MPENZI CHEUPE 12




Hali ya mzee Ndali ilikuwa mbaya,ndugu zake walikusanyika na kuamua kumpeleka kwa Brown baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa akimbeza sana,walimbeba mpaka kwa Brown,walipofika,walipokelewa na wapambe,Brown mwenyewe alikuwa ndani ana hudumia wateja wake,walipotoka wale wateja Mzee Ndali aliingizwa ndani "ah nini shida huyu si jirani yangu huyu?" aliuliza Brown kwa mashangao "ndiyo ni jrani yako hapo nyumba ya pili" "amepatwa na nini?" "hata hatuelewi" mara Slama alipanda kwa Brown na kumtumia kama kiti "waongo wakubwa nyie.... mimi ndiye niliyemfanya hivyo ili akome kuniongelea vibaya....haya msogezeni hapa" Haraka ndugu za mzee Ndali walimsogeza kwa Brown aliyekuwa amejifunika kitambaa chekundu,alitoa mkono wa kushoto nje ya kitambaa na kumsukuma singi mzee Ndali "usirudie tena mjinga wewe" mara mzee Ndali alipata nafuu shingo ilirudi kawaida.

Umaarufu wa Brown uliongezeka na kuvuma mpaka nje ya mipaka ya nchi,licha ya kuongezeka umaarufu pia masharti yaliongezeka toka kwa Salma,alitaka kila anapokuja kupanda kwa Brown lakima aandaliwe chakula,chakula alichochagua ni trei tano za mayai mabichi na dumu la lita tano la maji yaliyokorogwa na sukari nyingi,chakula hicho ni marufuku kupikwa,Brown hakuona kuwa ni kazi ngumu kumlisha Salma hicho chakula kwa kuwa wateja walileta fedha,gereji ilileta fedha,pia alikuwa akiuza mafuta ya dizeli na petroli ya wizi,kwa hiyo pesa alikuwa nayo ya kutosha kufanya chochote.

Brown alizoea ile  kazi ya uganga,sifa nazo zikamzidi,alitambua ana nguvu nyingi kuliko binadamu wa kawaida,alitenda mambo mengi ya kikatili,lakini pamoja na hayo yote aliyonayo wezi hawakuacha kuja kumjaribu,walikuja usiku wakaiba jenereta lake,alitangaza wiki nzima pale mtaani,misikitini,makanisani akitaka aliyeiba arudishe yeye atamsamehe,lakini jenereta halikurudi,aliamua kunyamaza na kuendelea na shughuli zake za uganga hata siku hiyo palikuwa na hitma mtaani kwake,jirani mwenye shughuli alimuomba amfanyie  dawa ya kufunga uwanja na kujikinga na wabaya wanaoweza haribu shughuli,Brown alienda akafanya kama mteja wake alivyotaka kisha lienda mpaka jikoni kafanya yake kwenye chakula.

Dua ziliombwa na visomo vilisomwa,chakula kikaliwa,shughuli ikafanikiwa vizuri,mwenye shughuli alisimama mbele za watu kuwashukuru,alimwomba na Brown aseme neno "ndugu zangu nawashukuru kwa kujumuika na ndugu yetu hapa na kufanikisha shuguli hii huu ni moyo wa upendo na utu...lakini naomba niwaambie kama katika shughuli hii wapo wale wezi wangu walioiba jenereta langu miezi mitatu iliyopita basi na wao ndiyo tumeshafanya hitma yao leo... ahsanteni kwa kunisikiliza" watu walitwanyika kila mtu akiongea lake,jioni kijana mmoja wa pale mtaani alianza kuumwa kichwa ghafla,walipoamua kumbeba na kumpeleka kwa Brown hakufika alifia njiani,asubuhi mwingine aliamka amevimba mshipa,kila baada ya saa moja mshipa uliongezeka,maumivu yalikuwa makali sana,walipoamua kumpeleka kwa Brown hakifika alifia mlangoni kwa Brown.

Baada ya siku tatu vijana sita walikuwa wamefariki katika hali ya kutatanisha,wakazi wa mtaa ule walikasirika sana,waliona njia pekee ni kumchoma polisi ili kwamba anauza mafuta ya wizi ili afungwe aondoke pale mtaani,polisi walipewa taarifa,walikuwa wageni hawakumfahamu vizuri Brown,walipanga kumvamia usiku,waliamini watapa hela za rushwa,mida ya saa tatu usiku polisi nane wenye bunduki waliingia nyumbani kwa Brown "upo chini ya ulinzi" aliongea Kamanda kiongozi wa doria "kwani tatizo nini" aliuliza Brown kwa sauti ya upole sana "hatuna muda wa kupoteza askari pekuwa kila sehemu" askari walitii amri na kutawanyika nyumbani kwa Brown,mwenyewe alikuwa hana wasiwasi,alikuwa akitabasamu muda wote.

Baada ya dakika kama tatu asjkari mmoja alirudi na taarifa kwa kiongozi yule wa doria "afande tumekuta nyuma ya nyumba shehena ya mafuta ya petroli na dizeli" "kama kiasi gani?" "afande kama pipa nne na madumu matani ya lita ishirini" 'sawa...sasa bwana unasemaje tukupeleke kituoni au unafanya maarifa?" "maarifa mimi sina kituoni pia afya" "anhaa wewe unadhani sisi tuna utani...haya simama juu" Brown alisimama "askari piga pingu huyu" "sawa afande" askari alikuja na kumfunga pingu Brown,kitendo cha kufungwa pingu kilimuuma sana Brown "kwani wataka kiasi gani yaishe?" "kama una milioni lete huna kesho mahakamani" "milioni mimi sina laki moja nawapa" "unatutania eeh laki moja alafu tunagawana vipi?" 'sasa huo mgawanyo mimi si kazi yangu" 'wewe jeuri sana basi utaozea jela".

Mabishano yaliendelea kwa muda kati ya askari mkuu wa doria na Brown "basi naongeza laki hapo..... zaidi sina cha kuongeza" "lete laki tano" "kweli sina zaidi ya hiyo laki mbili" "haya kalete usitupotezee muda" brown alifunguliwa pingu,aliingia ndani na kutoka na kiasi cha shilingi laki mbili taslimu na kumkabidhi mkuu wa doria "bakisha na ya sanda yako usitumie zote" aliongea Brown kwa sauti ya chini sana kiasi mkuu wa doria hausikia,polisi waliondoka na kumwacha Brown akiwa huru,majirani hawakuelewa kabisa kwa nini Brown aliachwa,walitaka achukuliwe,afikishwe mahakamani,afungwe wasimuone pale mtaani tena,sasa ameachwa huru,ilikuwa ngumu kuamini.

Siku iliyofuata askari wote waliokuwa doria jana usiku walikuwa mapumziko,kiongozi wa doria ile alipokwenda kulala hakuamka,alikutwa amekatwa shingoni na kitu chenye ncha kali,damu zililowesha shuka,wote wanane walikufa kifo cha aina moja, siku hiyo hyo moja iliwashangaza polisi wengine,mkuu wa kituo aliamua kumpigia simu mkuu wa kituo aliyehamishwa kumuuliza kama analolote analojuwa kuhusu Brown "hallo afande majanga tu huku nimepoteza askari wangu wanane kwenye mazingira tatanishi" aliongea kwa uchungu mkuu mpya wa kituo "pole sana afande yaani huko kuna magangwe very untouchable.... kuna ri jitu rinaitwa Brown lichawi mno ogopa sana hilo afande" " basi afande nimekuelewa jana hawa askari walizingira nyumba ya huyo mtu daah" "pole sana afande mimi yalinikuta...... afande yaani nilipo hamishwa nilishukuru sana...... pambana tu afande".

Vilio vilitawala kota za polisi,habari zikavuma,wenye imani zao walimtafuta Brown kwa ajili ya kugangwa,wengine waliona wamjaribu kwa nguvu zinzofanana na za Brown,mtanange mkali ulitokea baada ya mtu mmoja toka mkoani Mwaza al maarufu Ng`wana Kapolu yaani maana ya jina lake ni Mtoto wa porini,alifika kwa Brown akajidai anataka huduma,kabla Brown hajafanya chochote Ng`wana Kapolu alitoka nje ya nyumba ya Brown alinyoosha mkono mmoja juu kama dakika moja hivi,ilishuka mvua kubwa mpaka watu walitafutana,cha ajabu ni kwamba pale aliposimama yeye hapakulowa,ndipo Brown aliona anataniwa............. ITAENDELEA



No comments: