MPENZI CHEUPE 16




Brown alianza kuona dunia chungu,alifikiria ule mkwara kwa muda,aliamua kupiga moyo konde na kuamua kwenda kanisani lolote na liwe,ilipofika majira ya saa tisa alasiri aliamka,akaoga na kujiandaa kwenda kanisani,alitembea kwa shida sana mpaka kufikia eneo la kanisa mgongo ulimsumbua,alisikia sauti kali "Broooowwwnnn nnn nn nn" ile sauti ilimfanya alihisi kuchanganyikiwa,alichutama chini kwasababu alihisi ngoma za masikio zilitaka kupasuka,aliinuka na kujaribu kupiga hatua "Brown nitakuuwa" alishtuka na mapigo ya moyo wake yaliongezeka maradufu,miguu yake ilikuwa kama imefungwa nanga,alijaribu kuiburuza bila mafanikio.

Mchungaji aliyekuwa ndani ya kanisa akihubiri aliona kuna mtu mbali kidogo na kanisa amesimama,aliendelea kuhubiri huku macho yake yakiangalia nje mara kwa mara,waumini  nao walipatwa na shauku ya kuangalia nje,mchungaji alishindwa kutoa mahubiri "yaaani jioni ya leo tunavuka mto na kwenda ng`ambo nyingine aleluyaaaaa tumshangilie BWANA kwa makofi aleluya ale...alee...ale" mchungaji alikwama kwama kuhubiri,alikuwa akimwangalia Brown bila kumuelewa,aliamua kutoka nje kumfuata,waumini na wao walitoka kumfuata mchungaji "amani iwe kwako?" alimsalimia Brown "mmmhh mmmmhhh mmmmhh" aligugumia Brown huku akiwa ameuma meno akishindwa kutamka maneno,alikuwa bado akijaribu kupiga hatua asiweze kunyanyua mguu,

Waumini wote walipatwa na mshangao,ndipo mchungaji aliamua kumsogelea Brown na kumwekea mkono kichwani,Brown alibadilika na kuwa kama nyoka alimwagiwa mafuta ya taa "toka toka toka kwa jina..... toka toka" mchungaji alianza kumwombea Brown,lakini alikuwa hamalizii maneno,hakuna aliyegundua mbinu za mchungaji,waumini wote walikuwa wamefumba macho huku wakikemea pepo kwa sauti kubwa sana,wapita njia walistaajabu kilichokuwa kinaendelea pale nje ya kanisa,wengine waliangalia na kuendelea na safari,wengine waliwabeza,lakini mchungaji na waumini wake hawakujali waliendelea na maombi,baaada kama dakika kumi Brown alitulia,waumini walishangilia kuwa wamefanikiwa kumtoa pepo,walimwinua Brown na kuingia naye kanisani.

Ibada iliendelea,giza likaingia,Brown aliwaza atarudi vipi nyumbani,ibada ilipoisha Brown alimfuata mchungaji "samahani mchungaji mimi nashukuru kwa kunisaidia... lakini ninaogopa hata kurudi nyumbani" "oooh ! pole sana ndugu yangu... kwanza mimi si mchungaji,mimi ni Nabii... alafu ukishafanyiwa maombi hakuna nguvu yoyote ya kuzimu itafanya baya juu yako... uwe na imani tu mpendwa" manneo ya mchungaji hayakumwingia Brown ilikuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa,waumini waliondoka na Nabii aliondoka,Brown alilazimika kurudi nyumbani,alifika nyumbani kwake akiwa mwenye wasiwasi sana,alifungua mlango na kuingia taratibu kwa kunyata,moyo wake ulipiga kwa nguvu sana,akiwa ndani alisikia "hodiiii hodiii hodi" alienda kufungua mlango,alishika kitasa akasita,alikumbuka wale vifaranga,hodi ziliendelea.

Alishika mlango kwa mara ya pili na kuufungua "za saa hizi?" alisalimiwa Brown "nzuri" alijibu Brown akiwa macho makavu "samahani sisi tumekuja na shida ya matibabu" alijieleza mmoja ya watu watano walifuata matibabu ,moyo wa Brown ulipiga pigo moja la ngu kwa mshtuko "sss samahani huduma hapa hakuna mganga kahama" "lakini mimi nakufahamu wewe ni mganga nilishwahi......." "kabla hajamaliza kusema Brown alimkata kauli "we bwana we nimekwambia mganga kahama sasa wewe unanilazimisha?" aliongea Brown ka hasira "mh baba tunaomba utusaidie tuna shida kubwa" "we mama mwalimu wako alikufa? nimesema mganga hayupo tena hapa" aliuliza na kuonge Brown kisha liabamiza mlango kwa hasira na kuingia ndani.

Brown hakuwahi kwenda kanisani mpaka alipopata majanga kwa hiyo alikuwa hajui kusali,aliingia chumbani kwake,aliketi kitandani,alijikagua mgongo wake,ulikuwa bado na maumivu kwa mbali,alijaribu kusali akashindwa,alirudi jikoni akachemsha chai akanywa na mkate,akaenda kulala,alizima taa na kupanda kitandani,alipovuta shuka kujifunika,alihisi kuna mtu anavuta ile shuka upande wa miguuni na kuitoa kwa Brown,aliogopa,alishika kwa nguvu ile shuka,lakini aliona aliyevuta alikuwa na nguvu kuliko yeye,alikurupuka na kwenda kuwasha taa,haikuwaka,alichezea swichi ya taa kama mara nne,bila mafanikio,aliamua atoke nje ya chumba chake,alipapasa mlango hakupata kuushika,kila alipojaribu alihisi ukuta tu kama vile chumba hakikuwa na mlango,wasiwasi ulimzidi,jasho jembamba likaanza kumtoka,aliposhika ile pete alihisi kidole chake kimevimba sana,aliisugua ile pete hakuna kilichofanyika,alijiona kama yumo shimoni.

Aliendelea kuutafuta mlango bila mafanikio,aliamua atafute dirisha lilipo nalo hakuliona,chumba kukikuwa na giza totoro,Brown alijuwa wazi muda wake wa mateso umefika,alipapasa kurudi kitandani,alishika kitanda,alipotaka kupanda kitandani aligundua kuna mtu "mh nani wewe?" aliuliza Brown kwa sauti ya wasiwasi sana,hakujibiwa,alipapasa ili angalau akashike ukuta,mara alishika mapaja ya mtu "mh ! kwani tupo wangapi humu?" mara aliskia sauti nzito sana "tupo kumi" Brown alizidi kuchanganyikiwa,mara taa iliwashwa,macho yalimtoka baada ya kuona.............. ITAENDELEA



No comments: