MPENZI CHEUPE 09




"aaahggggrrrrrrrrhhhh" aliungruma Salma kama mwenye gadhabu kali,alimwachia Brown na kumnyooshea kidole "wewe umezubaa sana ilikuwaje uwaachie hawa wachawi wakukamate" alifoka Salma "ah sasa ningefanyaje mpenzi wangu?" "sasa hiyo pete ni ya nini hapo kidoleni mwako kama hujui jinsi ya kuitumia?" "ah hukuniambia mimi ningejuaje?" "wewe ungeisugua mara mbili hiyo pete hapo kwenye hicho kito chekundu ungeona balaa ambalo lingewapata wapumbavu hawa" "basi nimekuelewa nitakuwa nikifanya hivyo" "ipo siku nitakuacha wakutese kwanza ndio upate akili" "basi nisamehe mpenzi wangu nimekosa sitorudia tena" "sawa sasa utakaporudi duniani usiende kule ulikokuwa unaishi mwanzo kule hawakujui tena wakati ule ulikaa huku miaka thelathini ya duniani wewe uliona kama siku tatu ndiyo maana uliporudi uliona mabadiliko na watu hawakujui tena"

"duh ! hii kali" alishangaa Brown huku macho yamemtoka "usinitumbulie mimacho yako nataka kipindi hiki ufikie Kigamboni utafanya biashara za halali na haramu na zote utafankiwa lakina hasa za haramu" "mh ! za haramu kama zipi?" "tulia mtotot wa kiume mbona wasiwasi kama moyo wa jipu?" "haaaaa haaaa mpenzi wangu unanifurahisha sana" "baso nitakufurahisha zaidi huu ndio kwanza mkoko unaalika mauwa" "una maanisha nini sasa?" "yaani hapa ni mwanzo bado yapo mengi utayafanya na mengi utayashuhudia" "mh ! kazi kweli" "tena si kodogo atii nakuongezea nguvu sasa utakuwa na uwezo wa kufanya mambo makubwa sana kama kusafiri umbali mrefu kwa muda mfupi na mengine utakayotaka kufanya" Salma alimchukuwa Brown mpaka chumbani kwake,wakapiga mechi alafu alimrudisha katika ulimwengu wa kawaida.

Brown alianza maisha mapya,alikuwa akiuza pweza maeneo ya ferry nyakati za jioni,aliuza kuliko muuza pweza yeyote pale ferry,biashara ikakuwa,alitamani kufanya na biashara nyingine,alianza kwa kufungua gereji maeneo ya Mlaliji (Mural Jee),gereji iilijulikana kwa jina la Brown Auto Mechsi,gereji likuwa kwa kasi sana wateja walimiminika kwa wingi,Brown aliingiza pesa ya kutakata,maisha yalinyookea akajua sasa ameukata,mgari ya kila aina yaliletwa kutengenezwa,kunyooshwa na kupigwa rangi,kazi za gereji ya Brown zilisambaa mbali sana ndani na nje ya jiji la Dar,sifa zilifika mpaka kwa wezi walioshindikana,wezi wa mizigo bandarini,walienda kuiba bandanri kwa kutumia Lori aina ya Scania kwa kulipachika namba za usajili za bandia na kisha kuja kulitelekeza lile Lori kwenye gereji ya Brown.

Wale wezi walifika kwa Berown na kujitambulisha "sisi ni kampuni kubwa ya usafirishaji,tunataka utupigie rangi gari yetu itakuwa kiasi gani?" Brown bila kuchelewa alichukuwa kikokotoo alipiga hesabu "itakuwa milioni saba na nusu bosi wangu" alijibu Brown huku akitabasamu :sawa sisi tutakupa nane kabisa ili unyooshe na sehemu zilizopinda itachukuwa muda gani?" "sawa bosi wangu... mmmmh itachukuwa wiki moja tu" "safi sana kweli wewe upo kikazi zaidi" wale wezi waliondoka na gari wakaiacha pale gereji,ikapita miezi miwili wale wezi hawakurudi,magazeti yaltangaza upotevu wa lile gari pamoja na wizi uliofanyika bandarini,Brown hakuwa na taarifa zozote kuwa lile gari linatafutwa,ikatokea mama mmoja aliyekuja kuteneneza gari,aliliona lile gari pale gereji akalifananisha na lile analoliona kwenye gazeti,kimya kimya yule mama alikwenda kutoa taarifa polisi.

Brown akiwa hana hili wala lile alishangaa akizungukwa na polisi wenye bunduki "tulia hapo hapo upo chini ya ulinzi" alisema polisi mmoja huku akiwa ameelekeza mtutu wa bunduki kwa Brown,alitulia,askari walimpekuwa na kisha kumfunga pingu,walimpakia kwenye gari na kuondoka naye,walipofika kituoni,walimchukuwa maelezo,walimwamuru avue mkanda wa suruali,kama ana pesa na simu akabidhi kaunta,walipomtaka avue pete hapo ndipo mbilinge ilianza,ikawa vua vua na wewe,pete haikutoka kidoleni,muda wote Brown alikuwa kwenye bumbuwazi kwasabau hakuwa amejuwa kosa lake,walishindwa kuivua ile pete,waliamua kumweka rumande akiwa ameivaa.

Usiku Salma alimtokea "acha ujinga wewe tumia hiyo pte watakufunga wajinga hawa" Brow alizinduka aliisugua mara mbili alafu alitamka "nataka kuwa nje" mara alijikuta nje ya kituo,polisi waliokuwa doria walipatwa na mshtuko "huyu siyo yule jamaa mwenye gereji aliyeletwa leo mchana?" aliongea polisi mmoja wa zamu huku akiwa ametoa macho ili kumwangalia vizuri,Brown hakuondoka eneo la kituo,alikuwa kiazungukazunguka tu ili kuwatisha,ashkari wale walienda kumwangalia ndani,walipofungu vyumba vya mahabusu walimkuta ndani,uwoga uliwaingia askari,walipiga simu kwa mkuu wa kituo,alikuja haraka "kuna nini hapa?" aliuliza mkuu wa kituo "afande hapa pana maajabu yule jama wa gereji aliyeletwa leo mchana yupo humu ndani na pia tunamwona kule nje" "haaaa haaaa haiwezekani kabisa mh mh mh ! amewahonga ndiyo mnatafuta sabau za kumtoa eeh sasa ole wenu".

Mkuu wa kituo aliondoka akiwa mwenye hasira za kukatihwa usingizi wake,aliamini ni upuuzi mtupu,alirudi nyumbani kuendelea kulala,wakati usingizi unaanza kumchukuwa,alisikia akipapaswa nyayo.alishtuka "nani tena?" aliuliza kwa mshangao uliochanganyika na woga,alikimbilia kuwasha taa,alipowasha taa tu uso kwa uso na Brown na Salma akiwa kwenye sura ya kutisha alisimama nyuma ya Brown..................ITAENDELEA.



No comments: