HADITHI: RED BIKINI SEHEMU YA 20.






ILIPOISHIA👉🏽 Diana alifariki dunia wakati wa kujifungua na Irene akawa amepoteza wazazi wake wote wawili. ENDELEA👇🏽

"Inamaana unataka kusema wewe sio baba yangu mzazi?" Edwin aliuliza kwa mshangao huku akiwa haamini baada ya kusimuliwa ile habari ya kwanini Mr Dango aliamua kuiterekeza familia yake.
"Nazani naweza nikasema hivyo, kama nitakuwa sijakosea."
"Kwanini sasa hukuniambia tangu awali?"
"Nilishindwa kukwambia ili kuficha dhambi za mama yako" huku akisimama na kwenda aliposimama Edwin.

"Irene ni dada yako kwasababu baba yenu ni mmoja, na niliamua kukulea kwasababu nilijua fika wazazi wako wote wawili walishafariki." Huku akimshika bega Edwin.
"Dah! Aibu gani sasa hii mzee?" Huku akilia na kumkumbatia Mr Dango.

"Wewe hata kama hukunizaa lakini ulisimama kama baba yangu na hakustahili kuyafanya haya." Huku akiendelea kulia mwilini mwa Mr Dango ama baba yake mlezi.

"Najua nimefanya kosa lakini nilifanya vile kwa ajaili ya kisasi na sikutarajia kama haya yote yatatokea."
"Naiweka wapi sura yangu sasa kwa mfano?"

Edwin akiwa bado anaendelea kuzungumza na Mr Dango ambaye ni baba yake mlezi mara ghafla akaingia irene na hakutarajia kama angemkuta Edwin mahala pale licha ya kujua kwamba Edwin na Mr Dango ni mtu na baba yake.

Alisimama mlangoni huku akiwa anawashangaa baada ya kuwaona wanalia wote wawili.
"Kulikoni!?" Aliuliza huku akiwa bado amesimama mlamgoni.
"Karibu!" Mr Dango alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akijaribu kufuta machozi yake.

"Mueleze tu ukweli!" Edwin aliongea.
"Ukweli gani? Ya kwamba huyu ni baa yako mzazi?" Huku akifunga mlango na kusogea waliposimama wenzake.

"Bora hata ingekuwa hivyo kuliko hili nililolijua sasa!" Huku Edwin akikaa kwenye sofa.
"Kwani kuna kitu kinaendelea mahali hapa?"

"Sijui hata nianzie wapi kukueleza?" Mr Dango alibaki akijiuliza wapi pakuanzia.
"Ujue mnanichanganya? Hata siwaelewi" huku akikaa chini kwenye sofa.

"In short ni kwamba wewe ni dada yangu!" Huku akikaa chini nayeye.
"Unasemaje wewe!?" Irene alisimama kwa mshangao.
"Huo ndio ukweli irene, na naweza sema Mimi ndiye mwenye makosa" huku akilia kwa huzuni.

"Hata siwaelewi mnachozungumza."Waliendelea kuzozana huku Edwin na Mr Dango wakiendelea kumuelekeza Irene juu ya kile walichomwambia.

Ilikuwa sio kazi rahisi kumuelewesha Irene ambaye alikuwa hataki kuamini kwa kuamini yeye ni mtoto wa Mr Dango.

" inamaana wewe ni baba yangu Mimi?"
"Hapana"
"Sasa nitakuaje na undugu na Edwin?"
"Mimi sio mtoto wa Dango baba yangu anaitwa Frank ambaye alizaa na mke wa Dango na ndiye mama yangu Mimi." Edwin alijaribu kutoa maelekezo kwa maana alisha hadithiwa mchezo kamili na Mr Dango.

"Huyu ni baba yangu MLEZI tu!"
"Inamaana ulichukua jukumu la kumlea Edwin na Mimi huku ukiujua ukweli wote?" Irene aliuliza.
"Sikutaka mjue ukweli na uchafu uliofanywa na sisi wazazi wenu."

"Sasa ndio umefanya nini?" Irene aliuliza kwa sauti ya kukalikia.
"Sikuwa na jinsi na hata kifo cha baba yako kikitokana na kuujua ukweli ya kwamba Mimi nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wewe, isitoshe nikaamua kutembea na mama yako na hata ule ujauzito uliomuuwa mama yako ulikuwa ni wa kwangu!"
"Kelele acha ujinga wako! Mzee mchafu sijapata kuona." Irene alifoka huku akimrushia bakuli la mauwa lililokuwa mezani na kumpata Mr Dango kichwani.

"Huoni aibu kuyataja maovu yako? Ona sasa mpaka tukaja kufanya uchafu na ndugu yangu?" Irene hakutaka kuelewa hata kidogo.

"Nakuchukia sana!" Huku akimsogelea na kumpiga na miguu yake.
"Irene relax basi!" Huku akimshika na kumtuliza Irene.

"Edwin niache nimkomeshe huyu mbwa!" Huku akimsukuma Edwin pembeni.
"Haina haja kufanya hivyo, kumbuka bila yeye tusingefika hapa?"
"Kuna maana gani sasa ya kuyafanya yake yote? Msaada wake inamaana gani kama ndio katuvuruga kiasi hiki?"

Varangati lilikuwa kubwa hatari lililodumu masaa karibu matatu gani hadi watu wote wakawa wamekaa wakiangaliana kama madume ya kuku yaliyopigana yakachoka. Kila mmoja akiwa na hasira na mwenzake lakini sana sana Irene alionekana kuwa na hasira zaidi kuliko mwenzake.

**********
Miezi sita ilikatika na taratibu maisha yalianza kuwa Sawa baada ya lile tukio la kujuana kati ya Edwin na Irene kama ni ndugu. Na walikuwa washamaliza chuo kwa hiyo walijikuta wakiishi pamoja kwa Mr Dango lakini maelewano kati ya Irene na Mr Dango hayakuwa mazuri hata kidogo.

"Nimewaita hapa nina jambo nataka kuwaeleza." Mr Dango alizungumza huku akiwa amekaa kwenye sofa mbele ya Edwin na Irene.

"Najua nimewakosea sana lakini hamuna budi kunisamehe maana mkishindwa kufanya hivyo mtabakia na kisasi ambacho baadae kitakuja kuzaa tatizo lingine kama lilivyokuja kuzaliwa tatizo hili." Huku akiwa kama mtu mwenye majuto usoni.

"Nawaomba mnisamehe sana, na mjue ya kuwa halikuwa tarajio language kama yatakuja kutokea haya yote, ila nachowaomba ni kitu kimoja tu..." Alisita kidogo kisha akaendelea.

"Nitawaachia mali na nusu ya utajiri wangu sambamba na zile nyumba za wazazi wenu, irene utachukua ile nyumba ya marehemu baba yako na wewe Edwin utachukua ile nyumba ya marehemu mama.yako japo niliijenga Mimi lakini nilimuachiaga kipindi nilitoroka nyumbani."
"Unafikili hizo Mali zote zitafuta maovu yako?" Irene aliuliza lakini Edwin alimzuia kwa kumshika mkono.

"Maovu yangu yatafutika endapo nyie mtaamua kunisamehe maana sina mabaya tu pekee bali nina mazuri pia nimeyafanya katika maisha yenu." Huku akinyanyuka na kwenda chumbani kwake.

"Na wewe mbona unaonekana kumtetea sana?" Irene alimuuliza Edwin.
"Sio kumtetea, ila kumbuka amekuhudumia tangu wazazi wako walipofariki?"
"Ilikuwa ni wajibu wake kwa maana yeye ndiye chanzo cha vifo vyao."

Wakiwa bado wanajadikiana lile suala ndipo Mr Dango akatoka na begi lake hadi varandani.
"Kulikoni tena?" Edwin aliuliza kwa mshangao.

"Nimeamua kuondoka kwenda mbali nanyi kwa maana niliyoyafanya kwenu hayastahili hata kukaa na kuwaangalia usoni."
"Hapana usifanye hivyo mzee!" Edwin akijaribu kumzuia.
"Lakini si tushakusamehe?" Kidogo Irene huruma ilianza kumuingia.

"Sistahiki kuendelea kuishi nanyi." Huku akiondoka na kuawaacha Edwin na Irene wakibaki hawaamini kama ukweli mtu waliyemzoea anawaacha.

Mr Dango alipofika mezani akaweka karatasi na kuondoka zake huku irene akienda kuichukua ile karatasi na alipoiangalia kwa umakini ilikuwa ni cheki ya benki. Ikikuwa imeandikwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho ni nusu ya pesa alizokuwa anamaliki Mr Dango.

"Nini!?" Edwin aliuliza huku akimsogelea Irene.
"Mbona pesa nyingi sana?" Irene aliuliza kwa mshangao.
"Mmh! Inaelekea alikuwa ana pesa nyingi sana, Mpaka kutuachia kiasi hiki cha pesa?"

**********
Baada ya wiki moja kupita tangu Mr Dango aondoje nyumbani irene na Edwin maisha yao yaliendelea kama mtu na kaka yake. Ilikuwa ngumu kwa wao kuweza kuzishinda hisia zao za kimapenzi kwa maana walishawahi kuwa na mahusiano tena wakifanya na michezo yote yanayowahusisha wapenzi.

"Nahutaji kuhama hapa!" Irene alianzisha hoja huku wakiwa wanakula chakula cha jioni.
"Kwanini utake kufanya hivyo?"
"Nimeamua tu, Kwani tutaendelea kuishi hapa pamoja mpaka lini!?"

"Utaenda kuishi wapi sasa?"
"Naenda kuishi kwenye nyumba walikokuwa wakiishi wazazi wangu!" Huku akiwa anamalizia kula chakula chake.

"Sizani kama huo ni uwamuzi sahihi kufanya wakati huu." Huku akinyanyuka na kwenda kumzuia irene asiondoke.

Walijikuta wakiangaliana kwa muda hadi hisia Kali za mapenzi zikiwajaa na kushindwa kujizuia na taratibu wakajikuta wananyonyana ndimi. Na kwakua walikuwa wanahamu muda kwa kila mmoja akiwa anamtamani mwenzie. Unaambiwa ukilamba asali basi lazima utachonga mzinga kabisa, vijana walisahau ya kwamba  in ndugu na kujikuta wakivunja amri ya sita tena pale pale varandani.

Ilikuwa mechi ya kukata na shoka kwa maana pindi wakutanapo hawa watu huaga ni zaidi ya matusi maana ni rusha nikurushe.

"Assssiiiiiiiii....Edwin ila tulisemaje?" Irene alibaki akijiulizisha huku akiwa ameng'ang'ania Edwin kiunoni mwake kusudi aendeleze dozi. Risasi zilipigwa na wakajikuta wamepitiwa na usingizi pale pale varandani huku wakiwa hawajitambui kabisa wako hoi kwa ule mtanange.

**********
Asubuhi ya siku iliyofata Edwin alikurupuka toka usingizi huku akiwa yuko peke yake. Hakujali kabisa kwa maana alijua fika irene atakuwepo ndani chumbani.

"Irene!?" Aliita lakini hakujibiwa hata kidogo.
Edwin alizunguuka kila kona ya nyumba lakini hakufanikiwa kumuona irene.

"Sasa atakuwa amekwenda wapi!?" Alijiuliza huku akirudi varandani na kibukta chake.

Akiwa anatafakari ndipo alipoiona karatasi ikiwa na maandishi mezani. Edwin aliikamta kisha akaanza kuisoma.

"Samahani sana Edwin, najua nitakuumiza sana lakini sikuwa na jinsi hata kidogo. Ni heri niondoke nikaishi mbali nawewe kuliko kuendelea kukaa pamoja kwa maana tusingeweza kuvumilia kukaa pamoja bila kufanya mapenzi. Nimeamua kwenda mbali nawewe na kwa taarifa tu wiki ijayo nitaolewa na Sudi. Nisamehe sana ni mimi wako Irene."

Edwin aliitupa ile karatasi na kujitupia kwenye kiti huku akiwa haamini kama kweli Irene ameondoka.
"Kwanini usingesema sasa na kuamua kuondoka bila kuniaga?" Alijisemea peke yake huku mlango ukifunguliwa.

Alipotupia jicho mlangoni alikutanisha macho na Lecho aliyeingia huku akiwa anamuangalia Edwin kwa tabasamu.
"Nani aliyekuelekeza hapa?" Edwin aliuliza.

Lecho hakujibu cha zaidi alimpatia cheki Edwin iliyoandikwa na Irene.
"Ameniagiza nikupatie hii na suala lingine lililonileta hapa ni kuhusu Mimi na wewe!" Huku akikaa kwenye sofa na kufanya Edwin abaki ameduwaa.

Edwin aliisoma ile cheki kisha akaitupia mezani na kumgeukia Lecho alipokuwa amekaa. Wakati Edwin anamgeukia nayeye akawa anavua nguo zake kisha akabaki na chupi yake nyekundu aina ya bikini na kuanza kumsogelea Edwin aliyebaki ameshangaa.

Edwin kama kawaida ya ugonjwa wake alijikuta akipagawa na shetani wa ngono akimpanda na kumvamia lecho kisha akambebelea kwenda naye chumbani.

Huko ndani alikuwa ni balaa tu kwa maana Lecho alikuwa anatoa miguno ya mahaba huku Edwin akiendelea kushusha dozi ya maana.

Baada ya saa nzima Edwin alitoka chumbani na kujisemea.
" *_RED BIKIN_*" Huku akitabasamu na kwenda kuchukua jagi la maji ya kunywa kwenye fiza.

"Napenda sana kuangalia mapenzi ya jinsia moja haswa haswa wanawake na sijui kama hii tabia nitakuja kuiacha." Huku akimgeukia Lecho aliyetoka na kipande cha mtandio alichojitanda mwilini mwake.

"Itakuwa unamatatizo ya kisaikolojia sio bure!" Huku akichukua glasi ya maji na kukaa kwenye sofa na macho yakiwa kwa Edwin aliyekuwa amesimama mbele yake.

" *_RED BIKIN_*! ndiyo iliyokuwa ikipagawisha sana, na naweza sema katika wanawake waliokuwa wakinijulia ugonjwa wangu basi wewe ndiye haswa."

Miaka ilikatika na Edwin sambamba na Lecho walioana huku irene na Sudi pia walifunga ndoa na kuunda familia zao.

Maisha yalienda na mwishoe Irene na Edwin iliwabidi wakubaliane na ukweli ya kwamba walikuwa ndugu.

       *_MWISHO_*
Hepuka ngono zisizo za razima kwa afya ya ndoto zako. Nchi yako inakutegemea na jamii yako kwa ujumla, ngono zembe hupunguza uwezo wa kijana kuzalisha na kufanya na shughuli za kimaendeleo. Nini maoni yako? Na umejifunza nini kutoka kwenye hii hadithi ya *_RED BIKINI?_*



No comments: