MPENZI CHEUPE 02




Wakiwa njiani kuelekea Ilala dereva tax alikuwa na neno la kusema "mwanangu lakini mbona kama huyu mwanamke haeleweki?" "sijakuelewa mzee wangu unamaanisha?" "samahani kijana wangu kwani mmefahamiana lini na huyo binti?" "mh ! sasa wewe itakusaidia nini ukijua kufahamiana kwetu" "najua hutanielewa kirahisi lakini kama una kifua nikwambie nilivyomwelewa mimi" "sasa mzee wangu bila kifua mimi naishije? ina maana wewe unaniona na tumbo tu" "haaaa haaaa la! hasha naomba nisamehe kijana wangu nisije kuharibu uhusiano wenu" "huwezi haribu mimi nampenda na yeye ananipenda sana najua ninyi madereva tax mna siri nyingi sana za wanawake"

"ni kweli tuna siri nyingi sana lakini kazi yetu ukitaka kuendelea nayo vizuri lazima ukae kimya" "sawa mzee wangu mimi nimefika naomba niache nikutafute kesho saa hizi nimechoka sana wacha nikapumzike" 'ah sawa mimi huwa napaki pale mtaa wa Aggrey karibu na Clock Tower" "ahsante haya hela hii hapa" alirudishiwa chenji tax iliondoka.Brown aliingia ndani kulala,akiwa usingizini aliota yupo kwenye sehemu nyingine nzuri sana,mauwa mazuri yamepamba kwenye bustani,ghafla panabadilika na kuwa msitu mkubwa ulioshonana sana,wanyama wakali wanamfukuza,Brown anakimbia kwa nguvu zote lakini wanyama wale walikaribia kumshika,walikuwa wanatisha sana,walipojaribu kumrukia Brown alihisi atakufa alipambana na kuona anazidiwa,alikurupuka toka usingizini.

Ilikuwa ni saa nne za asubuhi,aliketi kitandani huku jasho likimtoka,kichwa kilikuwa kinamuuma sana mpaka alihisi mishipa ndani ya kichwa itapasuka,aliwaza na kuwazua asipate jibu la ndoto yake,baada ya kichwa kutulia,alikwenda kuoga,alijiandaa na kwenda kutafuta supu kwenye baa moja ya karibu,alitamani muda ufike wa kwenda kumuona mpenzi wake Salma,hivi kwa nini sikuchukuwa namba zake za simu?,na nilizubaa vipi sikupiga nae picha? ningekuwa namwangalia saa hizi kama sio kuongea nae,alijilaumu sana alihisi kukmkosa mtu muhumu kwenye maisha yake.

Jua lilianza kupoa,muda wa jioni uliwadia,Brown alijiandaa vema,alivaa akapendeza kama kawaida yake utanashati alizaliwa nao,alijipulizia manukato ya bei mbaya,yote ni kutaka kutoea maridadi mbele ya mpenzi wake,alijiangalia kwenye kioo mara mbili mbili alijikagua mpaka meno,alijiona yupo sawa,alitoka kuelekea panapo egesha tax,alikodi tax moja "nipeleke mtaa wa mission Kota" aliekeza Brown "sawa kaka itakuwa shillingi elfu tano tu" "mmh we bwana we yaani hapo tu hela yote hiyo?" "kama hapo mbona hukutembea hapo naenda kwa elfu tano" "dah ! haya bwana nipeleke" alikubali Brown kwasababu alikuwa na mchecheto wa kumuona Salma,alikuwa akiwaza atakavyo mkumbatia,anavyonukia,alivyo msafi aliona anachelewa kufika.

Brown alifika mtaa wa Mission Kota,gari liliegesha mbele ya nyumba ya kina Salma,alilipa tax alishuka taratibu,tax iliondoka kwa kuwa hakuwa mgeni wa kuondoka kwa haraka,aliahidiwa kupikiwa,aliwaza ale chakula alichopika Salma,alikaribishwa na wadada kama watano waliokuwa wameketi barazani "karibu...karibu" huku wakimshangaa mwanaume mtanashati Brown "ahsante...ahsante sana" "karibu tukusaidie nini?" "ahsante namuulizia Salama Cheupe" wale wadada kwa mshangao walitazamana wote watano kwa haraka "mh ! kwani wewe unamfamu vipi? au ni nani yako?" "mimi nilikuwa naye club jana" "kheee! jana?!!" wale wadada walishangaa kwa pamoja jambo lililomshtua sana Brown.

"hebu subiri kwanza unasema jana uliekuwa naye?" aliuliza mmoja wa wale madada "ndiyo jana nilikuwa naye....vipi kwani amehama?" "mh ! mazito hebu karibu ukae utueleze vizuri" "kuna nini jamani mbo mnanitisha?" aliuliza Brown huku akiwa ametanguliza mkono kukketi kwenye kiti "hapa hatukutishi ila tunapenda kujuwa mlivyokutana mpaka akakuelekeza hapa" "sio kunielekeza tu nimekuja naye jana usiku mpaka chumbani kwake" "eh ! wewe ! unasema" mmoja wa wale wadada alishangaa na kutega sikio vizuri............... ITAENDELEA



No comments: