MPENZI CHEUPE 05




Brown alikuwa ameingia kwenye himaya ya mauza uza,Brown alimfuata Salma mpaka kwenye eneo ambalo lilikuwa na mawe mengi makubwa sana.alipita katikati ya yale mawe akiwa katika hali ya woga maana hapakuwa na nuru kabisa,mbele kwa mbali aliona kama mlipuko wa volkano,alitumaini panaweza kuwa na kijiji,aliapata matumaini,lakini alipofika eneo lile hakuona kijiji wala mtu,aliona pembeni ya ile volkano kuna mlango,ghafla ulitokea mkono kubwa sana wenye kucha ndefu za kutisha,ulimshika Brown mgongoni na mara ule mlango ulifunguka kwa mtetemo mkubwa wakutisha,ule mkono ukaanza kumsuma Brown kuelekea ule mlango,Brown alijikuta hana nguvu ya kukataa,aliingia ndani,alipofika ndani aliona majeneza mengi sana yamepangwa kama kwenye ukumbi,mara ule mlango ukajifunga kwa nguvu.

Mara ulitokea mwanga mweupe lakini hafifu,aliangalia pande zote nne hauona kitu ila alisikia kelele zikitokea kwenye ngazi iliyokuwa ikishuka chini,mara jeneza moja lilifunguka, Brown alipata usahwishi wa kwenda kuliangalia,alikuta binti mdogo amelala,wakati akimwangalia aligundua kwamba yule mtoto alibadilika na kuwa mkubwa,na alikuwa hai,macho yalimtoka,alianza kurudi nyuma yule mtoto akawa mwanamke mzima alinyanyuka na kuketi akiwa bado ndani ya jeneza "Brown my darling" aliongea yule mwananmke,hapo Brown alishtuka sana na kuanza kutetemeka "we..we ni nani?" "sogea karibu utanifahamu" Brown hakuweza kusogea kwa kuwa aliogopa.

Yule mwanamke alitoka kwenye jeneza na kusimama pembeni ya lile jeneza "Brown sogea sogea gea gea"sauti ya yule mwanamke ilisikika huku ikijirudia rudia kama mwangwi,Brown alianza kusogea katika hali ya woga sana,yule mwanamke alianza kutembea kumfuata Brown,alikuwa akibadilika na kuwa Salma,dah ! hapo Brown aliishiwa pozi,alitaka kukaa chini lakini Salma alimzuia "nifuate" aliongea Salma,Brown alianza kumfuata tena,Salma alielekea kwenye zile ngazi na kuanza kushuka moja baada ya nyingine na huku akigeuka geuka kumwangalia Brown.

Walipo maliza zile ngazi, Brown aliona sehemu kama ukumbi wa sherehe umepmbwa kwa vitambaa vyekundu,kulikuwa na viumbe vya kutisha sana wameketi kwenye viti vya ule ukumbi,walikuwa na kucha ndefu,meno marefu makali,wote walikuwa wakimwangalia Brown kama wanamtamani,mmoja wao alisema kwa sauti kali "nasikia harufu ya binadamu nataka damuuuu",walianza kumsogelea,lakini kabla hawajamgusa,walikemewa na mwanamke aliyekuwa ameketi mbele kwenye kiti cha enzi yake,alimwonyesha ishara Brown aende kule mbele,alianza kuzipiga hatua kwenda kule mbele akiwa katika hali ya woga sana,alitetemeka mpaka meno yalikuwa yakigongana "karibu Brown karibu sana umekuja tufunge ndoa mpenzi karibu sana" aliongea yule mwanamke huku akiinuka kwenda kumlaki Brown,alimfikia na kumpapasa mashavuni.

Ghafla aliinua kidevu cha Brown kwa nguvu sana "mhhggghh" aligugumia Brown kwa maumivu ya kucha za yule mwanamke,yule mwanamke alifunua shela yake aliyokuwa maeivaa na kujifunika usoni,ndipo Brown alimtambua kuwa alikuwa ni Salma "Salma mbona wanifanyia hivi?" aliuliza Brown huku akimeza mate maana alihisi koo kukauka "haaaaa haaaaaaa haaaaaa Brown ulinipenda sana mimi najua na mimi nimekupenda sana ndiyo maana nimethubutu kukuleta kwenye himaya yangu" "sasa nimekosea nini mbona wanitisha hivi?" "sikutishi mpenzi nitakulinda muda wote hawa wote wapo chini yangu hakuna wa kukudhuru hapa" "sasa lengo lako nini?" hilo swali lilimuudhi Salma "Brown mbona unakuwa mpumbavu unataka kuniaibisha?"

Salma alionekana kuchukia sana "wewe mwenyewe ulikuja kwangu na sasa unajifanya huelewi? ebo!" "samahani Salma sijamaanisha hivyo" "kumbe umemaanisha nini?" "mazingira haya mimi siyajui kabisa na kwa kweli naogopa sana" 'unaogopa nini utazoea tu mbona mimi nimeshazoea na mimi nilikuwa mgeni kama wewe" "sawa Salma nimekuelewa" "usiniite Salma...niite mpenzi Salma" "sawa mpenzi Salma" "haya lete vinywaji na nyama tule sherehe ianze" zilipigwa shangwe za kutisha sana,wale watu walikuwa kama wanaunguruma,vililetwa vikombe vilivyojaa damu ya bina damu,alafu zililetwa maiti mbili za binadamu wa kike na wakiume,vichwa vyao vikiwa vimekatwa na kuwekwa kwenye sahani pembeni ya miili yao,Brown aliltetewa visu vikubwa viwili achague kimoja.

Brown akiwa katika hali ya sintofahamu alichagua kisu kimoja,alafu alipewa kitu kama Uma na kupewa ishara akate kipande toka kwenye mwili ule wa kike,Brown alikata huku akitetemeka "jikaze mtoto wa kiume wewe" aliongea Salma,Brown alikata na kuweka kwenye sahani ya udongo,alipewa ishara na mmoja wa wale apambe waliokuwa karibu na Salma kuwa amlishe Salma,Brown alimsogelea Salma na kipande kimoja mkononi,samu zilichirizika kwenye mkono wa Brown toka kwenye kile kipande,alimlisha Salma huku akiwa amegeukia pembeni,mara alihisi mkono mgumu,wa baridi ukimgusa kidevuni na kumgeuzia kwa Salma,alikuwa mmoja wa wale watu wa ajabu akimgeuza Brown,aligeuka huku amefumba macho,alisikia amenaswa kofi shavu la kushoto,alifumbua macho ili kumwangalia aliyempiga,daah aliishiwa nguvu.................ITAENDELEA



No comments: