SIMULIZI: NITAKUFA NA BIKIRA YANGU EP..... 01






Nikiwa nyumbani huwa sina majukumu mengi ya kufanya,
kwa siku nzima huwa nashinda tu kuangalia movie na kusoma baadhi ya vitabu,

kama tunavyojua elimu ya chuo hainaga mambo mengi kiasi chakufanya mtu hadi akiwa likizo awe anasoma,

semista (muhula) moja ikipita ndio imepita,
tukirudi tunaanza na mambo mapya kabisa na yaliyo pita huwa hayajirudii kwenye mtihani labda tu kuwe na muingiliano wa hayo masomo,

sikutaka kuichosha sana akili yangu kama nilivyo jiumiza nikiwa kidato cha sita kwa kulala masaa mawili au matatu kwa siku,
yote hiyo ilikuwa ni kwaajili ya kusoma kutafuta ufaulu wa kuingia chuo kikuu...

***

Hajra, chukuwa hii pesa, kuna fundi wa kuzibua choo atakuja hapa, utamwelekeza kuwa mfumo wa vyoo vya wapangaji kumeziba na maji yanarudi ndani ya vyoo,

"sawa baba, kazi njema...

nilimwitikia baba na kupokea zile fedha,

nilikuwa nikiishi mimi na baba na msichana wa kazi, mama alikuwa kijijini kumuuguza bibi,

nilitulia sebuleni kuangalia movie zangu za kinigeria kwenye laptop yangu,
nilikuwa nikipendelea sana movie za Nigeria sikujua ni kwanini, asilimia kubwa ya waigizaji wa nchi ile nilikuwa nikiwafahamu,
lakini nilie mpenda zaidi ni Regina Daniel,

Nilikuwa nikimuona tu yumo hatakama movie hiyo nimbaya lazima niiangalie hadi mwisho, alikuwa ni binti mzuri na mwenye kujituma na mtafutaji sana,

***

baada ya kama lisaa limoja alikuja fundi, nilimkaribisha na kuzunguka nae hadi kwenye vyoo vya wapangaji,

nyumba yetu ilikuwa na ukubwa fulani pamoja na vyumba vinne vya wapangaji ndani ya fensi,
walikuwa wakiishi mabinti tu wanaosoma chuo cha St. Joseph,

Nyumba yetu ilikiwepo mtaa wa mazimbu, jirani kidogo na Mazimbu Farm hapa Morogoro...

Walikuwemo mabint kama sita walio panga nyumba na walipapenda sana kwetu kwasababu za kiusalama,
Nyumba ilikuwa na fensi na mazingira yake yalikuwa tulivu sana kwa kujisomea,

***

Binti hii choo sijui imeziba kwa wapi,
 hembu nenda pale mbele ya nyumba yenu kuna mfuko wangu inayo vifaa niletee "aliongea fundi'

kwa haraka nilienda kuchukua ule mfuko na kumkabidhi,
alitoa ovaroli yake ndani ya mfuko na kuivaa kisha kuvaa gloves mikononi na kutoa spana kisha kufungua Chemba moja ilipo nyuma ya choo...

"Binti hii chemba haijaziba nadhani  kuna uchafu mkubwa umekwama njiani kwenye hizi bomba za kutoka ndani ya choo,
tatizo hawa watoto wa chuo hutupia pedi zao humu wengine anafulia chooni na mifuko ya sabuni wanaiflashi humu inasababisha kuziba"

aliongea yule mzee na kuinuka pale chini kuingia ndani ya vyoo,
alifungulia maji kwenye kila chumba cha choo na kurudi kwenye chemba....

"bint katengeneze povu la sabunu ya unga kisha kamwage kwenye matundu ya choo,

sawa"

nilijibu na kuweka maji kwenye ndoo kubwa kisha kumwagia sabuni ya unga na kumwaga chooni,

mzee alitoka na dawa yake fulani kwenye chupa na kumwaga kwenye kila tundu,

alimaliza na kuniambia turudi kwenye chemba,

harufu ilianza kutoka kali sana kwenye chemba,
uchafu ulio kwama ulianza kutoka kwenye njia ya choo,
niliziba pua kwa leso na kuendelea kushangaa pale,
sikuwa na kinyaa sana kwasababu nilishazoea kushika mavi nikiwa chuo,

nilikuwa nikisoma degree ya Labaratory science kwenye chuo kikuu cha Dodoma,
hivyo kushika mavi na kupima ilikuwa kitu cha kawaida kwangu,

" binti kweli wewe katili,
hata huoni kinyaa kuangalia hizi mavi, (aliongea mzee)

' enhee,
nilicheka tu na kujisemea kimoyomoyo laiti angejua huyu mzee ni jinsi gani nashika mavi na mikojo kila siku nikiwa maabara chuoni,

Uchafu ulitoka na mwishoe kuna mfuko mweusi wa nailoni ulitoka pia,
ulikuwa umeviringishwa kama mpira,

"dada mwambie baba yako awakanye hawa wapangaji kutupa pedi zao huku,

" aliongea yule mzee huku anaifungua ile mfuko kujua nini kilichomo ndani,

Ule mfuko ulizidi kutoa harufu kali sana na baada ya kumalizika kufunguliwa dam nyingi zilimwagika pale chini zikitoka ndani ya mfuko,
harufu mbaya ilienea karibu sehemu yote ya nyumba,

Fundi alirudi nyuma lakini mimi nilisogea na kuchukua kipande kidogo cha kijiti na kuanza kuupekuwa ule mfuko,

nilishtuka na kusisimka mwili mzima baada ya kuona ni kijusi kidogo (mtoto mchanga wa miezi kama mitatu na nusu au minne)

Kwa haraka kabla fundi hajarudi niliukunja ule mfuko kwa kijiti na kuusukumia kwenye chemba,

sikutaka aone ni nini kwasababu angemwambia baba na ingekuwa kesi kwa wapangaji...

nilimwaga maji mengi pale chini na kusafisha na sabuni ya unga hadi harufu ikaisha,
nikamwacha mzee anaendelea na kazi yake ya kuifunga ile chemba,

***

"Binti ni kitu gani kile kinanuka vile.??

ni pedi tu walikusanya na kuzifunga kwenye mfuko, nadani ziliingia maji ndomaana zikawa vile,

Nilimjibu mzee kisha nikaenda ndani kwangu,

nilikuwa na mawazo sana,
ni nini hasa wanakosa wasichana wenzangu hadi kufanya ukatili kama ule,
ni tamaa gani inawarubuni jamani.....

"nilijikuta nawaza hadi machozi yananitoka kama maji,

Eeee Muumba wangu naomba tusamehe Waja  wako,

niliongea na kujifuta machozi kisha kurudi sebuleni,

baada ya muda alikuja mzee na kumpa fedha zake kisha nikarudi chumbani...

Nitaitoa bikira yangu nikiwa ndani ya ndoa na mume wangu,
kumbe madhara ya kuwa na mahusiano yasiyo eleweka ndio makubwa kiasi hiki,
"niliongea na kuendela kulia"

Siku nzima sikuwa na raha hata kidogo, hadi jioni wapangaji wanarudi kutoka chuo nilikuwa nawaangalia tu wanavyo jichekesha wakifurahia choo kuzibuliwa na ilhali wanajua kabisa kilichoziba ni nini......

ITAENDELA....

LIKE, COMENT & SHARE

WHATSAPP: 0788294399



No comments: