HADITHI: RED BIKINI SEHEMU YA 18.





ILIPOISHIA👉🏽 Mr Dango alimlewesha Irene na kumpeleka ndani ili kusudi akapumzike. ENDELEA👇🏽

Mr Dango alipomuingiza ndani Irene alifanikiwa kumfanya alichodhamilia kwa yule binti. Alifanikiwa kumkata utepe binti wa watu aliyekuwa bado binti ambaye hakuwahi hata kutumika licha ya kuwa na mpenzi.

Mr Dango alifurahia kile kitendo moyoni kwasababu zake binafsi, na alipomaliza kufanya yake akatoka varandani na kujipumzisha huku akijisifu ya kwamba yeye kidume.

**********
Yalikatika masaa takribani matano ndipo Irene alipofanikiwa kuzinduka toka kwenye usingizi mzito uliosababishwa na zile pombe kali alizochanganyiwa na Mr Dango. Na ilikuwa ishatimu majira ya saa 1 jioni huku giza likiwa linajiandaa kuchukua zamu yake baada ya jua kumaliza zamu.

"Kwanini umenifamyia hivi!?" Irene aliuliza kwa sauti ya unyonge huku akimtizama Mr Dango na machozi yakimtoka.

"Listen binti mrembo!"
"Nimekuuliza kwanini umenifanyia hivi? Mimi si Sawa na binti yako lakini?"
"Nilishindwa kujizuia kutokana na uzuri wako."
"Ndio ukaina kunifanyia hivi utamaliza haja zako?"
"Hapana sikuwa na nia mbaya!"
"Hukuwa na nia mbaya!? Inamaana hiki ulichokifanya ni haki kweli?" Huku akiendelea kulia kwa uchungu.

Mr Dango ilimbidi kutumia nguvu ya ziada kumbembeleza Irene ili kusudi amuelewe. Ilipobidi alitumia pesa ili kumtuliza na alimpa pesa za kutosha ambazo Irene hakuwahi kuzishika zaidi ya kuzisikia tu midomoni mwa watu.

Irene alitulia lakini moyoni bado ilikuwa ikimuumiza kwa kutolewa bikra yake na mzee mwenye makamo tena mbaya zaidi alikuwa ni mzee kumzidi hata baba yake.

"Usijali mrembo, ni jambo la kawaida tu" huku akijaribu kumsaidia kunyanyuka kitandani.
"Hizo pesa zote ni za kwako binti, na usiwe na wasi wasi hata kidogo, utakapohitaji vingi utaniambia maana huu ni mwanzo tu." Huku akimpeleka bafuni akajisafishe.

**********
Naada ya miezi sita mapenzi ya Mr Dango na Irene yalizidi shamili ikafikia kipindi wiki haipiti bila ya kukutana kwa wawili hao. Muda mwingine Irene alifikia kudanganya nyumba kwao ili mradi apate wasaa wa kulala na yule mzee na yote hayo ilikuwa ni kwa ajili ya pesa. Irene alikuwa akipewa kiasi chochote akitakacho na ilifikia muda Mr Dango akawa kama mzazi wa Irene kwa maana aliweza kumpa kila kitu alichokuwa akikitaka. Masuala ya shule, mahitaji yake binafsi, mavazi na mambo mengine yote alifanyiwa na Mr Dango.

Basi maisha yaliendelea hivyo mpaka siku Mr Dango alipoamua kurekodi video na akiwa anafanya mapenzi na Irene bila ya mwenyewe irene kujua. Baada ya kufanya uchafu wake alioukusudia akahifadhi vizuri na kumtafuta mwalimu Frank ambaye ndiye aliyekuwa akitembea na mkewe kipindi kile cha nyuma hadi akafikia kumpa ujauzito.

**********
"Sikuwahi kuwaza kufanya hivyo mpenzi wangu."
"Najua hilo honey, na yote ni kwaajili ya upendo ulionao kwangu."
"Nashukuru kwa kulifahamu hilo honey."

Alikuwa si mwingine bali Mr Dango aliyekuwa akizungumza na mke wa mwalimu Frank ambaye alikuwa anamahusiano naye   kabla hata ya irene.

"Lakini mpenzi Leo nina jambo nataka nikwambie."
"Jambo gani tena mpenzi?"
"Dah! Hata sijui nianzie wapi kwa maana linanichanganya sana kichwa." Huku akikaa vizuri kitandani.
"Hebu niambie tafadhali labda naweza kulitatua." Huku akimsogeza mwilini mwake.

"Nina ujauzito wako!" Aliongea kwa unyonge.
"What!!?" Aliuluza kwa mshangano.
"Nina mimba yako! Inamaana hujasikia au ndio umeanza.?"
"Oohhhooo my God! Asante Mungu" huku akionekana kutabasamu.

Kile kitendo cha Mr Dango kilimshangaza sana mke wa Frank hadi akabaki ameduwaa asijue azungumze nini.

"Hivi unawazimu!?"
"Kwanini?" Mr Dango aliuliza.
"Kinachokufanya ushangilie ni nini?"
"Kwani mtu akipata ujauzito si jambo la heri hilo?"
"Eeehhee! Kama jambo la heri?"
"Inabidi tumshukuru Mungu kwa baraka zake." Alijibu kwa kujiamini.
"Kumbuka mimi ni mke wa mtu lakini?"
"Nalijua hilo, na sijui shida ni nini?"

"Mme wangu akijua kwamba hii mimba sio yake ni yako?"
"namimi ndivyo navyotaka hivyo!" Huku akinyanyuka kitandani.

**********
Ilifika siku ya siku Mr Dango aliamua kumpeleka mke wa Frank hadi nyumbani kwake. Frank akiwa yuko ndani amekaa varandani alisikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yake. Alijikaza kunyanyuka kwa maana alikuwa akiumwa ugonjwa wa kupooza, uliomsumbua kwa takribani miaka miwili. Frank alifanikiwa kuona gari aina ya range ikiwa imepaki na mkewe akishuka ndani ya gari huku akiwa anasindikizwa na mtu ambaye hakuweza kumfahamu vizuri.

Mlango wa varandani kwake ulisukumwa na mkewe aliingia huku nyuma yake akifatiwa na Mr Dango aliyeingia kwa dharau ya kuiangalia ile nyumba kila kona.

"We mwanamke! Hivi muda wote huo ulikuwa wapi!?" Aliuliza kwa ukali.
"Za saa hizi muheshimiwa!?" Dango alisalimia huku akikaa kwenye sofa na macho yakiwa kwa Frank.
"Huyu nae ni nani?" Aliuliza Kwani alishamsahau kwa vile Mr Dango alivyobadilika kutokana na pesa alizokuwa nazo, pesa zilimbadilisha hadi muonekano na ule muonekano wake wa zamani ukawa haupo tena. Hapo ndipo utayakubali maneno ya wahenga waliosema ya kwamba mla ndizi husahau ila mtupa maganda huaga anakumbukumbu nzuri tu.

Frank alikuwa ameshamsahau kabisa Mr Dango licha ya kuwa alimfanyia dhambi mbaya sana ya kutembea na mkews kipindi cha nyuma.

"Si nina kuuluza wewe, huyu ni nani!?" Huku akimtizama mkewe na kutaka kusimama lakini alishindwa kwa maana gongo lake lilikuwa liko mbali kidogo.

Haraka haraka Mr Dango aliliwahi lile gongo na kumkabidhi huku akimtizima kwa huruma kidogo ilichanganyikana na hasira sambamba na moyo wa kisasi. Lakini moyoni Dango alianza kujilaumu na kujuta alichomfanyia Frank baada ya kumuona yuko katika hali ile. Alimuangalia kwa muda kidogo na alioyakumbuka Yale mambo ambayo alishawahi kumfanyia nyuma pale pale moyo wa kikatili ulimrudia tena na kurudi alipokuwa amekaa mwanzo kisha akabaki kumtizama.

"Kaka yangu!" Huku akitupia mkoba wake mezani.
"Kaka yako!?"
"Ndio, mbona unauluza kwa mshangao?"
"Mbona simfahamu?"
"Inamaana wewe ndugu, ndugu zangu wote unawafahamu?"

Frank alishindwa kujibu cha zaidi akabaki anamtizama tu Mr Dango kwa kujaribu hata kumkumbuka lakini alishindwa.

"Sorry Frank!" Huku akisimama vizuri mbele ya Frank.
"Napenda kuanza kwa neno la samahani japo mwanzo wewe mwanzoni wakati unauwanza huu mchezo hukutaka kuanza kwa ustaarabu." Huku akimuangalia kwa umakini.

"Tafadhali niambie wewe ni nani?"
"Usijali nitakwambia!" Huku akirudi nyuma na kusimama mlangoni.
"Kwa Leo sitokwambia chochote lakini ipo siku inakuja utayajua yote, nazani itapendeza tukiwa wawili tu." Kisha Mr Dango akaaga na kuondoka zake akiwaacha mtu na mkewe watayamaliza wenyewe.

**********
"Kiukweli iliniuma sana japo hukuhitaji kujua maumivu yangu na ndio kwanza yalikuwa kama wimbo mzuri ama filamu nzuri iliyokuwa ikikuburudisha bila kujali nyota wa ile filamu anateseka ili wewe akupe burudani." Dango alizungumza huku akiwa amekaa na Frank kwenye grosali moja iliyokuwa ikipatikana katika ule mtaa wa Frank.

"Niliumizwa sana hadi ikafikia kipindi nikaamua kuikimbia familia yangu ambayo wewe uliifanya kama yako" huku akiburuza mkono wake wa kulia mezani ukiwa umeshika CD na kumkabidhi Frank.

"Naomba ukaiangalie hii filamu nazani utajua nini ninachomaanisha napokwambia kipindi kile niliumia." Huku akiondoka zake na kumuacha Frank hajielewi na ile CD akiwa ameishika.

"Kweli nimeamini dunia inatembea na usimdharau mtu kwa muonekano wake wa sasa bila kujua baadae atakauwa nani." Frank alijisemea huku akimuangalia Mr Dango aliyekuwa anaingia ndani ya gari. Frank alijizoa zoa na gongo lake kusha akaanza safari ya kurehea nyumbani kwake japo ilikuwa kwa shida.

ITAENDELA



No comments: