tungekunyanganya nguvu zote uwe kama wanao..
Sauti ilisikika ikiongea baada ya mama kuwazidi nguvu..
Hapo mama ndio alijua fika kuwa wanae hawakufa ila wamekuwa tu ni wanadamu..
Mama alianza kuzunguka kila kona ya jiji akiwatafuta wanae bila mafanikio..
Siku yakwanza ilipita bila mafanikio..
Siku ya pili alihisi kama harufu ya Ojala mahali fulani..
Mama alifunga safari na kwenda kama upepo..
Ilikuwa ni kambi ya kijeshi.. Alimkuta mwanae yupo kwenye mazoezi makali sana..
Mama alishuka kama upepo na kumpulizia mwanae nguvu..
Ojala akiwa kwenye mazoezi na wenzie alishangaa anakuwa mzito sana na kudondoka chini..
Wenzie wote walikusanyika kumpepeaa..
Baada ya mda Ojala aliinuka akiwa na maono ya kijini..
Alifurahi sana kumuona mama yake..
Aliita tu mamaaaaa.. Na kupotea kinafsi kisha kuacha mwili unapepewa tu pale chini..
Wanajeshi walimbeba na kumpakia kwenye ambulance kumpeleka hospitali..
Kumbe waliubeba mwili tu ila nafsi ilikuwa inaongea na mama yake...
***
"Mamaaa.. Ulitutelekeza sana mamaangu. Nimeteseka kwenye huu mji.. Pamoja na changamoto zote lakino mimi natamani niendelee kubaki duniani..
Ninayo majukumu makubwa sana mama, ila mwisho wa siku nakuahidi nitarudi na Saidi akiwa ameukomboa mtandao wake wa giza..
Kwasasa naandaliwa kwa kazi kubwa sana kule Tanzania..
Aliongea Ojala huku anamtazama mama yake..
'mbona unaongea tu Ojala.? Mwanangu Omera yupo wapii.??
"Mama.. Samahani sana.. Omera hatunae tena... Alibakwa na kupoteza maisha..
Yule mama kusikia vile alihisi kuchanganyikiwa..
Mikono ya yule mama iliwaka moto na macho yake.
Alikuwa na hasira sana..
Waliongea na mambo mengine kwa muda mrefu..
Baada ya mda yule mama alimwongezea mwanae nguvu kisha yeye akapotea kurudi ujinini..
Dakika kadhaa tu wakiwa hospitalini Omera aliamka baada ya nafsi yake kurudi mwilini..
wanajeshi walishtuka sana kuona mwenzao aliekuwa hoi kainuka na kutembea..
Walirudi zoezini na kuendelea na mazoezi..
***
***
Mchana wa leo RC renatus alikuwa bize uwanja wa ndege akipokea mizigo yake ya madumu yenye maji ya upako..
Hakuwa akiwaza hata kifo cha mwenziee..
Nabii Renatus alipeleka nyumbani mizigo yake kwaajili ya muujiza wa ibada ya jumapili..
Kumbe alikuwa akiagiza maji ya maombi nchini nigeria kwa waganga wa jadi...
Alikuwa na kanisa kubwa sana hasa kilibebwa kwa umaarufu wa kazi yake ya awali..
Alipotosha uma na kuwaambia Mungu kamuita amtendee kazi yake na aache kazi ya ukuu wa mkoa...
Aliaminika sana hasa kwa muujiza wake..
Viziwi walisikia..
Vilema walitembea..
Vipofu waliona..
Na kila mwenye tatizo alikuwa akitatuliwa pale pale..
Lile jambo lilimuongezea umaarufu mkubwa sana Renatu..
Alifuatwa na watu kutoka mikoani hasa vijiji masikini na kwenda kwa nabii waombewe wapate pesa..
Jumapili ilifika na watu walijaa sana kwenye viwanja vya shule ya msingi Ndugumbi pale magomeni..
Nabii alifika akiwa na walinzi wakutosha..
Aliponya na kusoma baadhi ya mafungu ya biblia ili kuaminisha watu na kuondoka zake..
Sadaka zilikuwa zikihifadhiwa kwa kiongozi wa kwaya Mama Masanja...
Hivyo basi baada ya kumalizika majukumu yake nyumbani.. Alipitia kwa mama masanja.. Ili kujua ni sadaka kiasi gani kipo...
Alifika na kupiga honi kwa muda mrefu sana na haikuwa kawaida yake..
Baada ya kuona kimya aliamua kushuka na kwenda mwenyewe hadi ndani..
Alishtuka sana kukuta mama masanja ameuliwa na amelazwa kwenye kona nyuma ya kochi..
RC alimpima na kugundua alikufa kwa kuvunjwa shingo..
"what is this.. Alisema RC..
Inamaana Hajra anacheza na mimi.??
Aliongea RC na kuondoka zake kuelekea polisi..
Alijua kabisa hakuna mwingine wakufanya vile tofauti na Hajra..
***
***
Baada ya kumuua yule Mtunza fedha wa Rc nilishika sim yangu na kumtumia ujume RC..
"Nimerudi baba.. Lazima ufe sasa..
Niliituma ile meseg lakini ilikaaa mda sana bila kujibiwa.
Nilikusanya zile fedha na kwenda Azania kituo cha yatima..
Nilinunua vitu na kuwapelekea watoto yatima..
Watoto walifurahi na kuniimbia nyimba nyingi zakunieka sawa..
Nikiwa natoka alikuja mtoto mmoja na kunishika miguu..
"mama naomba nisadie mimi.
Aliongea yule mtoto..
"unaitwa nani.?
'Mwalimu aliniambia mimi naitwa Ciprian Nicson..
Nilimshika yule mtoto na kumtazama alikuwa amefanana sana na nic..
"Au ndio yule mtoto wa nic aliezaaga na Monika.??..
Nilimtazama tena na kuiona sura ya Nic yote kwa yule mtoto..
Nilimhurumia sana yule malaika..
Niliongea na waalimu wake na kwenda kusaini kuwa namchukua yule mtoto..
ππ.... 47
Nilikubaliwa na kuondoka nae hadi hotelini nilipokuwa nikiishi...
Mcha huo nilitafuta dalali na kutafuta nyumba..
Nilibahatika kupata nyumba yenye vyumba viwili na sebule na jiko....
Vilikuwa vyumba vya kisasa sana.. Nilianza maisha yangu mapya na kijana yule...
Nilimtafutia shule na kutwa nzima alikuwa akienda shuleni na kurudi usiku...
Mtoto kadiri siku zilivyozidi kwenda alizidi kukua sana na mwonekano wake alikuwa ni kama Nic kabis kuanzia kuongea hadi tabia.. Kutembea ndio kama baba yake kabisaa..
Kila siku nilikuwa nikipokea kesi za Cyprian kuwapiga wenzie shule..
Mara kanyang'anya mwenzie daftari.. Mara kawatisha wenzie kuwaua...
Yaani alikuwa ni mkorofi kupita maelezo.. Ilifikia hatua hata nikaanza kujuta kwanini nilimchukua yule mtoto..
Nilikuwa nikijitahidi kumpa malezi mazuri ila bado hali ilikua ngumu.. Mwishoe niliamua kumpeleka kwenye shule ya watoto watukutu iliyopo manyara.. "Manyara rengers"
Kidogo nidhamu ilianza kumjia kulingana na kuchapwa na uangalizi mkubwa aliokuwa akiupata kule tofauti na hapa nyumbani..
Nilishukuru sana kuona Cyprian au kifupi nilipenda kumuita (Rian) anaendelea vyema..
Matokeo yake pia yalikuwa yakiridhisha sana hadi kupewa uongozi na walimu wake..
Nilitenga siku moja na kwenda kwenye kile kituo cha watoto yatima nilipomtoaga Rian mwanzoni..
Nilienda kufuatilia taarifa zake ili nijue ilikuaje hadi akaigia pale..
Nilifanikiwa kukutana na mkuu wa kitu kile..
***
'habari mama.. Sidhani kama unanikumbuka ila mwaka mmoja nyuma nilikuja hapa na kuondoka na kijana mmoja aitwae Cyprian..
Niliongea na kumtazama yule mama..
"Nakukumbuka bintiangu.. Nakumbuka ulituachia fedha nyingi sana za kuendeshea taasisi yetu hii..
Nashukuru kukuona pia kwasababu kwasasa taasisi yetu inakabiliana na changamoto nyingi kubwa sana.
Nilinyamaza kimya nikimsikiliza.. Nilijua tu mbongo ukishamsaidia siku akikuona tena anajua ni msaada umekuja.. Ataanza kukulia shida hadi ujute...
"Mwanangu.. Kwasasa hatuna hata fedha za mradi wetu huu. Wafanyakazi wameacha kazi.. Na baadhi ya watoto wametoroka na wengine kupotea katika mazingi ya kutatanisha..
Mwanangu siendeshi huu mradi kwa maslahi bali kusaidia tu watu na upendo wangu kwa watoto yatima.
Huwezi kuamini sasa nimebaki na watoto 15 tu wakati mwanzo nilikuwa na watoto zaidi ya 80..
Nateseka mwanangu unavyoona hawa watoto wanashinda njaa na kukosa huduma...
Nilinyamaza kimya nikiendelea kumsikiliza yule mama huku napiga mahesabu ya chakula cha wale watoto kwa siku..
Kwa hesabu ya haraka ya mtoto mmoja kula kwa siku ilikuwa ni kama 5000 ambayo kwa mwaka ingekuwa kama milioni 27.375
Haikuwa fedha za kunisumbua kwa wakati ule.
***
Sawa mama itapatika hizo fedha.. Naomba usilie basi mama..
Amani yako itarejea mamaangu.. Nitausimamia huu mradi wako na kukutafutia wafadhili wakukujengea hata madarasa ya shule na kuajiri baadhi ya walimu uanze masomo hapa..
Mama alifurahi sana.. Nilitoa cheki na kumuandikia milioni 60 akachukue benk..
Yakumsaidi hata kwa mwaka mmoja na nusu...
Mama alionekana kweli anao uhitaji mkubwa sana wa msaada..
*
"Nashukuru mwanangu najua unahitaji nini kwangu..
Cyptian aliletwa hapa na RC mstaafu mr Renatus, aliletwa akiwa mtoto mdogo sana..
Renatus aliniambia kuwa yule mtoto alitelekezwa na mama yake..
Wakati huo huumradi ulikuwa chini yake akiuhudia kuanzia mwanzo kwasababu kuna mjomba wake tuliwahi kumlea hapa hadi akawa mwanajeshi..
Nicson alikuwa kijana mtulivu sana ila baada ya kumaliza masomo yake alichukuliwa na mjomba wake na kwenda jeshini..
Hapo ndio nilianza kujua kuwa Nic pia alikulia kwenye hii hii taasisi ambaye aliletwa mwanae..
Baada ya kuchukuliwa na mjomba wake hapo alianza ujasusi wa kila aina.. Uuzaji wa madawa ya kulevya na uuaji wa watu na kuuza viungo kama figo na macho...
Pia walikuwa wakiwakuza watoto kwa mda fulani na baadae kuwauza kwenye mataifa makubwa kama urusi na marekani..
Walijua kuwa watoto hawa hawana wazazi hivyo wanawachukua watakavyo na kuwatumia kujiingizia vipato..
**
Mmmmhhhhhh.. Niliguna na kukaa vizuri..
"Mama kwanza ulijuaje kama mimi hitaji langu ni hilo.??
Niliongea na kumtazama mama kwa umakini sana..
'mwanangu.. Najua hakuna mtu anaweza nunua kitu bila kuangali ni wapi kimetengenezewa..
Unaweza kununua simu bila kujua kinetengenezwa wapi.?? Aliniuliza mama.
" hapana mama siwezi....
Nilijibu na kucheka.
" Hivyo ndivyo inakuwa... Nilijua ungekuja mda mrefu sana lakini nashangaa umekaa hadi mwaka umepita..
Nilikuwa najua ukorofi wa mtoto yule na nilijua angekushinda na ungemrudisha..
"Hahahhaahah.. Kweli mama yule Rean ni mkorofi sana.. Kila siku nilikuwa nikisuluhisha kesi.
Kila siku nilikuwa nikilipa fidia za uharibifu wake shuleni..
Lakini baadae niliamua kumpeleka kwenye shule ya watoto watukutu.. Kwasasa ananidham sana.. Akija likizo nitamleta akusalimie
Alifurahi sana yule mama kusikia vile..
"Mamaa.. Tunampata vipi Renatus..? Nahitaji kumuua yule mtu,
Niliongea na kumtazama mama atalipokea vipi lile suala..
" Hajra mwanangu... Muue yule mtu.. Anaangamiza taifa tafadhali mwanangu.. Nakuomba sanaa..
Aliongea yule mama kwa hisia sana..
Mwanangu.. Naomba nisamehe kwa nitakacho kuonyesha..
Aliongea yule mama na kunyanyua juu gauni lake..
" Mwanangu unaona natembea na nepi kama mtoto.??
Mwanangu hapa nimeshajinyea na kujikojolea bila hata kujua mwanangu..
Baada ya wewe kuondoka na Cypria. Alikuja Renatus wiki moja baadae...
Aliulizia alipo huyo mtoto..
Nilimwambia sijui kaenda wapi.. Nilimjibu vile kwasababu ya kukulinda wewe...
Kile kitendo kilimuudhi sana na kusitisha msaada hapa kwenye taasisi yetu...
Aliona haitoshi kutotusaidia lakini baadae aliamua kunitumia mabaunsa kama nane..
Waliniteka na kunibaka.. Waliniingilia kinyume na maumbile hadi sehemu ndogo ya utombo wangu kutoka njee..
Nilikaribia kufa mwanangu.. Nadhani Mungu kanisitiri ili hawa watoto ninao walea wapate kuishi..
Nilitibiwa lakini ndio hivyo hadi sasa kila haja inanitoka bila kujua..
Alimaliza kuongea yule mama na kujifunika..
Wakati huo mimi uso mzima ulikuwa mbichi kwa kuloa machozi..
Nadhani hakuna siku nimelia kiasi kile tangu nimezaliwa...
"Mwanangu... Muue Renatu.. na Mungu atakubariki sana mwanangu..
Nitakuombea usiku na mchana...
Niliinuka nikiwa nalia na kupanda gari langu kurudi nyumbani..
Njia nzima nilikuwa nikiwaza unyama alio fanywa mama wa watu kwaajili yangu...
Nilikuwa nikijilaumu sana kwa kazi hii ngumu niliyoamua kuifanya.. Nilijikuta naanza kumkufuru hata Mwenyezi Mungu kwa madhila haya aliyopanga niyapitie..
ITAENDELEA....

No comments: