MPENZI CHEUPE 14




Brown aliona anataniwa,alitoka akasimama barazani kwake,alimwangalia Ng`wana Kapolu kwa muda,alitabasamu alafu alinyoosha kidole kimoja juu,mara Ng`wana Kapolu alianza kulia kwa sauti ya maumivu alikakamaa misuli ikaanza kuvimba na kupasuka na kutoka nje alafu ilipiga radi kali na kumchana chana vipande vipande Ng`ana Kapolu,tetemeko kubwa na ngurumo ya ajabu ilitetetemesha mtaa mzima mpaka majirani walitafutana Brown aliibuka mshindi,alitabasamu na kuingia ndani mwanume kamaliza kazi kwa kishindo,majirani walipiga simu polisi kutaarifu tukio la kifo cha Ng`wana Kapolu,polisi walifika wakakusanya mabaki ya majivu ya Ng`wana Kapolu na kupeleka hospitali.

Habari za Brown zilizidi kuvuma,upinzani na tamaa ya kujaribiwa ilizidi miongoni mwa waganga na wachawi toka mikoa yote ya Tanzania,Brown alijikuta kwenye upinzani mzito sana ambao ulihitaji nguvu kubwa na ya ziada,alilazimika kumwomba Salma amwongezee nguvu "mpenzi wangu naona wajinga wanaongezeka tu kutaka kunijaribu naomba uniongezee nguvu maana hili jaribio la Ngwana Kapolu limenishtua kidogo" "haaaaa haaaa haaaaaa aaaaa aaa Brown mpenzi wangu yaani wewe unataka nguvu tu bila malipo?" "malipo gani tena?" aliuliza Brown kwa ukali sana "ee eeeh iwe mara yako ya kwanza na ya mwisho kunikaripia umenielewa" ilimlazimu Brown kuwa mpole sana.

"sawa nimekuelewa mpenzi wangu naomba nisamehe sana" "sawa sasa wewe tangu unipe damu ya yule mwendesha mashtaka mpaka leo hujakumbuka kwamba mimi njaa inaniuma na nguvu sina nipe damu nikusaidie" "mh ! mbona ulikunywa ya wale polisi na leo nimekupa ya huyu mjinga toka mwanza"  "haaaa haaaa wale polisi ni kama nilikamata mwenyewe tu .... nataka utakaonipa wewe" "sasa nikukupa mimi na ukikamata mwenyewe tofauti yake nini?" "haaa haaa hujui ngoja nikujuze...... ukinipa wewe maana yake damu yao itadaiwa mkononi mwako" "khaaa ! Salma !" "nini... tena tangu lini wewe ukaniita jina?" "hayo mambo mimi ndiyo niliyakataa mapema" "usijifanye kutumbua macho jua kwamba huku kwetu damu ni bidhaa muhimu sana hakuna namna utakwepa hilo na wewe ulishingia huo mkataba wa kunipa damu tangu ulipo kubali nimuuwe yule mwendesha mashtaka"

Brown aliishiwa pozi,aliinama huku ameshika kidevu,aliwaza na kuwazua bila majibu "sasa nitakupa nani ili hali mimi naishi huku bila ndugu?" "wala sitaki ndugu zako hata wagonjwa wako tu wananitosha sana" "eheeee ! sasa wewe unataka kuniongezea balaaa" "mara ngapi? ukishindwa mimi nakuchukuwa wewe mwenyewe lakini siwezi kosa damu kizembe haaaaa haaaa aaaaa aaa" aliongea Salma na kupotea,Brown alibaki kwenye mshtuko na mshangao sana,dunia aliona inamwelemea,alitamani sana apate hata wa kumwomba ushauri asipate,aliamua kupambana mwenyewe,kazi nzito ilimkabili,usiku huo alipokuwa amelala alifatwa na wazee wawili,waliingia chumbani kwa Brown "ninyi kina  nani mnataka nini?" "haaaa haaa tulia utatutambua muda si mrefu,mara yule mzee mmoja apiga kitanda cha Brown kwa usinga,kitanda kikaanza kuwaka moto.

Moto ulishika chumba chote lakini wale wazee hawa kuungua "haaaa haaaa haaa wewe si unajifanya gangwe tutakufundisha" Brown alikuwa akihangaika pale kitandani moto ulimuunguza sana,aligugumia kwa maumivu,alikumbuka kusugua pete yake moto ukazimika,aliinuka na kukabiliana na wale wazee,aliisugua tena pete yake na kunuia maneno yasiyoeleweka wale wazee wakaanza kutafuta pa kutokea wasipaone "haaa haaa haaaa mnajidai magangwe kumbe wepesi tu" Brown alicheka na kuwakebehi,alichukuwa fimbo na kuanza kuwatandika,kisha aliwapa kilo moja ya chumvi ya mawe kila mmoja ili waile,walitaka kukaidi aliwachapa bakora za maana,walianza kula ile chumvi,ilipokaribia asubuhi aliwaacha wakaenda zao.

Siku iliyofuata taarifa za vifo vya wale wazee zilimfikia Brown,mmoja alikuwa ndiye mchawi mkuu wa Kigoma na mwingine alikuwa mchawi mkuu wa Sumbawanga,iliwalazimu wachawi wote wakutane kumjadili Brown kwasababu alionekana kuwa tishio kwenye ufanisi wa nguvu na kazi zao,kikao kilipangwa kufanyika Nchini Msumbiji usiku wa maanane,kila mhusika kwenye kikao hicho alijiandaa na tunguli za kutosha,walimhofia Brown anaweza kuwavamia,walikusanyika kijiji cha Chakha,kikao kilianzalakini walipofika kati.................... ITAENDELEA



No comments: