HADITHI: RED BIKINI SEHEMU YA 17.





ILIPOISHIA👉🏽 Mrs Dango akiwa na mchepuko wake wakila raha. ENDELEA 👇🏽

"Frank! Jamani mbona unanifanya nisiwe na hamu hata ya kumuona Mme wangu?"
"Hahahaha usijali mbona kawaida mpenzi wangu." Huku akimuweka vizuri kitandani apate kumkandamiza vizuri kwenye kona ya kitanda.

**********
"Nimesema huwezi ukanipangia muda wa kurudi hapa ndani."
"Hivi nani ni mwanaume humu ndani?"
"Mwanaume? Mwanaume gani unayemzungumzia humu ndani?" Huku akikaa kwenye kitandan.

"Hivi kwa akili yako, wanaume watoke mbele nawewe utatoka? Unajiona unasifa za kiume?"
"Dah! Naona mke wangu leo umeamua kunitukana?"
"Sikutukani ila ndio ukweli huo." Huku akijilaza kitandani.
"Nataka nipumzike sihitaji kelele zako."

Mr Dango alibaki akimuangalia mkewe na asijue amfanye nini kwa maana alijikuta akijawa na hasira moyoni. Akiwa bado anamshangaa mkewe mara simu ya mkewe ikaita na haraka haraka Mr Dango aliiwahi na kuipokea.

Mkewe akawa anamuangalia huku akitabasamu tu bila kutia neno lolote.
"Yes hellow!"
"Samahani namuhitaji mwenye simu?" Sauti ya Frank ilisikika.
"Wewe nani unayemuhitaji mke wa mtu muda huu?" Mr Dango aliuliza kwa sauti ya ukali kidogo.
"Brother! Mbona unakuwa mkali kiasi hiko? Tuepushe tu mgogoro namuomba mwenye simu hiyo niongee nae."

Pale pale mkewe akaidaka simu na kuongea na Frank.
"Yes darling!" Huku akirembua jicho lake na kumuangalia mmewe kwa dharau.
"Dah! Eeh! Mungu sina wakumshtakia zaidi yako naomba unilinde na hasira maana nisije fanya kitu cha ajabu na jamii nzima ikanishangaa." Kisha akafungua mlango na kutoka nje.
"Mmmh! Nimefika salama mpenzi wangu." Mrs Dango alizungumza kwa kujiamini zaidi.

***********
Baada ya miezi kadhaa kupita Mrs Dango alipata ujauzito na kwa haraka haraka ulikuwa ujauzito wa wa Frank na ukaleta mtafaruku mkubwa pale nyumbani.

"Nazani hiko ndicho ulichokuwa unakitaka muda mrefu?" Mr Dango alimuuliza mkewe.
"Kwani shida iko wapi?"
"Shida iko wapi? Inamaana unaona ni sawa tu kwa upande wako?"
"Unajua unataka kunichekesha."
"Mke wa mtu kupata ujauzito nje ya ndoa? Halafu unasema hakuna shida?"

"Kwani nani atakaye jua hilo suala? Au umesahau kitanda hakizai haramu?" Huku akijikalisha kwenye sofa.
"Huna akili leo nimeamini ase, katika wanawake wapumbavu duniani basi wewe ndio mwalimu wao." Huku akiandaa chakula mezani baada ya kupika. Yani Mr Dango alifanywa kama ndio mpishi ama house boy.

"Yani nakushangaa sana kelele nyingi utazani wewe ndiye utakaye hudumia hii mimba, una hela kwanza za kuhudumia wewe?" Huku akimuangalia kwa jicho la dharau.

"Sawa sina ila utakuja nikumbuka ipo siku."

**********
Siku ya siku Mr Dango akitoka kwenye mihangaiko yake ya kutafuta kibarua akakutana na jambo la ajabu ndani kwake. Ilimbidi abaki ameduwaa tu bila kuzungumza chochote kwa maana ilikuwa ishafikia hatua mbaya.

"Vipi mbona umesimama kutushangaa?" Mkewe alimuuliza mmewe huku akiwa amelala miguuni mwa Frank.
"Karibu brother!" Frank alimkaribisha kinafki.

"Yani mmeaona haitoshi huko mlikokuwa mnafanya uchafu wenu, sasa mmeamua kuja kuufanya mbele ya macho yangu?" Huku chozi likitaka kumtoka.

"Wewe bado ni kijana mdogo sana tena sana, na una safari ndefu ya maisha jua haya unayonifanyia mimi ipo siku yatakuridia na namuomba Mungu akujibu angali tuhai." Huku akilia kwa uchungu na kukaa kwenye sofa akimuangalia mkewe.

"Babby! Tuondoke hapa tuwapishe watu na nyumba zao." Mrs Dango alizungumza huku akinyanyuka na kumtaka frank anyanyuke pia. Walijiandaa wanavyojua kisha wakaanza safari ya kutoka.

"Haya mbaba tunakuachia nyumba yako." Huku akisimama mbele ya mmewe.
"Brother tunaenda sisi!"
"Mke wangu unaweza ukaniambia unaelekea wapi?"
"Kha! Kwani unahitaji nini? Si umetaka tukajifiche usituone? Ndio tunaenda hivi." Kisha wakaondoka zao wakimuacha Mr Dango akiwa amebaki na maumivu yake.

Ulipita mwezi mzima bila mkewe kurudi nyumbani huku Mr Dango akiwa haelewi aanzie wapi kumtafuta mpaka siku aliporudi mwenyewe.

Maisha yaliendelea kama kawaida kwa wanandoa hao wawili kwa kuishi kwa msuguano mpaka ilipofikia siku mkewe anajifungua mtoto wa kiume ambaye kwasasa ndiye tuliyemuona anaitwa Edwin.

Mr Dango ilikuwa ikimuuma sana moyoni lakini alishindwa cha kufanya hadi pale siku alipoamua kumtoroka mkewe na kumuachia nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe kipindi alipokuwa ana kazi. Miaka mingi ilikatika mpaka Edwin alipofikisha miaka ya kwenda shule lakini Mr Dango hakurudi.

Mahusiano ya Mrs Dango na mpenzi wake Frank yalivunjika baada ya kugundua yule jamaa alikuwa ana mke na mtoto mmoja wa kike aitwae Irene na ndiye mpenzi wa Mr Dango na Edwin mwenyewe.

Unaambiwa Mr Dango alirudi kwa ajili ya kufanya malipizi kwa Frank kwa kutembea na binti yake.

**********
"Habari yako binti?" Huku akisiamamisha gari yake pembeni ya Irene aliyekuwa anatoka shule. Alikuwa bado ni binti mdogo mwenye kuvutia mbele ya wanaume rijali.
"Nzuri shikamoo?"
"Marhaba." Huku akitabasamu.

Mr Dango huyu alikuwa ni tofauti sana na yule aliyekuwa akipelekeshwa na mkewe, kwa maana alipokimbia familia yake aliamua kwenda mugodini kutafuta maisha. Na mungu alimsimamia mpaka mwisho wa siku alifanikiwa kupata maisha na kuamua kurudi tena jijini lakini akiwa amenunua nyumba masaki akiishi kama mfalme.

Alikuwa anapesa chafu ambazo alizitumia kuponda starehe na kufanya miradi yake mingine.

"Samahani, wewe ndiye Irene?" Swali lililomshtua kidogo Irene.
"Yeah ndio mimi!" Alimjibu kwa mshangao.
"Kwani wewe nani?"
"Usijali utanifahamu tu!" Huku akifungua droo kwenye dashboard na kutoa noti nyekundu kama tano hivi na kumpatia Irene.

"Zanini sasa hizi?"
"Kuna kazi nahitaji unisaidie."
"Kazi gani!?"
"Usiwe na haraka kiasi hiko binti, nazani nitakutafuta weekend ili nikueleze kazi yangu ninayohitaji unisaide." Huku akipandisha kioo cha gari na kuondoa gari yake kwa fujo.

"Irene vipi?" Edwin aliuliza huku akiwa nayeye anatokea shule.
"Safi vipi?"
"Fresh! Mbona uneduwaa na umeshika mpunga wa maana mkononi?" Edwin aliuliza huku akiziangalia zile pesa zilizokuwa mkononi mwa Irene.
"Hapana kawaida!" Huku akiziweka kwenye begi lake la madaftari kisha wakaondoka zao.

**********
"Samahani lakini mzee wangu, ulisema kuna kazi unahitaji nikusaidie?" Irene alimuuliza Mr Dango huku akiwa anapata kinywaji.
"Mbona una haraka sana?"

Walikuwa wamekaa kwenye nyumba ya Mr Dango iliyokuwa ni nyumba ya kifahari sana na ilikuwa inapatikana ufukweni mwa bahari. Ilikuwa nyumba nzuri iliyomchanganya sana Irene pindi alipokuwa anaingia kwa mara ya kwanza.

"Kwani kuna ubaya kuuliza kila mara?"
"Hapana sio vibaya!" Mr Dango alimjibu Irene huku akikaa kwenye kiti chake cha kivuvi.

"Unajua binti, katika hii dunia mambo hua yanaenda mbele na mwisho wa siku hurudi mwanzo, lakini kurudi kwake mwanzo sio kama mwanzo bali hurudi nyuma kwa kutumia watu wengine." Huku akikaa vizuri.
"Mmmh! Sijakuelewa!"
"Najua huwezi kunielewa, lakini utanielewa usijali."

"Watoto zetu baadae watakuja kuishi maisha yetu kwa marudio kama hatukuyamaliza yale tuliyokusudia kuyafanya." Huku akipiga fundo moja la wine.

"Vipi unatumia hii?"
"Hapana situmii, mimi bado mwanafunzi!"
"Ok! Nilisahau lakini sio mbaya."
"Hivi hapa unaishi peke yako?"
"Hapana ninaishi na mfanyakazi wangu wa kiume." Huku akitabasamu na kumuangalia Irene.
"Aaahhhaaaaa kumbe!"
"Sasa sikiliza nikwambie kitu Irene! Kuna kazi moja hivi nahitaji unisaidie." Huku akikaa vizuri.
"Kazi gani hiyo maana ndiyo ikiyonileta hapa."

"Kwanza nikusifu wewe ni binti jasiri sana, maana mwingine asingeweza kuja hapa na nazani ndicho kitu kilichonifanya nikuchague wewe."

Irene alibaki akimsikiliza kwa umakini Mr Dango bila kujua nia ya yule mzee.
"Nina kampuni yangu inazalisha bidhaa za kike, na ninahitaji modo ambaye atatumika kwenye matangazo ya biashara." Kisha akatulia kidogo.
"Mmh!" Irene aliishia kuguna.
"Nimetafuta na mwisho wa siku nimekuona wewe utanifaa."

"Mmh! Mimi huyu?" Irene aliuliza huku akijishangaa.
"Yeah wewe huyo huyo, mbona hujiamini?"
"Hapana naona kama bahati vile nisiyostahili."
"Usijishushe bwana!"

"Ok! But sorry nahitaji kwenda msalani." Irene alimuuliza Mr Dango.
"Aahhhhaa! usijali, nenda pale kwenye kile kijumba kuna choo pale." Mr Dango alimuelekeza Irene.

Wakati Irene akienda chooni huku nyuma Mr Dango alichukua pombe Kali na kumchanganyia Irene kwenye juisi yake kisha akatulia.

Irene alirejea kisha wakawa wanaendelea na mazungumzo yao huku nayeye akiifakamia ile juisi iliyokuwa ishachanganywa na pombe Kali.

Taratibu Irene alianza kujihisi vinaya huku akilewa kwa ajili ya ile pombe.
"Mmh! Mbona kichwa kama kizito?"
"Mmh! Labda itakuwa umechoka tu!"
"Hapana haijawahi kunitokea hii"
"Mmh! Sasa itakuwa ni nini? Au twende ndani ukapumzike kwa muda ukiwa fresh urudi nyumbani." Huku akinyanyuka na kwenda kumnyanyua Irene kusudi ampeleke ndani akapumzike.

Je! Nini kitakacho endelea? Usikose.



No comments: