MPENZI CHEUPE # 08




Wachawi wote waliokuwa wakimtisha Brown walipatwa na mshtuko,walianza kurudi nyuma,Salama alitua mbele yao huku radi zikimzunguka "huyu lazima atakuwa binti wa miungu" alisema yule mama kiongozi wa wale wachawi akiwa katika halia ya kutetemeka,alikuwa akitafuta namna ya kukimbia,Salama alijua kuwa yule kiongozi wa wale wachawi anataka kukimbia "wewe tulia ulipo ukitoweka tu umekwisha" aliongea Salama akiwa mwenye hasira sana "nisamehe malikia wangu nilik....." "kelele wewe ulitaka kumtesa huyu mume wangu amekufanya nini?" "hapana sikutaka kumtesa nilitaka nimshauri ajiunge nasi" "mwongo wewe hukuona lama ya himaya yetu kichwani mwake? alafu vinguvu vyenyewe unavyo kidogo sana unajidai na wewe gangwe haya sasa pambana na mimi"

"hapana hapana malkia wangu sithubutu kupambana na wewe" "sasa itakupasa utoe kafara mwanao mmoja ili kufidia kosa lako" "malikia wangu watoto wamebaki wawili tu wengine nilishawatoa" "anhaa sawa vizuri sana sasa naanza na wewe mwenyewe" "tafadahali malkia wangu si mbele ya hawa wafuasi wangu" "ndio vizuri nata waone na wajue wakikengeuka na kutesa watu bila hatia nini kitwapata" "mama weee uwiiii mama nakufaaa unautoa moyooooo" alipiga kelele yule mama mchawi,Salma alinyoosha mkono wake na kuukita kifuani mwa yule mama,alikuwa akiunyofoa moyo wa yule mama mchawi,kelele za kuomba msaada zilisikika mpaka kwa wachawi wenzake,walijipanga kuja kumsaidiawalipofika walimuona Salma,walishtuka,kugeuza walishindwa,mmoja wa wale wachawi kwa jina mzee Kazengo,aliamua kujaribu kupambana na Salma.

Wenzake mzee Kazengo walijaribu kumsihi asijaribu kwasababu Salma ni mpole lakini akikasirika atawapoteza wote,maneno hayo haya kumwingia mzee Kazengo,alianza kwa kurusha bomu la mkono.Salma alicheka kwa dharau sana "haaaaaa haaaa haaaa unanijaribu hunijui sasa utakuwa fundisho kwa wengine" alimyooshea kidole mzee Kazengo alafu alianza kukishusha taratibu kuelekea chini,kadiri alivyoshusha kidole ndivyo, mzee Kazengo alivyokuwa akikunjamana na kuwa mfupi,mifupa yake ililia kama hali ya kuvunjika,damu zilimvuja,Salma alitoa ulimi wake mrefu akalamba damu a mzee Kazengo,lile kundi la  wachawi waliokuwa pale walistaajabu,walianza kulia na kuomboleza,walijuwa huo ndiyo mwisho wa mzee Kazengo,wakati wote mzee Kazengo aliugulia maumivu,alibadilika na kuwa na urefu kama wa mita mbili au tatu.

Salma alianza kutembea kuwafuata wale wachawi,wachawi walimwogopa Salma walikuwa wakirudi nyuma Salma alipiga hatua "wote sogea hapa' Salma alitoa amri kwa sauti kali,walianza kurudi kumsogelea Salma huku wameinamisha vichwa vyao chini "bado nina kiu ya damu jichagueni kati yenu nimnyonye nani?" aliongea Salma,wachawe wote vifua vulikuwa vinapanda na kushuka,walikuwa wakitazamana usoni bila kupata jibu,Salma alipita katikati yao kama Rais anakagua gwaride,kila mchawi alikuwa akitetemeka,walihofia kuwa Salma anaweza kuchagua mwenyewe,mara alimchagua mama mmoja "hapana hapana malkia wangu mimi nina watoto wadogo" alilalmika yule mama mchawi "kwa hiyo? aliuliza Salma "bado wananitaji mimi tafadhali" "mimi nilikuwa binti mdogo mrembo kwa ushenzi wenu mkanileta huku sasa chakula changu ni damu na nyama unataka nikale wapi?".

Yule mama aliishiwa maneno,Salama aliendelea kuzunguka alimgusa mwanaume "wewe nadhani utanifaa sana "malkia wangu mimi bado hata sielewi chochote ndio kwanza nimejiunga miezi miwili iliyopita nihurumie kilinileta nini mimi huku" "haaaa haaaa mnapenda uchawi alafu mnaogopa kufa mbona ninyi mnauwa?" aliongea Salma akiwakebehi wale wachawi, wakati wote huo Brown alikuwa kimya akishuhudia mambo mazito,alikuwa ameketi chini bila wasiwasi kwasababu mlinzi wake yupo kuwaadabisha wabaya wake,alitamani sana Salma afanye kitu kingine cha ajabu kisicho wezekana katika ulimwengu wa kawaida lakini Salma alikuwa anakawia kuwatenda mambo mabaya na kuufanya moyo wa Brown kutotulia.

"mpenzi wangu Salma si umchukwe huyu na huyu alafu huyu na huyu wape adhabu kali wengine wote wasamehe" aliongea Brown "sawa mpenzi wangu ameshanisaidia haya aliowachagua nyanyukeni" waliiinuka wanaume wawili na wanawake wawili,vilio vilitawala wale wachawi waliwaomboleza wenzao,Salma alimshika mwanaume wa kwanza akamvuta karibu,alipeleka mdomo wake shingoni mwa yule mwanaume,alimuuma kama dakika moja alafu alimwachia,yule mwanaume alibadilika rangi na kuwa mweupe,alianguka chini,wale wachwi walishika vichwa kwa uchungu wa kuondokewa na mwenzao,Salma alimshika mwanaume wa pili kumnyonya shingoni,alimwachia na kumshika mwanamke,alinyofoa matiti kisha alimyonya damu kipitia matobo ya yale matiti,alimwachia mwanamke yule alianguka chini,alimshika mwanamke mwingine ambaye alikuwa wa nne kuchaguliwa na Brown.

Yule mwanamke alikuwa akilia sana,aliogopa kufanyiwa kama wenzake waliomtangulia katika adhabu ile,Salma alimwangalia kwa macho makali alafu alipiga kelele kali sana iliyopasua masikio ya yule mwanamke,damu zilianza kutoka masikioni,Salma alinyonya damu ile kupitia sikio la kushoto,alimkausha damu na kumwachia,yule mwanamke alianguka chini,Salma alinyoosha kidole chake cha shahada zile maiti za wale wachawi zikapuputika na kuwa majivu,wale wachawi walianza kumsujudia Salma "kuanzia sasa mtakuwa chini ya himaya yangu ya miamba na moto,himaya ya bahari haitawaona tena mmenielewa?" "ndiyoooooo" wale wachawi waliinuka na kuanza kumpigia makofi malkia wao mpya,aliwapa ishara wapite mbele yake,aliwatia alama juu ya nyusi ambazo wakionana wao kwa wao wanatambuana kuwa ni wa himaya moja ya miamba na moto.

Salma alimshika Brown begani "pole sana mpenzi wangu"  "ahsante sana mpenzi wangu hakika uliahidi kunilinda na kweli umenilinda" "acha unafiki Brown hayo maneno ni ya kinafiki hayajatoka moyoni nakuona unaniogopa" aliongea Salma huku akitoa kucha zake ndefu na mdomo wake uliolowa damu na meno marefu aliusogeza shingoni mwa Brown...................ITAENDELEA



No comments: