MPENZI CHEUPE 07




"Mh wewe si Brown wewe" aliuliza Dula " ah ndio mimi" alijibu Brown, mara Dula alimwita yule dereva tax pembeni "we bwana huyo jini" "kivipi sasa?" "huyo jamaa alikufa kitambo sana" mara Dula na yule dereva tax walianza kutimua mbio,pale kijiweni hakubaki hata dereva mmoja,wapita njia na wao waligeuza njia na kukimbia bila kujua sababu ya kukimbia.

Hali ya taharuki ilitanda pale maeneo ya Amana,habari zilisambaa maeneo ya jirani kuwa kuna jini Amana,watu walifurika maeneo ya jirani ili kumuona jini, wengi walipatwa na sintofahamu kwa kumuona jini aliyevaa shuka nyeupe tena zenye chapa ya bohari la madawa msd,Polisi walifika eneo la tukio, walimkuta Brown amekaa chini ame egemea masanduku ya barua " wewe ulitoroka hospitali?" aliuliza mmoja wa wale Polisi,Brown hakujibu kitu,Polisi walimwinua wakampakia kwenye gari na kuondoka naye na kuwaacha watu wakiongea maneno mengi yakiwamo maswali yasiyo na majibu.
Brown alifikishwa kituoni akiwa mwenye mawazo sana, alishindwa kuelewa wale madereva tax walivyodai alikufa wakati yeye anaona kuwa aliondoka kama siku tatu zilizopita,polisi walianza kumhoji lakini Brown alipotaka kueleza Salma alimtokea huku akiwa ameweka kidole cha shahada mdomoni kama ishara ya kumtaka asiseme chochote ,Brown alizidi kuchanganyikiwa,alianza kupatwa hasira, maisha aliyaona machungu.

Polisi walizidi kumwuliza maswali, lakini Brown alikuwa kimya hakuongea neno zaidi ya kutokwa machozi,Polisi walishindwa kumwelewa Brown, walikubaliana wamwache kwanza atulize mawazo kwanza.Baada ya kama saa mbili kupita,pale kituoni alikuja mkuu wa kituo " haya huyu vipi na mashuka yake" " afande huyu ni yule aliyeokotwa jana pale kando ya barabara ya uhuru" "sasa mbona yupo hapa?" "Afande amezua taharuki wananchi wanahisi ni jini" " jini? yaani huyu jini?" "Ndio afande " " jini gani ana nyusi anapepesa macho?" "Afande yaani watu wakimuona wanaweza kuumia au kumpiga hawana imani naye kabisa" "haya tufanyeje sasa?" "Afande....afande afande...." aliongea yule askari bila kumaliza kauli,aliona kitu cheusi angani,upepo mkali sana ulivuma, upepo ulitua mbele ya kituo Brown own own own own wn" sauti ilisikika kutoka katikati ya ule upepo,Polisi wote wapatwa na taharuki, wenye imani zao potofu bado kidogo kuzimia,iliwalazimu kumtoa nje Brown, upepo ukamzunguka Brown, ulizunguka kwa muda kama dakika moja, alafu upepo ulitoweka kwa kupanda juu sana angani,Brown alitoweka kwenye mazingira ya kutatanisha,baadhi ya askari waliogopa na waliamini Brown ni jini, habari zikasambaa, magazeti yakaandika habari za Brown.

Brown alijikuta katikati ya kundi kubwa sana la watu, walikuwa wamevalia kaniki nyeusi, weusi sana kama vile walipaka masizi,mapigo ya moyo wa Brown yaliongezeka, hakuwa akiwafahamu hata mmoja,mara alitokea mwanamke mmoja ameshika usinga mkononi "Brown pendapenda leo upo kwenye mikono yetu haaaaa haaaa " aliongea yule mama huku akimsogelea Brown, aliinua usinga wake juu ili amchape nao Brown lakini kabla hajashisha ule usinga kilisikika kishindo kikubwa sana,Salma alikuwa amefika.........ITAENDELEA



No comments: