MPENZI CHEUPE 10



"eh ! Mungu wangu kumbe kweli" aliongea mkuu wa kituo huku akipapasa kitasa cha mlango "nini nini baba Jay nini kwani?" aliuliza mama Jay ambaye ni mke wa mkuu wa kituo huku akivuta shuka ili kujisitiri,mkuu wa kituo alikurupuka mbio mpaka sebuelni,alianza kupekuwa nguo zilizo anuliwa na kuwekwa sebuleni kusubiri kupigwa pasi,alitafuta suruali na shati akavaa japokuwa zilikuwa vimejikunja lakini wala hakujali hilo,aligeuke kuuelekea mlango wa kutokea nje,aliwaona Brown na Salma wamesimama pale mlangoni,alichanganyikiwa,alipitisha mkono usoni ili kjiridhisha kwmba hayupo kwenye ndoto,aligundua kuwa hayupo ndotoni,alipiga magoti ili awaombe radhi,kabla ya kutamka neno,Salma na Brown walipotea mbele za mkuu wa kituo.

Mkuu wa kituo akiwa mwenye mawenge mengi sana,alifungua mlango haraka sana,alitoka nje na kukimbilia kituoni "eeh yule mshenzi yumo humu kweli?" aliuliza kwa sauti ya kupagawa,askari wote walimshangaa "samahani afande unamaanisha nani?" aliuliza askari aliyekuwa kaunta "yule mjinga mwenye gereji,alikuwa nyumbani kwangu sasa hivi" "haaaa haaa afande itawezekana vipi?" alijibu yule askari kama mkuu wa kituo alivyojibu masaa machache yaliyopita "mpumbavu wewe unadhani natania?" nakwambia alikuwa kwangu sasa hivi" "samahani afande...lakini afande wewe tulikwambia huyu jamaa anavituko ulibisha sasa yamekukuta unataka na sisi tuamini" "nitakuweka mhabusu wewe huna adabu" aliongea mkuu wa kituo kwa gadhabu sana,aliona yule askari alikuwa akimdhihaki.

Askari alifungua mlango wa mhabusu aliyowekwa Brown,alimwita Brown atoke nje,alitoka huku akipikicha macho kama mtu aliyekuwa amelala "wewe ulifuata nini nyumbani kwangu?" aliuliza mkuu wa kituo "mimi? kivipi ?" "anhaa unajidai mchawi siyo? sasa utajuwa kama mimi kwetu niliaga...we askari asubuhi peleka mahakamani jalada lake huyu alafu tuone kama serikali inarogwa" "sawa afande",Brown alirudishwa rumande,asubuhi polisi mwendesha mashtaka alikabidhiwa jalada la Brown,kesi ilipangwa kusikilizwa mchana,yule mama aliyetoa taarifa polisi kuhusu upotevu wa lile Lori aliitwa kama shahidi namba moja mahakama ikaanza "haya mama wewe ulisema mtuhumiwa ni jirani yako mtaani lakini hukujuwa kuwa najihusisha na uhalifu ndiyo au hapana?" aliuliza mwendesha mashtaka "ndiyo" alijibu yule mama.

Maswali yaliendelea "katika hawa watu kumi unaweza kumtambua Brown M. Kibonge?" aliuliza mwendesha mashtaka "ndiyo naweza kumtambua" alijibu yule mama kwa kujiamini sana "haya mama tafadhali pita mbele ya watu hawa na umtambue mtuhumiwa" "sawa" yule mama alianza kupita mbele ya wale watu akiwemo Brown,alipita mwanzo mpaka mwisho,akarudia tena "hapana hapa hayupo" watu waliojaa mahamakani walilipuka kwa kushangilia "weweeeee hii koboko.......kweli hamuoni au?" kila mmoja aliongea lake "eh we mama hebu kuwa serious Brown yupo kati ya hao watu hebu ionyeshe Mahakama kwa kumtambua mtuhumiwa" "mh ! hapa hayupo" "we mama unaitania Mahakama?" "Hapana kweli simuoni" "mheshimiwa shahidi ameshindwa kumtambua mtumiwa angali yupo miongoni mwa hawa tau waliosimama mbele yako...naomba uamuzi wako mheshimiwa" aliongea mwendesha mashtaka akimuomba mheshimiwa hakimu kufanya uamuzi.

Mahakama ilighairishwa mpaka siku iliyofuata,Brown alipata dhamana akarudi nyumbani,usiku Salma alimfuata Brown "hii kesi ni mbaya kwako yule mwendesha mashtaka anajua tulichokifanya mpaka yule mama ameshindwa kukutambua,ukifanya machezo huyu mwendesha mashtaka atakusumbua" aliongea Salma "kwa hiyo unashauri nini mpenzi wangu?" "tumuuwe" alionea Salma akiwa macho makavu "mh ! kuuwa tena? hayo si ndio mambo ambayo mimi niliyakataa tangu mwanzo?" "anhaa vizuri pia kama huyataki lakini chagua wewe jela miaka thelathini au huyu afe wewe uwe huru" "mh ! kuuwa hapana kwa kweli" "ohoo kwa hiyo nakukosa mpenzi wangu?" "kivipi?" " si utakuwa jela jamani" "hivi una maanisha huwezi kufanya kitu ili kunilinda?" "hakuna zaidi ya kukubali ninywe damu ya mwendesha mashtaka" Salma alizidi kumchanganya Brown.

Brown aliwaza kwa muda "kwani lazima nikubali mimi? na wewe unajuwa una uwezo wa kufanya kitu kingine ukaniokoa" "ndiyo lazima wewe ukubali ndiyo niweze kutekeleza hilo sasa unataka nifanye kitu kingine kama kipi? kumbuka una masaa machache kabla ya kusomewa hukumu ya kwenda jela" "aaagghhhhhh basi sawa" "sasa siku nyingine ukisitasita nitakuacha na sitarudi kwako mpaka majanga yakupate" Salma aliondoka kwa kicheko kikali cha kijini "haaaaa haaaaaa haaaaaaaaaaaaa aaaaa aaa aaa aaa".

Brown alikosa usingizi akiwaza yule mwendesha mashtaka,palipo pambazuka alijiandaa na kuelekea mahakamani,waliingia mahakamani alafu alikuja mwendesha mashtaka mwingine "samahani tunasikitika kutangaza kifo cha mwendesha mashtaka tuliyekuwa naye jana sasa nitasimamia mimi" moyo wa Brown ulipiga kwa mshtuko.aliwaza moyoni ni kweli Salma ameshafanya yake?,watu waliokuwa pale mahakamani kila mmoja alishtushwa na taarifa zile wakaanza kuongea kila mtu lake "order in court" aliongea mwendesha mashtaka "wote simama juu mheshimiwa anaingia" watu walitii wakasimama kwa heshima.

Maswali yalianza tena "shahidi uliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa unamfahamu vizuri sana na ni jirani yako mtaani ndiyo au hapana?" "ndiyo" "sawa unaweza kumtambua miongoni mwa hawa watu hapa mbele yako?" ndiyo naweza" "haya mama pita mbele ya hawa watu mara tatu na umguse mtuhumiwa" "sawa" yule mama alianza kupita mbele ya watuhumiwa,alianza mwanzo mpaka mwisho mara tatu "hapana hapa hayupo" 'mama ionyeshe mahakama mtuhumiwa yupo miongoni mwa hao watu hapo mbele yako" "hapana hayupo" "kwani unaona wanaume wangapi hapo?" "wanaume tisa na mwanamke mmoja" 'eh ! we mama umechanganyikiwa? hapo wote ni wanaume hapo" "hapana huyu mmoja ni mwanamke" Eh ! mheshimwa sina la zaidi naomba uamuzi wako juu ya shauri hili" mwendesha mashtaka alirudisha kesi kwa hakimu.

Brown aliachiwa huru,kwa kukosekana ushaihidi,alirudi nyumbani kwa furaha japokuwa furaha iliondoka alipomkumbuka yule mwendesha mashtaka,alipofika nyumbani alikuta kuku wake wa kienyeji kama ishirini na tano wameibwa,alikasirika sana,alianza kupepeleza walipouzwa kukuwake,Salma alimwambia usipate tabu kukuwako wapo sokoni Kisutu,Brown alienda mpaka sokoni,alizunguka mpka akalifikia banda walilomo kuku wake."ee bwana za saa hizi?" Brown alimsalimu muuza kuku "nzuri karibu" "ahsante sana naomba kuketi maana nimechoka" "hapana tabu keti tu" Brown aliketi na kuanza kuongea "ndugu yangu samahani hao kuku unaouza ni wangu umeuziwa kukuwa wizi" "nini? unawazimu nini wewe!" "haaaa haaa sasa kama nina wazimu au mzima itajulikana sasa hivi usiwe na haraka" "kuku wako wana alama gani unataka kunijazia Inzi tu" aliongea kwa kugomba muuza kuku.

Brown alimwangalia yule muuza kuku kwa muda huku akisugua ile pete yake "sasa kama  hao kuku ni wako watoe humo bandani" "nikutolee unanunua au unataka usumbufu tu mjomba?" "namaanisha watoe hata wawili tu" muuza kuku alikubali akaanza kukamata kuku,dah ! ikawa kamata kamata na wewe,kuku hawakushikika,nusu saa ilipita bila kutoa kuku hata mmoja muuza kuku alikuwa hoi "sasa pumzika nikuonyeshe kuwa hao kuku ni wangu"...................... ITAENDELEA



No comments: