MPENZI CHEUPE 06




Alimuona kiumbe wa kutisha sana,wale wote waliokuwa pale hawakuwa wwanatisha kama huyo,yule kiumbe alimwangalia Brown kwa jicho kali sana kiasi cha kumfanya Brown aishiwe pumzi na kutaka kuzimia,Salma alichukuwa kipande kingine cha nyama ya binadamu na kumsogelea Brown,alimpelekea mdomoni,Brown hakuwa na namna zaidi ya kufungua mdomo,aliwekewa kipande cha nyama,alifumba macho,akataka kutapika lakini alijizuia "ooogggghhhh" alianza kutafuna akiwa mwenye kinyaa sana,alipomeza tu,shangwe za kijini ziliitawala eneo lile "sasa mpenzi umefaulu mtihani mkubwa njoo univike pete" Brown alisogea.mdomo wake ukiwa umelowa damu na michirizi mingine kwenye shati lake.

Brown alipokea pete toka kwenye mkebe maalumu mwekundu,alikuwa inawaka sana,dhahabu safi,aliishika mkononi na kuitumbikiza kwenye kidole cha Salma,na Salma alichukuwa pete yenye kito chekundu katikati na kumvisha Brown,ndipo yule kiumbe wa kutisha alimshika mabegani,Brown alipokea nguvu za kuzimu "mmmh mmmhhhffff" aligugumia Brown,shangwe ikaongezeka,nyama na damu zikanywewa,Salma alimshika Brown kimahaba na kuelekea naye kwenye chumba chake,kilikuwa chumba kikubwa sana,kilipambwa na vito vya thamani kubwa sana,palikuwa na kitanda cha malkia,dressing table iliyojaa kila ina ya manukato,chetezo za ubani "karibu mpenzi wangu hiki ni chumba chako kuanzia sasa jisikie huru" aliongea Salma huku akipunguza nguo za Brown mwilini.

Brown alikuwa hoi kwa matukio yale,Salma alimwonyesha Brown bafu ili aoge,lakini Salma yeye hakwenda kuoga,Brown alioga,alitoka na kujifuta maji kwa taulo safi jeupe,alipomwangalia Salma,alimwona ameshika vichupa mikononi mwake "ukimaliza sogea hapa nikupe maelekezo" aliongea Salma,Brown alisogea "nakusikiliza mpenzi wangu" alijibu Brown "sasa hapa pana miiko mitatu lazima uchague mwiko mmoja utakaoutekeleza maisha yako yote" "miiko gani mimi siwezi mambo hayo" "sikiliza Brown wewe umeshakuwa mume wangu na nilipokuwa duniani sikuwahi kuolewa hii ni ndoa yangu ya kwanza,kwa hiyo nataka nikupe mali ili usiteseke na maisha" "sawa lakini isjie ikawa kuuwa mtu sijui kutoa kafara mimi siwezi kabisa hayo mambo" "hapana wala si hayo haya ni rahisi tu" "sawa".

Salma alitabasamu "sawa sasa mwiko wa kwanza iwe marufuku maisha yako yote kuwa na mwanamke mwingine yeyote zaidi yangu na ukiwa naye tu nitamuuwa,mwiko wa pili nikufanye upate shepu ya kike na marufuku kuona aibu wala kujifunika usionekane,mwiko wa tatu,uwe hanithi ukiwa duniani na ukija huku utakuwa mzima" "duh ! bora nisiwe na mwanamke mwingine" "umejibu vizuri sasa hii chupa ya kwanza ni dawa ya kukuza biashara,hii ya pili ni kwa ajili ya ulinzi wako na hii ya tatu ni kwa ajili ya kufungua milango ya kuzimu ili uingie huku,lakini kabla ya kuitumia hii lazima utangulize yali la kuku wa kienyeji pale kwenye mlango,ndipo utaweza kufubgua mlango umenielewa" "sawa mpenzi nimekuelewa" wakati huo Salma alikiwa kwenye umo zuri sana la mwanamke isipokuwa meno yake tu yalikuwa marefu kuliko kawaida.Brown alishamzoea.

Brown na Salma waliangaliana kwa macho ya mahaba,licha ya kuwa Brown alikuwa amechoka ilimlazimu ashughulike hata kidogo,alimsogelea Salma,alimshiki kiunoni,Salama alijilegeza na kujiachia mikononi mwa Brown,walisogelea kitanda,Salma alilalia mgongo na Brown alikuja juu yake,walipiga mechi kali sana yaani ya kibabe,kwa muda wa saa tatu Brown alikuwa hoi,alijitupa pembeni na kupitiwa usingizi mzito sana,akiwa usingizini aliota viumbe wa ajabu wengi walikuwa wakimfurahia jambo liliomshangaza,alikuwa akiwaogopa kwasababu walikuwa wanatisha sana,kwa mbali alianza kusikia sauti "ee bwana ni mwanaume lakini bado anapumua njoo haraka tumsaidie" ziliambatana na kelele za watu wengine wengi "eehana nguo bwana sijui alikuwa anwanga wapi?" "itakuwa kachelewa kurudi" "wenzake walimwacha" "aliishiwa mafuta huyu" kila mtu alisema lake kwa waliokuwa eneo la tukio.

Brown alikutwa amelala kando ya barabara ya uhuru alfajiri,alikuwa hana nguo hata moja na alikuwa na masizi mwili mzima,aliokotwa na wasamalia wema,walimpeleka polisi,alihojiwa lakini hakuweza kueleza chochote,polisi waliamua kumpeleka Hopsitali ya Amana,alipokelewa na kupewa kitanda,alichukuliwa vipimo,baada ya muda majibu yalitoka kuwa hakuwa na tatizo lakini cha kushangaza alikuwa kama mtu aliyelewa,walimwacha apumzike,giza lilipoingia alitoroka na kwenda nyumba aliyokuwa akiishi,aalikuwa amejifunga shuka za hospitali,alipofika kwake alipotea,alikuta kuna ghorofa jipya limejengwa,alijiuliza kuwa ni pale au pengine maana palikuwa na nyumba ya kawaida tu sasa anaona ghorofa,alienda mpaka kwenye duka moja liliokuwa mtaani kwake alikuta muuzaji si yule anayemfahamu.

Aliamua kuuliza vijana waliokuwa wamesimama pembeni ya lile duka "za saa hizi jamani samahani naulizia nyumbani kwa Brown" :hapana hatumfahamu" alizidi kuchanganyikiwa "Brown aliyekuwa anaishi nyumba ile" aliongea Brown huku akionyesha kwa kidole pale ilipokuwa nyumba aliyokuwa anaishi "pale sisi tumelikuta hilo ghorofa" duh ! ilikuwa vigumu Brown kuamini anachosikia,alianza kuondoka taratibu bila kujua anapoelekea,alifika maeneo ya Amana posta,aliketi chini na kutafakaria,aliamua kumfuata mooja wa madereva tax waliokuwa wakipaki pale Amana "za saa hizi samahani naulizia nyumbani kwa Brown" alikuwa akiuliza hivyo kwa lengo la kuona kama watu watamkumbuka au watampa taarifa zozote muhimu kumhusu yeye "dah mimi brown simfahamu ila niliwahi kusikia stori kitamb sana,alikuwa anaishi mtaa huo lakini sijiu alikufa sijui ndugu zake walimtoa kafara wakauza nyumba yaani sina uhakika....kwani upoje naye wewe?"

"mimi ni ndugu yake nimekuja toka mkoani nikakutana na wahuni wakanivua nguo na kunichukulia kila kitu" aliongopa Brown ili apate msaada wa nguo "duh ! kweli Dar es salaam noma sasa hebu subiri kwanza.... oya Dula njoo mara moja" dereva tax aliita dereva tax mwingine "hebu msikilize huyu jamaa kwanza" "jamaa gani?" "si huyu hapa humuoni au?" "mh ! wewe si...................ITAENDELEA



No comments: