HADITHI: RED BIKINI SEHEMU YA 19.
ILIPOISHIA👉🏽 Mr Dango alimkabidhi CD Frank ili akaangalie filamu aliyompelekea kama zawadi ili kusudi ajue maumivu yake aliyokuwa akiyahisi zamani. ENDELEA👇🏽
Frank hakuamini hata kidogo alipoiangalia ile CD, alijikuta akipigwa na butwaa chumbani huku akiwa ameishika laptop yake.
"Dah! Irene binti yangu!" Huku machozi yakimtoka na kuanza kutetemeka kwa hasira kwa kutokana na kile alichokuwa akikiona kwenye ile CD. Mbaya zaidi Mr Dango alirekodi kila kitu kuanzia mwanzo alipomtoa bikra Irene na siku zote alizokuwa akienda kwake.
Frank ilimuuma vibaya kiasi kwamba alibaki hana la kufanya cha zaidi ni kulia huku akiwa anaangalia ule uchafu wa Mr Dango.
"Kweli what goes around comes around." Huku akijishika kichwa na kujikuta akikurupuka toka kitandani na kujiona kama maajabu kwa maana alisimama bila hata ya kutumia gongo lake.
"What!?" Huku akijishangaa na kabla hajaamua kufanya chochote mara mlango ulisukumwa na mkewe akaingia huku akiwa amejawa hasira kichwani.
Kwanza mkewe nayeye ilimbidi ashangae baada ya kumuona mmewe akiwa amesimama bila kutumia gongo. Waliangaliana kwa muda huku kila mmoja akiwa ana lake kichwani, Frank akiwa kwanza anahasira za binti yake huku akiwa haamini kama kweli alikuwa amepona ugonjwa wake na mkewe nayeye alikuwa haamini kama mmewe ndiyo amepona au alikuwa akimuigizia huku pia akiwa ana hasira za kuambiwa ya kwamba mmewe alikuwa ana mtoto nje ya ndoa.
"Mmh! Naona sasa umepona?" Huku akisimama mbele yake.
"Hata siamini ujue!"
"Na huwezi kuamini kwa maana nimekuja na habari mbaya zaidi!" Huku akibadili uso wake ghafla.
"Unaongea nini wewe?"
"Usijali utanielewa tu." Huku akisimama vizuri.
"Edwin ndio nani?" Huku akishika kiuno.
Lile swali lilianza kumchanganya Frank na kujikuta akisimama huku akiwa ameyatoa macho yake asiamini kama mkewe angekuja kumuuliza lile swali.
Alifanya kwa siri sana kuficha ule ukweli licha ya kuwa alishavunja mahusiano na Mrs Dango na kumkataa mpaka mtoto kwa kisa cha kulinda ndoa yake.
"Usitumbulie macho yako hapa kama sijui fundi saa aliyepiteza mshale wa sekunde, nimekuuliza Edwin ni nani!?" Kwa sauti ya juu na ya ukali.
"Sikuelewi ujue"
"OK! Sawa, inamaana unamtoto nje ya ndoa si ndio?" Huku akimuangalia kwa jicho la umakini mmewe.
Frank hakuwa na la kujibu zaidi ya kukaa kitandani kwa uchovu.
"Sasa nisikilize kwa umakini" huku akifungua kabati la nguo huku mmewe akimtizama bila kujua anachotaka kukifanya.
"Mimi nimeshindwa kukuvumilia sawa baba?"
"Sasa unataka kufanya nini?"
"Wewe si kidume? Ngoja niondoke nikuachie nyumba yako ili uendelee na umalaya wako."
"Hapana usifanye hivyo mke wangu."
"Nimesema usinishike" huku akimsukuma na kwenda kuangukia kitandani.
Mkewe alichukua kila kitu kichamuhusu kisha akaanza safari ya kutoka chumbani huku Frank akimbembeleza bila mafanikio. Unaambiwa mwanaume hadi akamwaga chozi, ndio ile John Saimon a.k.a Joh Makini aliimba kwenye wimbo wake ujulikanao kama bye bye *_"muuwaji anapofiwa hulia machozi halisi na sio bandia"_*.
Frank licha ya kuwa alifanya uchafu ule na kutenda usaliti lakini kwenye suala la kuomba msamaha, aliomba msamaha wa dhati toka moyoni.
Mkewe alitoka hadi nje huku mmewe akiwa anahangaika kumzuia bila mafanikio.
"Sorry ndugu" Mr Dango alizungumza huku akimpokea begi mke wa Frank.
"Ngoja nimpokee begi ili msije mkaumizana" kisha akaenda kuliweka kwenye gari.
"Brother!" Aliita huku akimfata Mr Dango lakini alijikuta akisukumwa hadi chini.
"Usijaribu kunigusa kwa maana huu mchezo uliuanzisha mwenyewe na wakati wewe unaucheza kipindi kile Mimi niliamua kuplay fiar, sasa huu ni wakati wako wa kucheza kiungwana." Huku akisimama mbelw yake.
"Hahahahaha!!.... Naona umepona sasa? Vipi ile filamu uliiangalia?" Huku akitabasamu kwa dharau.
"Mshenzi wewe!" Frank alikurubuka toka ardhini lakini alijikuta akipoa baada ya kukutana na mdomo wa bastora.
"Fanya tu kama unajikuna halafu nikuoneshe kitakachofata." Huku akiwa ana sura ya jazba.
"Honey! Ingia ndani ya gari." Mr Dango alimuamuru mke wa Frank huku akiwa bado amemahikia bastora Frank.
Mke wa Frank kabla hajaingia ndani ya gari alirudi hadi aliposimama mmewe na kuanza kushika shika tumbo lake.
"Malipo ni hapa hapa duniani, namimi nina ujauzito wa mpenzi wangu!" Huku akitabasamu na kwenda kumbusu Mr Dango kisha akaishia ndani ya gari.
Frank ile habari ilimuumiza mara mbili zaidi ya kile alichokiona kwenye ile CD na kubaki akilia kama mtoto mdogo mbele ya nyumba yake.
"Vipi umefanikisha?" Mr Dango alimuuliza Diana ambaye ndiye mke wa Frank.
"Yeah!" Huku akitoa CD kwenye mkoba wake na kumkabidhi mkononi.
"Kazi nzuri!" Huku akiwasha gari na kuiweka ile CD kwenye droo.
Gari iliondoka kwa fujo na kumuacha Frank haamini kama kweli mkewe amebebwa kirahisi rahisi na Mr Dango. Mwenzake mwanzoni alikimbia nyumba ila yeye safari hii kaachiwa nyumba na mkewe. Frank alijikuta akikumbuka kitu na kurudi ndani kwa kasi huku akijisemea.
"Lazima nikufunge mbwa wewe! Mwanangu bado mwanafunzi halafu unaenda kufanya naye uchafu?" Akiwahi kwenda chumbani.
Baada ya kufika chumbani frank hata hakuamini baada ya kukuta CD haipo mahali alipoiweka na akabaki amechanganyikiwa kwa maana alijua fika ule ndio ushaidi tosha wa kumtia hatiani Mr Dango ya kwamba alitembea na mwanafunzi. Lakini ndoto zake zikayayuka baada ya kuikosa ile CD na alijua fika mkewe ndiye aliyeondoka nayo.
"Diana!!!!!?" Aliita kwa sauti kubwa huku akijitupia kitandani na machozi yakimbubujika.
**********
Hali ya huzuni ilitanda kwa irene baada ya baba yake kujiuwa kwa kunywa sumu na mbaya zaidi alijiuwa bila ya kuacha Ujumbe wowote. Irene sambamba na mama yake wakiungana na ndugu wengine walijumuika kwenye mazishi hadi msiba ulipoisha.
"Mama?" Irene alimuita mama yake.
"Vipi binti yangu?"
"Hivi unaweza ukajua baba alijiuwa kwa sababu gani?"
"Mmh! Hata aielewi mwanangu"
"Au sababu ni kuuguwa kwa muda mrefu?" Irene aliuliza huku wakiangaliana na mama yake.
Diana alijua fika alichozungumza mwanae hata sio kweli kwa maana siku ile kabla ya kujiuwa Frank alipona ugonjwa wake.
"Mmh! Halafu weww ndiyo ufakuwa umeongea kitu cha kweli!"
"Sasa unazani kuna nini zaidi ya hilo? Au mligombana?"
"Hapana!"
"Basi itakuwa ni kuuguwa kwa muda mrefu bila kupata tumaini la kupona."
"Lakini wakati anakunywa sumu wewe ulikuwa wapi?"
Swali lilikuwa gumu kidogo kwa mama yake na kujikuta akiangaliana na binti yake.
"Nilitoka mara moja kwenda mjini na nilimuacha akiwa mzima na tuliagana vizuri tu" huku akiwa kama hajiamini.
"Mmh! Kwa maana niliporudi toka shule na kuingia ndani nilikuta nyumba haieleweki na chumbani kulikuwa hakutamaniki yani vurugu mtindo mmoja utazani kulikuwa kuna ugomvi" huku akiwa anaongea kwa huzuni kubwa.
"Haoana mwanangu usiwaze hayo!" Huku akimkumbatia mwanae.
Diana alimficha mwanae ukwwli ili asije kujua Lisa cha baba yake kujiuwa, na hata suala la msiba irene ndiye aliyempigia mama yake kwamba mmewe kanywa sumu na kipindi hiko anaoiguwa simu ndio kwanza alikuwa akiingia nyumbani kwa Mr Dango.
Ikabidi arudi ili kusudi kuuficha ukweli kwa mtoto wake, na Diana mwenyewe akawa hajui kama ile CD aliyoambiwa akaiibe kwa mmewe ilikuwa ni ya uchafu wa Mr Dango na Irene.
Basi maisha yaliendelea na mwisho wa siku msiba ulisahaulika na Diana na Irene waliendelea kuishi pale pale lakini Mr Dango akawa anaihudumia ile familia na kuwatumia mtu na mama yake bila ya wao kujijua.
Baada ya miezi Tisa kufika Diana alifariki akiwa anajifungua na kwa BAHATI mbaya zaidi hadi mtoto naye alipoteza maisha na kumfanya Irene abaki peke yake mkiwa.
ITAENDELEA
No comments: