SIMULIZI: NITAKUFA NA BIKIRA YANGU EP..... 03





ENDELA NAYO.......
Nilimuona Samweli anaanza kushika kalamu pale mezani mara ashike kijiko kilikuwa kimekaa ovyo,
mara asugue sugue chini kwa miguu yake asijue nini cha kufanya...... hakutegemea kama ningemgeukia kiasi kile........

Nilikuwa natambua fika kuwa kila kitu tangu sam alivyokuwa akiwachezea akina Asha tena wakijua kabisa lakini wakawa wanajichekesha tu kwake,
 nadhani vihela vya boda boda alivyokuwa anapata ndio vilimpa kiburi...

"mbona kimya sana Sam,
nilimuuliza swali la kichokozi...

unasema ulikuma kozi gani Sam...

'Nasoma ualim wa Kemia na Fizikia...

umeona ulivyo muongo Sam..
mwanzo siuliniambia wewe unasoma ualimu wa Hesabu na fizikia,
Gafla Hesabu imegeuka kuwa Kemia(chemistry)

hayo ni majina ya kozi unayo yajua kwa kuyasikia eti...
Hivi Unakumbuka kuna siku nilikuwa CNMS ulinibeba hadi huku Tiba kwenye pikipiki yako tena ukaniomba namba nikakupa zisizo zangu,?

Hembu mda mwingine muwe na akili sawa,
mbona mnawaona watu wote wapumbavu eti..
unadhani kila mtu wakumchezea kama ulivyo zoea,
kuwa makini sam,

Maisha ni haya haya kama mnavyo jidanganya lakini maisha huhisabiwa kwa mema uliyo yafanya na siyo kwa mabaya kama unayo yaeneza wewe....

Hakuna mwanamke asie kufahamu kwenye hii block,

tunaingia humu ndani kila binti anatushangaa,
wananisikitikia ninavyo potea kwako.... naomba ujitambue Sam,

Kwa kazi yako unapata fedha nyingi ungekuwa makini ungekuwa mbali,

Sasa maamuzi ni yako na akili yako...
 ukiona nayokwambia ni mema naomba uyafanyie kazi,
na ukiona ni ujinga basi endelea...

Usiku mwema naomba uniondokee humu ndani.......

kwa hofu na aibu nyingi Sam alitoka mule ndani akiwa ameinamisha kichwa,
nilishusha pumzi na kupanda kitandani...

***

Baada ya dakika chache tu tangu Sam atoke mule ndani nilisikia mlango wangu ukigongwa,

niliinuka na kujifunga kitenge kwasababu nilishapunguza nguo kwaajili ya kulala,

nilifungua na kuchungulia...
walikuwa ni wadada kama sita wa vyumba viwili vya jirani yangu...

"hongera shost,
wenzio tulitega tu hapa mlangoni kutaka kujua nini kinaendela..

tulikuwa tunaumia sana kuona mtoto wa watu mpole na mstaarabu kama wewe unataka kurubuniwa na play boy kama yule.....

yule kaka ni kicheche sana na sasaiv amenyang'anywa pikipiki na bosi wake,
 alikuwa hapeleki hata mia moja kwa bosi,
hela zote alikuwa anahomga....

'mmmmhhhh...
nilibaki kuguna tu kwa zile kauli za jirani zangu,
kumbe walikuwa mlangoni wanakusanya umbea,
na wote walikuwa wakimjua sam kwa ujinga wake.....

"msijali jirani zangu,
huyu kaka mjinga sana,
kuweni nao makini,
vishawishi vidogo kama hivi ndivyo huharibu malengo ya watu....

sawa shost.....
Tunashukuru kama upo salama....
Usiku mwema hajra...
(waliongea wale wadada na kwenda vyumbani kwao)

Baada ya muda nikiwa sijasinzia nilisikia mlango unafunguliwa,
nilijua fika ni akina Asha..

waliingia na kufunga mlango,
walikuwa wakinuka sana pombe,
japo walikuwa hawapepesuki,

nilikuwa nawaangalia tu huku nacheza gemu kwenye simu yangu,

"pole mtoto mzuri,
umeumia sanaaa,
umesikia raha au inaumaaaaaa????,
(aliongea Brenda huku naniangalia,)

wenzake waliwahi na kumziba mdomo kisha kumfinya.......

" Msinitonyeeee mie,
kwani uongo kuwa Hajra kaliwa na Sam.?
mbona kila chumba ni skendo iliyo tapakaa,
anajidai kitoto saaana kumbe mbwaaaa tu.......
(alizidi kuongea brenda huku akivua nguo ili apande kitandani kwake kulala.)

Inamaana wenzangu ndio wamesambaza umbea kuwa nilikuwa na Sam humu  ndani,
Lakini mbona mda huu watu wametulia makwao,
kwani wamerudi saangapi hawa akina Asha,

nilitoka kwenda kwenye chumba cha wale wadada waliotoka ndani kwangu mda mchache kabla ya akina Asha,

'Mambo Monica,
eti akina Asha walikuja huku room kwenu mida hii...?

"hapana shost"
(alijibu Monica)

sasa nani kawaambia kama mimi nilikuwa na sam kule ndani.?

Hajra, baadhi ya mambo jiongeze mamy,
huu ni mchezo ulichezewa,
jana nilikuwa namsikia Brenda anaongea na sim na sam,
hakujua kama nilikuwa namsikia lakini njama yao kubwa walitaka bikira yako itolewe ili uache maringo yako,

kwasasa hii korido na vyumba vyote humu vinajua kuwa wewe ni bikira na sababu kubwa ni hao rafiki zako,

"Sawa Monika,
nashukuru kunifumbua jambo nisilokuwa nalijua.

Nilitoka na kurudi ndani kwangu,
lakini kabla sijafika nilisikia kelele nyingi kutoka mlango wa tatu kutoka ndani kwetu,

kwa uoga nilikimbia na kuingia ndani kwetu ili nijue kwanza ni nini ndio nitoke njeee,

'ni mapepo haya jamani,
yanamtesa sana mary,
halali kwa raha binti wa watu,

yalikuwa ni maongezi ya wadada wawili waliotoka kwenye kile chumba,
 na hapo ndio nikajua kuna mdada kapandisha majini,

Nilitoka na kwenda hadi kwenye kile chumba,

NITAFUTE WHATSAPP: 0788294399
***

Niliingia kwa kujihami lakini nilimkuta mary chini anagaragara tu na rafiki zake kila mmoja kajikunja kitandani kwake,.

"hivi nyie mnaakili kweli,
mwenzenu kapandisha mashetani badala mumuombee nyie mnalala,
 (niliongea kwa ukali kwa kumhurumia Marry)

wenzake walinyamaza tu kimya huku kila mmoja akiwa anachati,

Nilisogea hadi karibu na mary nikiwa na hasira sana kwa dharau za rafiki zake,

nilimshika mary kichwa na kuanza kumsomea angalau dua ili awe huru,

Bismilah rahman raheem!!!!! Alhamdullilah Rabi'l alamim, Aarahmani rahiiim.....
 kabla sijamalizia Mary aliinuka na kukaa,

Niliendelea kumshika kichwa na kumalizia dua zangu,
Baada ya kumaliza nilimuacha akalale na mimi kwenda ndani kwangu,

Ilikuwa kama gumzo pale hostel,
 wadada wa vyumba karibu vyote walikusanyika wakishangaa ni jinsi gani nimemuombea Marry hadi kuinuka na kupanda kitandani kwake......

nilipita bila hata kuwasemesha na kuingia ndani kwangu...

"heeeee!!!!!!!  Gwajima ndio hata hautusalimii waumini wako...... (aliongea dada mmoja kwa masihara baada ya kuona nimepita bila kuwasemesha jambo lililonifanya hadi mimi mwenyewe kucheka nikiwa chumbani)

yaani hawa wachungaji wa sikuizi bana hata salam hamna,
kamaliza kumponya mtu basi mbio ndani kwake.....

wale wadada waliendelea na masihara pale huku wanacheka,

nilipanda kitandani kwangu nikiwa na furaha sana kwa kumuweka marry salama,
wakati huo Akina Martha, Asha na Brenda walikuwa wameshalala Fo fo foo...

Nilipitiwa na usingizi lakini asubuhi nilikuwa wakwanza kuamka,

niliziba pua kwa harufu mbaya sana ya pombe na vyakula visivyo eleweka walivyokula akina Ashaa...

Walikuwa wametapika vyote kwenye sakafu chini,
Brenda ndio kabisa alikuwa ametapika kila kitu kwenye godoro lake kitandani......

ITAENDELA........

NITAFUTE WHATSAPP: 0788294399

SKY whatsapp group inawakaribisha.. kuchat na kusoma story mbali mbali.. hii story usiku wanasoma sehem ya 6..

kiingilio ni 1000 tu kwa mwezi mzima....

Nitafute whatsapp sasa



No comments: