SIMULIZI: NITAKUFA NA BIKIRA YANGU EP..... 02






ENDELA NAYO.......
Siku nzima sikuwa na raha hata kidogo, hadi jioni wapangaji wanarudi kutoka chuo, nilikuwa nimekaa njee nawashangaa tu wanavyo jichekesha wakifurahia choo kuzibuliwa na ilhali wanajua kabisa kilichoziba ni nini......

"Hajra, cheza uchezavyo lakini angalia sana Mwisho wako,
 'ni kauli ya kujipooza nilijipa na kuinuka kuingia ndani bila hata kuwasalimu wale wale wapangaji,

***

Jioni sana nilisikia honi na kukimbia haraka kufungua geti,
alikuwa ni baba katoka kwenye mihangaiko yake,

pamoja na biashara alizokuwa akifanya baba,
lakini alikuwa ni mwanasheria wa kujitegemea kwenye mahakama ya rufaa Mjini Morogoro,

ni miongoni mwa kazi ya pekee iliyokuwa ikimuingizia kipato kizuri nje ya biashara zake,

Tulikula chakula cha usiku pamoja huku tukiwa tunapiga story nyingi sana

"Mwanangu vipi nasikia ulikuwa unawajibika sana kumsaidia fundi leo,
hahahahahha safi sana mwanangu,
nikajua umetoka chuo basi hata kazi ndogondogo usingefanya....
'aliongea baba akiwa anacheka'

hapana baba mbona ni kazi ndogo za kawaida tu,
siwezi kuwa hivyo babaangu,
nitakuwa na malezi mazuri uliyonipa tangu mtoto, siwezi kuwa waajabu kiasi hicho....

Baba alitabasam baada ya kusikia maneno yangu,
tulikula na kuendelea kuangalia taarifa ya habari kwa usiku ule kisha baba akaenda kulala,

kwa haraka tulisaidiana na msichana wa kazi kuosha vyombo kisha kila mmoja akaingia ndani kwake kulala...

***

Siku zilisogea,
wiki ziliienda na mwezi uliisha na kurudi chuo,

ilikuwa ni furaha sana kwa kumisiana na rafiki zangu tuliokuwa mbali kwa mawiki kadhaa,

tulipendana sana kwasababu tunakaa chumba kimoja na tulishirikiana vitu vingi sana,

Martha alikuwa mwenyeji wa  same kilimanjaro,
alikuwa mpole sana hakuwa na maneno hata kidogo,

ila Asha na Brenda walikuwa hawaambiliki,
ni kila mda maneno,
haipiti siku kadhaa bila kukwaruzana au hata kupigana kidogo,

yote ya yote mwisho wa siku amani ilikuwa ikirejea na kukaa kwa amani sana..

"enheee mtoto wa baba Hajra umetuletea nini huko kwenu.?
maana wewe kila nikisikia unaongea na simu basi unaongea na baba yako,
 mama yako unaongea nae mara chache sana sijui kwanini (aliongea Brena huku akintumbulia macho)

hamna mimi nimeleta asali tu lita nzima,
mjilambe humu hadi mchoke,
nilijibu na kuvua juba langu nililo vaa kisha kufunga kanga kwenda kuoga

nilikuwa nimechoka sana kwa siku ile,

nilioga na kuvaa kisha kuongozana na wenzangu hadi (cafeteria) mgahawani kula chakula cha usiku..

"Mashost vip tutokeni basi out leo shemeji yenu kanitumia mesg hapa anakuja kutuchukua tukale mjini, (aliongea Asha)

Mweeeehhhh...!!!
twendeni tukavaeni viwalo hizi ofa hazijirudi jamani,  (alidakia brenda)

Martha alitabasam tu na kumshika bega Asha ili wageuke kurudi hostel kuvaa..

mimi niliendelea kwenda kula chakula,
 sikutaka kwenda mjini kwa siku ile nilikuwa nimechoka sana...

"we mtoto wa baba siunajidai umechoka sawa wewe nenda ukale ulale mtoto mzuri,
utatufungulia mlango tukirudi sawaeee! (aliongea Brenda huku akijibinua,)

nilicheka sana alivyojibinua na ufupi wake alikuwa kama kigoda,

Walirudi hostel wote watatu,
kwa haraka nilienda hadi kwenye chakula na kula kwa haraka..

Nikiwa njiani narudi room nilikutana na mkaka mmoja aliaonekana mstaarabu sana na mwenye kujiheshimu kwa kumtazama tu,

NITAFUTE WHATSAPP: 0788294399
***

Hajra mama...!!

"khaaaa we nani unae nijua jina langu.? mbona sikufaham na ndio kwanza nakuona leo...

" naitwa Samwel,
Nasoma degree ya Ualimu wa Hesabu na Fizikia..

samahani nimekufahamu tangu muhula ulio pita lakini muda tu wakukuona ulikuwa mgumu Hajra,
nashukuru kukutana na wewe leo, lakini naona kama unaharaka sana,

" ndio....
siunaona giza limeingia sasa"

nilimjibu kisha nikaangalia chini kwa hofu sana,

sikuwa na ujasiri wakumuangalia machoni kwa mda mrefu yule kaka,

nilijikuta nina aibu tu wakati hajaniambia chochote...

"nakuomba muda japo dakika kadhaa kuongea na wewe kwa jioni hii,
au turudi cafe (mgahawani) tukae tuzungumze japo nusu saa tu,

'aliongea yule kaka na kuniangali tena'

room kwako upo na  nani kwa saizi tunaweza kwenda kuongelea kule kama kurudi cafe utakuwa usumbufu kwako....
'alizidi kuongea yule kaka'

"nipo mwenyewe wenzangu wametoka muda huu kwenda mji,"

sawa naomba tukazungumze hajra..

"Oky"

Nilimjibu yule kaka na kuongozana nae kwenda ndani,

***

Ma shostoto,
nachati na Sam hapa kaniambia ameshampanga na sasaivi wanaenda room kuongea,

nmemwambia Sam amalize mchezo,
 huyu hajra sianajikutaga mtoto bikra,
 ngoja sam aende kumlegezea macho mule ndani hadi atoe mzigo..

Asha alikuwa akiwaambia wenzake wakiwa kwenye gari wakielekea mjini,

kumbe mpango wote waliuandaa mapema na lengo lao lilikuwa ni hajra atolewe  bikira anayo ringa nayo...

"Shosti, yaani sam sijui anayo macho gani,
yaani siku ile nakutana nae tu mjini nilijikuta nimelowa kabla hata hajaniambia kitu....
" alidakia Martha na kuongea....

kumbe martha pia alikuwa wale wale tu pamoja na upole wote alio nao lakini alikuwa ni kifagio hatari..

"namuaminia Samweli lazima amalize kazi pale,
kama aliweza kututia wote watatu bila sisi kujuana na tunakaa room moja kwanini ashindwe kwa hajra,
(alizidi kuongea Asha).....

" heeeeeee, tulieni Sam kasema wameingia room,
ona mesg hii hapa,
nilijua tu hachomoi kuku huyu anajidai mtoto mwema kumbe nyau tu,
ngoja atiwe hadi utoto umwishe,
maana ule ni utoto anatuletea shida zake apa...

NITAFUTE WHATSAPP: 0788294399
***

Karib samwel,
hapa ndio chumbani kwetu,
nakaa na rafiki zangu japo kwasasa wameenda out kidogo mjini nadhani baada ya masaa kama mawili watakuwa wamerudi...
'niliongea nikiwa nimeinamisha macho chini,
sijui hofu niliipata wapi mimi,'

"Ahsante sana hajra,
kwanza hongereni mmekipanga vizuri chumba kisafi,
nimepapenda sana kwa kweli....."

ahsante pia.... 'niliitika lakini nilikuwa natambua kabisa anajikomba tu,
watu tumekaa likizo mwezi mzima na tangu mchana tumerudi hakuna alie deki mabegi na nguo yametupwa ovyo kitandani alafu mtu anakwambia hongereni mmepapanga vizuri.... hahhaaha zitakuwa dharau hizi' 

Nilijikuta nacheka kimya kimya huku nakunja baadhi ya nguo zangu za ndani zilizokuwa kitandani na kuzifunika kwa shuka asizione.......

"unaonekana unapenda sana rangi ya pink,
aliongea samwel,

'hapana, kwanini umeniuliza hivyo.??

hamna naona nguo zako nyingi ulizokunja sasaivi rangi yake ni pink... (aliongea sam kwa kujiamini na kuniangalia)

aaaahhh hapana ni nguo za rafikiangu, nimeona tu siyo vyema zikae wazi na kuna mgeni humu ndani....

Enhe nakusikiliza,
twende kwenye mada...
maana mda unaenda...
kwanza kabla ya yote umenifahamia wapi jina langu.??

"Eee  eee ee... mimi kuna jamaangu mmoja unasoma nae aliwahi kunionyesha wewe tulikuwa kwenye Cafe tunakula... alafu,

Hembu kuwa streight.....
mtoto wa kiume inabidi ufunguke,
wewe ukianza kung'ata maneno mapema hivyo sasa mimi mtoto wa kike nitafanyaje...
Kuwa specific.. yaani eleweka...

haya enhe alivyo kwambia jina langu ikawaje tena...

Nilimuona Samweli anaanza kushika kalamu pale mezani mara ashike kijiko kilichokuwa kimekaa ovyo pale mezani,
mara asugue sugue chini kwa miguu yake asijue nini cha kufanya...... hakutegemea kama ningemgeukia kiasi kile.......

ITAENDELA......

WHATSAPP Group Kiingilio ni 1000 kwa mwezi mzima,
pia kuna story zingine nyingi za chombezo ya mapenzi... Lakini wanao ruhusiwa ni miaka 18 na kuendelea....

SEHEMU YA TATU YA STORY ITAENDELEA WHATSAPP USIKU WA LEO......

NITAFUTE WHATSAPP: 0788294399



No comments: