MPENZI CHEUPE 11




Brown aliketi vizuri kwenye kiti mbali na lilipokuwa banda la muuza kuku,watu walianza kusogea na kujaa pale alipokuwa Brown,alianza kwa kuita majina ya wale kuku wake "Kuzi,Kizi,Kanu,Keto,Khanga,Khail....." kila kuku aliyesikia jina lake aliruka mwenyewe toka bandani mpaka miguuni mwa Brown,kelele za shangwe,vifijo,miluzi matusi vilisikika pale sokoni,soko lilizizima kwa muda,shughuli zote zilisimama,maana kilichokuwa kinatokea hakijawahi kuonekana mahala popote,wachuuzi wa pale sokoni walivutiwa na Brown,kila mmoja aliomba namba za simu za Brown,alionekana shujaa na mganga kweli kweli,pale sokoni kumbe wengi wao hufanya biashara kwa imani za kishirikina,walikuwa wakishangaana wao kwa wao.

Muuza kuku aliona aibu na kujisikia vibaya,alikuwa akitetemeka kwa kutikujuwa hatma yake "blaza naomba nisamehe sana sisi huwa tunaletewa tu hawa kuku ni ngumu kujuwa kama ni wa wizi au lah..."pole sana usijali ila siku nyingine uwe na kauli nzuri kwa mtu anayekujia kistaarabu" "sawa blaza nimekuelewa" "eeh ! siku nyingine utageuzwa pimbi jinga kabisa wewe na sasa hawa kuku utawabeba wewe mpaka nyumbani kwangu" "sawa blaza hamna shida nitabeba" waliongozana mpaka nyumbani kwa Brown,muuza kuku akarudi zake sokoni,baada ya Brown kupumzika Salma alikuja na kicheko "haaaaaa haaaaa haaaaa safi sana mume wangu kipenzi Brown Martin Kibonge yaani umenifurahisha sana leo" 'mh ! si bure wewe una jambo unataka kuniambia au kuniongezea mizigo si bure kicheko hicho" "ni kweli mpenzi sasa umeanza kunielewa kabla sijatamka kitu hiyo ni dalili nzuri sana"

brown alikuwa amejiinamia akiwaza ni nini Salma anataka kumweleza na je akikataa itakuwaje? "weeeh ! kataa uone" alongea Salma baada ya kuyasoma mawazo ya Brown "haya basi si uniambie" "vizuri sasa itakupasa uwe mganga" Brown alishtuka sana aliinua uso na kumwangalia Salma kwa ghafla sana "unashtuka nini haaaa haaaaa haaaa utapendezaje ukiwavaa kaniki,simbi zikipishana mabegani mwako haaa haaa utapendeza sana" "ah mimi siwezi bwana kama ndio hivyo bora nife tu nishachoka mimi" "unasemaje wewe unajuwa nini kuhusu kufa wewe unaleta mchezo eeh sasa subiri njikuonjeshe" Salma alipotea kwa hasira mbele za Brown "Salma Salma Mpenzi Cheupe daaah nimesha lichuma",Brown alikula na kwenda kulala kwa kuwa alikuwa amechoka sana.

Asubuhi kulipopambazuka Brown alitaka kuamka lakini alishindwa kutokana na kujihisi mzito sana,alijilazimisha na kufanikiwa kusimama kwa taabu,alishindwa kusimama amenyooka aliinamia upande wa kushoto,maumivu ya mbavu na mgongo yalikuwa makali sana kadiri muda ulivyokwenda ndivyo hali ilizidi kuwa mbaya,ubavu ulizidi kujipnda "Salma Salma mpenzi wangu nisamehe sana nimekubali yote unayotaka" aliongea Brown kwa huruma sana huku machozi yakitiririka mashavuni mwake kwa maumivu aliyoyapata,ghafla alisikia kicheko na maneno "haaaaa haaaaa na bado utabaki hivyo mpaka jioni wewe si jeuri?" "hapana Salma inatosha sasa nakubali kila kitu" "mmmh mtoto wa kiume wacha ulele mama kidogo tu je ingekuwa na hii" mara Brown aliona mkono na mguu wake umebadilika na kuwa kama wa mtu aliyepooza "mmhhh mhhhh shhhssshhh" aligugumia na kupumua Brown kutokana na maumivu aloyoyapata.

Hali ya Brown ilikuwa tete,jioni aliina ipo mbali sana,aliomba msamaha lakini Salma alikataa kumwondolea zile adha,mchana wote Brown alishinda nyumbani tena bila kula,ilipofika jioni Salma alikuja kwa Brown "eeh cha ubishi unajisikiaje?" alionge Salma huku akimzunguka Brown aliyekuwa taabani amelala kwenye sofa "naumwa Salma naomba nisamehe sana..... niondolee hali hii ili niweze kukusikiliza vizuri" "hata hivyo unanisikia vizuri sana" "daaah mmmgghhh" "sasa sikiliza kwa kuwa umejipatia jina kubwa pale sokoni lazima uifanye kazi ya kuagua watu" "sawa nita...fanya hivyo" Brown alijibu huku akigeuka na kumwangalia vizuri Salma "wateja wa kwanza ni wale waliochukuwa namba zako za simu pale sokoni sawa?" "sawa mpenzi wangu" "haya inuka nikupe nguvu na maelekezo" Brown aliinuka na mara viungo yake vilianza kurudi katika hali ya kawaida.

Salma alimshika Brown kwa nguvu sana kwenye mikono karibu na mabegani,michrizi ya damu ilianza kutoka kwenye mikono ya Brown kwa kutobolewa na kucha za Salma "mmgghhhh" aligugumia Brown kwa maumivu,alihisi kizunguzungu,Salma alimwachia Brown akapoteza fahamu,alizindika baada ya kama nusu saa,alijiona amebadilika na kuwa mzito sana,alihisi ana nguvu nyingi "sasa unaweza kuanza kazi hiyo kuanzia leo" "sawa mpenzi wangu" "chukuwa hela nenda kanunue kaniki na vitu vingine nitakavyokwambia" "sawa mpenzi wangu" "haya kazi njema" "asante" Salma aliondoka,Brown alifanya kama alivyoambiwa,watu walianza kupiga simu kwa Brown wakitaka kuelekezwa alipo,sifa za Brown zilisambaa sehemu mbalimbali ndani na nje ya Dar es salaam,alikuwa akiogopwa sana kwa vimbwanga vyake.

Baada ya miezi kama sita kupita,watu wawalikuwa wengi sana wakifuata huduma ya matibabu kwa Brown,majirani walianza kubeza tiba zake,Sama hakupendezwa,alidhamiria kufanya kitu ili kuwafundisha adabu,siku moja walikusanyika wazee wa jirani kwa maongezi ya jioni huku wakinywa kahawa,mara mzee mmoja aliuliza "jamani nasikia huyu jirani yetu siku hizi kawa mganga?" "ah wapi mganga atakuwa yeye? anawaibia tu" alijibu
mzee Ndali ambaye ni jirani kabisa na Brown,mara mzee mwingine aliyekuwa amekaa nyuma ya mzee Ndali alisema "ni kweli mganga maana watu wasingekuja hivi" "ah waoi wewe uganga mjini mwizi tu huyu" aliongea mzee Ndali huku akigeuka kumwangalia yule mzee aliyeongea,mara shingo ya mzee Ndali ikakataa kurudi,ikabaki huko huko nyuma,ikawa heka heka,wakambeba na kumwingiza nyumbani kwake,shingo ilizidi kuuma,ilifika hatua mpaka alikuwa akilia.

Hali ya mzee Ndali ikuwa mbaya,ndugu zake walikusanyika na kuamua kumpeleka kwa Brown baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa akimbeza sana,walimbeba mpaka kwa Brown,walipofika............ITAENDELEA



No comments: