MPENZI CHEUPE 15




Walikusanyika kijiji cha Chakha,kikao kilianza lakini walipofika kati,lilisikika tetemeko la ardhi,kila mchawi alipatwa na hofu,walianza kuhaha wakigeuka huku na huko wasijue la kufanya,tetemeko lilichukuwa takriban dakika mbili ndipo likatulia,kishindo kikubwa sana kilisikika,wachawi,wote wakatahayari,ikasikika sauti kali "mnanitania?" wote walipatwa na mshtuko na kutetemeka,Brown alijitokeza pembeni yao akiwa ameshika fimbo na usinga mkononi mwake,alianza kutembea akiwazunguka huku akipunga ule usinga na kunenena maneno yasiyoeleweka,wachawi wote walishikwa na bumbuwazi,walikuwa wamechutama,waligeuka kumwangalia Brown alivyowazunguka,alipomaliza kuwazunguka wale wachawi walijikuta hawana uwezo tena wa kuondoka eneo lile.

Brown alianza kutamba "naona mmekaa kikao kunijadili..... kuna nani anayeniweza hapa,wote nawaona kama makinda ya ndege yanayojifunza kuruka... sasa leo nitawaonyesha mimi ni nani.... haya kiongozi wenu atoke mbele" aliongea kwa sauti ya majigambo sana,wachawi wote waligwaya hakuna aliyetoka "anhaa mnataka nimtambue mwenyewe siyo?" wachawi wote kimya waliinama chini ili kura isije ikamwangukia aliyemtazama Brown "nasema kwa mara ya mwisho atoke mwenyewe aliyekuwa kiongozi wenu" mara mzee mmoja alitoka mbele akiwa amenyoosha mkono mmoja juu kama vile alisema mimi hapa mkuu.

Alimwamuru yule mzee kusogea karibu,alisogea karibu na kushika sehemu zake za siri,aliziminya kwa nguvu mara Brown alipata maumivu makali sana "aghhhh" aligugumia Brown,wachawi wote waliangua kicheko kuashiria kuwa wamemuweza Brown,tukio lilidumu ka nusu dakika Brown alikumbuka kusugua pete yake na kunena maneno yasiyoeleweka,mara yule mzee ulimi wake ulianza kutoka nje,macho yalimtoka,ulimi ulijaa mdomoni mwake na kumfanya akose pumzi,alianguka na kufa,wachawi wote walifyata,mmoja wao alisimama na kuanza kuomba msamaha "bwana mkubwa tunakuomba utusamehe sana" "ninyi mnajifanya wajanja na mnajifanya mna umoja haya sasa uko wapi umoja wenu?" "utusamehe tu kwa kuwa huyu aliyekufa ndiye aliyetuponza" "mkitaka niwasamehe basi chagueni miongoni mwenu watu kumi nichukuwe damu zao"

Hapo palikuwa pagumu,watachaguana vipi? "msinipotezee muda fanyeni haraka la sivyo nitawamaliza wote" alisimama mzee mwingine na kuanza kuwashika vichwani baadhi yao akimaanisha kuwachagua,walipotimia kumi yule mzee alitoa kitu kama mpita wa moto na kumrushia Brown kama shambulizi,Brown alijikuta amerushwa mbali kidogo na pale walipokuwa wachawi,alianguka chini na kuinuka haraka,alitikisa kichwa kujiweka sawa kisha aliwaangalia wale wachawi amabo walianza kuruka na kuondoka "wote tulia hapo hapo" hakuna aliyebaki wote waliruka,Brown alisugua pete akawafuata huku huko juu,alianza kuwafukuza  mmoja baada ya mwingine,alikuwa akiwapiga na wao wanajibu,vita ilkuwa kali usiku kwa usiku,kila aliyeshindwa alianguka kwenye bati la nyumba ya mtu.

Mapambano yaliendelea kwa muda mrefu sana,mpaka walibaki wazee wawili,Brown alionyeshana nao makali,walikuwa wakizuia na kujibu mapigo ya Brown,mabomu ya kichawi ya kila aina yalitumika,ilikuwa kama vita ya tatu ya dunia,wazee wale walishangazawa sana na uwezo wa Brown katika mapambano kwa kuwa aliwashinda wachawi hodari kama mchezo,wakati mapambano yakiendelea na muda nao ulikuwa unasonga,asubuhi ilikuwa ikikaribia,walikuwa wakifukuzana kama ndege za kivita,mpambano ulifika juu ya nyumba ya mlokole aliyekuwa akiomba muda ule,wale wazee pamoja na Brown walijikuta wakiishiwa nguvu na kaungukia juu ya paa la yule mlokole,kishindo kikubwa kilisikika juu ya paa la nyumba,Brown alifanikiwa kuinuka na kutoweka japokuwa aliumia mgongo,alifika nyumbani kwake na kuanza kujiganga.

Wakati hayo yote yanatokia Salma alikuwa kimya,alikuwa akimwangalia Brown toka kwenye ulimwengu wa roho,alijuwa muda si mrefu nguvu zitamwishia na atapatikana na balaa kubwa,alikuwa akimfuatilia kila sekunde moja. Asubuhi magazeti yaliandika habari za wale wazee "WANGA WAKAMATWA WAKIWANGA" "WACHAWI WADONDOKEA NYUMBA YA MCHUNGAJI" "WAWILI WAKAMATWA WAKIWANGA MMOJA ATOWEKA" hivyo vilikuwa baadhi ya vichwa vya habari katika magazeti ya udaku. Hali ya Brown alianza kuwa mbaya,mgongo ulimuuma sana,alishindwa kuhudumia wagonjwa wake na wengine walimkimbia.

Salma alijitokeza "haaaa haaaaa haaaaaa aaaa mmmh Brown mume wangu unaendeleaje?" alimkejeli "ah ! naende.... lea vi..vibaya" "nilikwambia nipe damu niweze kukusaidia ukakaidi unaona sasa?" "mmmhh aaaagghh sshh" aligugumia Brown kwa maumivu na baridi "sasa endelea kuugua ukichoka utaniita" Salma aliongea na kutoweka,Brown alizidi kuwa mgonjwa,hakujuwa namna ya kujitibu,alijaribu kila aina ya tiba asili lakini hali ilizidi kudhoofu,muda wote alisikia sauti ya mtu akisali kama wanavyosali walokole,aligeuka huku na huko kumtafuta anayesali asimuone,alipata shida sana,alianza kama kuchanganyikiwa kwasabau ya ile sauti,alikuwa akiongea peke yake kila mara.

Sauti ile iliongezeka kichwani mwa Brown,aliamua akajisalimishe kanisani,kabla hajatoka kwenda kanisani Salma alimtokea akiwa mwenye hasira sana "na ole wako uende huko nitakuuwa" duh ! ilikuwa ngumu kwa Brown,hali ilizidi kuwa mbaya alafu Salma alimchimba mkwara mzito................. ITAENDELEA



No comments: