MPENZI CHEUPE 17



Brown macho yalimtoka baada kuona mchungaji wake na kina mama wawili aliokuwa nao kanisani wamemtembelea usiku ule "ah...ah daah..ah mchung...." alitaka kusemea neno Brown asiweze "sssshhhhhh.... unataka kusema nini? ulipokuwa unaingia kwenye mambo haya ulitakiwa ujue kwanza siyo unavamia kazi za watu.... haya sogea huku" mchungaji alimwamuru Brown atoke karibu na kitanda asogee kwenye kona moja ya chumba "lakini wewe ni mchungaji" "alikwambia nani... wewe hujui ugumu wa maisha?" "naujuwa sasa ulitaka sisi tukale wapi?..... tukalime?" "hapana mchungaji sijamaanisha hivyo ila..." "kelele wewe....unajuwa wewe unacheza na maisha yako?.... mkataba uliouingia ni mgumu sana kwasababu mwisho utakwenda mwenyewe..... tazama sasa ulivyo mweupe yaani huna nguvu kabisa.... sasa sisi tutakuchezesha gwaride".

Kasheshe ilianza,mchungaji alianza kwa kugeuza nyayo za Brown badala ya kuangalia mbele zikawa zinaangalia nyuma "mh ! ndiyo nini sasa hiki?" aliuliza Brown huku macho yamemtoka "na bado heheeee hee" alijibu huku akicheka kwa dharau mmoja wa wale wanawake walikuja na mchungaji "jamani tafadhalini msinifanyie hivi" aliongea Brown huku akitia huruma sana "haya mama Mwaisa mpe ile kali achanganyikiwe kabisa" aliongea mchungaji akimwamuru yule mama mwingine amfanyie Brown kituko,mama Mwaisa alitoa majani aliyokuwa ameyafunga kwenye kaniki yake,aliyapikicha kwa muda wa takribani dakika moja,yalitoa harufu mbaya sana inayofanana na harufu ya kinyesi cha binadamu kisha alimsugua nayo Brown puani,alianguka na kupoteza fahamu,mchungaji pamoja na wale wamama walikuwa wakicheka kwa dharau sana.

Baada ya kama dakika tano Brown alipiga chafya,alizinduka,aliamka na kuketi,alihisi kuna maji maji yakitoka sehemu za siri,alipoangalia tu,mchungaji na wale wamama waliangua vicheko vya dharau na kukera sana "haaaa haaaa haaaa ulijitia mjuaji wewe tembea uone" aliongea mama Mwaisa "eeh bwana wewe ukijuwa huku wenzako wanajuwa huku"aliongea mchungaji huku akuonyesha mbele na nyuma kama anavyofanya Inzi,Brown alichanganyikiwa "khaa jamnai mambo gani tena haya yaani.... yaaani...." masikini Brown alijikuta amegeuzwa mwanamke na ameingia kwenye siku zake,alijiuliza moyoni "ina maana kuna wachawi zaidi yangu?" aliona hana namna zaidi ya kuwaomba kuungana nao "jamani tafadhalini msinitende hivi naombeni niwe mmoja wenu naona kuna mengi ya kujifunza" "weeeh muongo wewe kama uliweza kumgeuka jini itwakuwa sisi?" aliongea yule mama mwingine "na tena ole wako ukaseme sijui mchungaji mchawi nakwambia hutokufa ila cha moto utakiona".

Mchungaji na wale wamama walimdhihaki sana Brown,alijisikia uchungu kupitiliza,alitamani zingekuwa zile enzi zake angewaonyesha yeye ni nani haswa,lakini kila zama na msahafu wake,Brown amekwisha,hana nguvu tena,pete ipo kidoleni haimsaidii wala haivuki,ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Brown,"sasa sisi tuondoke tumwache ajifikirie ili akifanya maamuzi afanye maamuzi sahihi" aliongea mchungaji "na hizi siku zake atafanyaje?" aliuliza yule mwanamke mwingine "hizo itabidi asubuhu akanunue pedi haaa haaaa haaaaaa Brown" aliongea mama Mwaisa,mara mchungaji na wale wamama walitoweka "Salma... Salma Mpenzi wangu Cheupe nisaidie tafadhali" "haaaaa haaaa haaaa haaaaaa aaaa aaa aa aa aa" alisikia kicheko kikali sana,alitambua kilikuwa kicheko cha Salma.

Brown alitirirka machozi,aliumia sana moyoni "kwani nini nilikubali kuingia huku?.... ni lidhani kila mtumishi wa kanisa ni mtumishi wa Mungu...dunia imeharibika..... sina la kufanya...maisha yangu yote yameharibika,kweli kuna wakati wa kucheka na wakati wa kulia.... sasa nalipa gharama ya maovu yangu.... ee Mungu nisaidie" alijiuliza na kulalamika Brown,liwaza maisha yake atayamudu vipi? maana hatoweza kutoka akiwa katika hali ile,wakati akiwaza hayo,alipigiwa simu na mwenye eneo aliloweka gereji "hallo we mshenzi sikiliza nakuvumilia sana sasa nimefika mahali nashindwa nataka hela yangu,usiponipa leo kesho natia kufuli pale" aliambiwa maneno makali,kabla hajajibu chochote simu ilikatwa,aliinama kwa muda kutafakari,siku ilianza kwa kuwa chungu,aliona jahazi linazama na hakuna namna ya kujiokoa.

Nyayo za Brown zimegeuzwa nyuma,sehemu zake nyeti zimegeuzwa kuwa za kike,njaa inamuuma,anatokaje kutafuta chakula?,mchana wote alishinda bila raha kabisa,njaa ilimnyong`onyesha,mawazo yalitawala kichwa chake,alijuwa akitoka nje kutafuta chakula fedheha itampata,watu wakimuona miguu yake ilivyogeuka,aliishiwa pozi,hakuwa na mtu wa kumtuma,mtaa mzima walimuogopa,wapambe wake walishaondoka,aliishi kibabe sana enzi zake,sasa ni wakati wake kukutana na malipo yake hapa hapa duniani mbinguni ni mahesabu tu,Brown alishinda njaa,giza lilipoingia alikosa amani,mida ya wanga akiwa ameketi kitandani kwake huku ameshika tama ghafla alianza kuona giza wakati taa ilikuwa ikiwaka "eh ! hiki nini tena?" aliuliza katika hali ya woga "haaa haaaa haaaa tumekuja tena.... lazima tukutie adabu" alisikia sauti ya mchungaji "haaaa haaaa unaendeleaj na siku zako?" alisikia sauti ya mwanamke ikiuliza,brown alikuwa akipapasa papasa mara alishika........ ITAENDELEA



No comments: