MPENZI CHEUPE # 01



Saa nne za usiku kituo cha mabasi Kongo jijini Dar es salaam,upepo mkali ukivuma,wingu jeusi likiwa limtanda angani,kibaridi cha wastani kinapuliza,Brown akiwa amesimama kusubiri usafiri mara linasimama basi anashuka msichana  mrembo,mweupe sana,mrefu,mwenye kunukia vizuri,anamvutia Brown,kabla hajafanya chochote mvua kubwa ya ghafla inashuka na kuwalazimisha abiria walikuwa kutoni kukimbilia chini ya baraza la ghorofa lililopo nyuma ya kituo.

Brown alijikuta yupo karibu na mrembo yule aliyeshuka kwenye Basi muda mfupi uliopita "hii mvua inataka kuharibu starehe za watu" Brown alijisemesha,mrembo alionekana kutoelewa alichozungumza Brown,alitabasamu na kumsogelea "unasema?" aliuliza mrembo "hii mvua inataka kuharibu starehe za watu" " ni kweli kabisa nilikuwa nawaza nikilowa naingiaje Billcanas" "oh na mimi naelekea huko....unaonaje tuchukuwe tax?" "sawa itakuwa vizuri maana hii hali ya hewa na muda huu usafiri mgumu itakuwa tabu".Brown aliita tax iliyokuwa inapita walipanda na kuelekea Club Billcanas.

Walifika Billcanas,Brown alilipa kiingilio wakaingia,wakiwa ndani "samahani unaitwa nani?" aliuliza mrembo "naitwa Brown" alijibu huku akinywa funda moja la kinywaji chake "okay vizuri nafurahi kukufahamu" "na wewe unaitwa nani?" "Salma... lakini maarufu Cheupe au ukipenda yote mawili Salma Cheupe ni sawa pia" "anhaa nimefurahi pia kukufahamu" waliendelea kucheza na kufurahi,hakika walipendezana sana,watu wengi ndani ya club walikuwa wakiwaangalia sana kwasababu Brown na yeye alikuwa mtanashati sana.

Hisia za mapenzi ziliibuka na kupiga kambi kwenye mioyo yao wote wawili,muda wote Salma alikuwa akitabasamu,Brown alimuona Salma anafaa kuwa mpenzi wake "unaishi wapi?" "mmh! naishi Kariakoo mtaa wa Mission Kota.... na wewe?" naishi ilala Shariff Shamba karibu na hospitali ya Amana" "sawa" "samahani umeolewa?" " mh! ningeolewa ningekuwa huku saa hizi? hapana sijaolewa hata mchumba sina" " haiwezekani huna mchumba uzuri wote huu?" aliongea Brown kwa mshangao mkubwa sana "kweli sijaolewa nipo alone ndio maana huwa nakuja huku kujifariji" "mh haya...mimi naomba tuwe tunakuja wote" "sawa hapana tabu nitashukuru" walikubaliana na kuendlea kuponda starehe.

Muda wa saa kumi alfajiri walitoka club ,Brown alichukuwa tax ili kurudi nyumbani,walikaa siti ya nyuma,baada ya tax kuanza kuondoka Salma alilalamika anahisi baridikutokana na upepo wa alfajiri,Brown alivua koti lake na kumvisha Salma "ahsante mpenzi wangu" alishukuru Salma maneno yaliyoshtua moyo wa Brown "usijali nakupenda sana nipo tayari kukulinda na chochote" "ahsante nami nakupenda pia" Brown alimchumu Salma shavuni "mmh ahsante na wewe mwaaah" Salma alirudisha lile busu,Bown alimkumbatia Salma na Salma aliegemeza kichwa chake kifuani mwa Brown.

Walifika mtaa wa Mission Kota kariakoo,Brown alishuka ili aagane na Salma "sasa mpenzi ?" aliuliza Brown "yaani unataka uishie nje? hapana bwana tafadhali ingia hata uone chuba changu" aliongea Salma huku akimvuta Brown mkono "hapana nitakuja kesho saa hizi muda umeenda sana" "unadhani nani atakuona hakuna aliye macho wote wamelala fofofo" mwanamke ana nguvu sana Brown alishindwa kuendelea kukataa,alijikuta akiingia ndani ya nyumba ya kina Salma "karibu sana hiki ni chumba changu jisikie huru wakati wowote karibu sana" "ahsante nitakaribia Mungu akipenda" Salma alifungua kabati lake na kutoa mkufu wa dhahabu,alimkabidhi Brown.

"hii cheni nakupa kama ishara ya upendo wangu kwako" aliongea Salma "ahsante sana nashukuru" Brown aliinuka na kumkumbatia Salma "utakuja lini tena ili nikupikie tule wote na ndugu zangu wakujue" "kesho jioni nitakuja" "sawa karibu sana" walitoka chumbani Salma alimsindikiza Brown mpaka kwenye tax "haya usisahau koti lako" aliongea Salma huku akilivua "hapana hapana na mimi hilo ni ishara ya upendo wangu kwako" "eh asante jamani" waliagana Brown aliondoka.

Wakiwa njiani kuelekea Ilala dereva tax alikuwa na neno la kusema "mwanangu lakini mbona kama.............................ITAENDELEA



No comments: