SIMULIZI: NITAKUFA NA BIKIRA YANGU EP..... 08





SONGA NAYO...
Pole mama....
Lakini hujanijibu swali langu..
wewe ulikuwa msichana wa kazi tu kwetu ..
sasa imekuaje ukawa mke wa baba.???

"Daaahhh Hajra unamaswali magumu jamani...

Ilikuwa hivi.??

***

Baada baba yako kwenda msibani mama yako alirudi kufuata vitu vyake na kunikuta nipo mimi mwenyewe nyumbani...

Aliniagiza niolewe na baba yako...
na kwasababu alikuwa akijua kuwa mimi ni tasa basi hakuhofia madhara yeyote ya kuchanganya watoto.

Lengo lake kuu lakutaka mimi niolewe na baba yako ni kutaka siku moja mwanae ukija nyumbani usipate mateso ya mama wa kambo..
na ndio maana tangu uje hapa ukiwa mdogo sijawahi kukugombeza au hata kukuchapa..

nilikulea kama mboni yangu...

lengo kubwa ni kutekeleza maagizo ya mama yako mzazi..

Hajra wewe ni sawa na mwanangu.. mama yako ni kama dada kwangu... nilimpenda na kumheshim sana....

***

Siku kadhaa alirudi baba yako kutoka msibani ili kuendelea na majukumu yake..

nilijitahidi sana kumuomba amrudishe mama yako ila alikataa..

na kwasababu alinitoa uschana wangu baba yako alikuwa akiniomba sana aendeleze mahusiano na mimi...

nilimkatalia ili siku moja awaze kumrudisha mama yako..

lakini niliona anaanza mahusiano na mwanamke mwingine kutoka kazini kwake...

baada ya kuona ile hali niliamua kuanza kujirudisha kwa baba yako na kumtega kwa kila namna ilimradi tu awe na mimi kuliko aoe mwanamke mwingine..

lengo kuu ilikuwa ni kuhakikisha unaamani siku ukija kwa baba yako...

nilikusuburi kwa ham sana hajraa hadi ulivyorudi...

Mama yako alikata  tamaa ya maisha na kwenda dodoma kuanza kazi ya kujiuza...

nasikia alikuwa ni malaya alie kubuhu...

alishawishiwa na rafikiake mmoja alieitwa eliza...

Alikata tamaa kabisa na kutaka ajiue tu..
lakini baadae aliona bora akajiuze ili afe na Ukimwi tu..

hadi sasa sina mawasiliano nae na sijui hali yake au maisha yake huko dodoma...

***

baba yako aliingia kwenye mtego wangu na kujikuta anaanza mahusiano upya na mimi..

ilifikia hatua nilikuwa silali chumbani kwangu na kuwa nalala na baba yako..

baadae tulikuwa mke na mume hadi sasa..

Nisamehe Hajra ila nimefuata maagizo ya mama yako..

ukirudi dodoma nakuomba sana jitahidi kuulizia habari kuhusu mama yako huenda yupo hai angalau umuone tu maana humjui mama yako..

ulipotezana nae wewe ukiwa mdogo sana...


***

Nilishusha pumzi kwa mkasa alio nipa mama,

Ahsante mama kwa kunifumbua kwenye mambo ambayo sijawahi kuyajua hadi nafikia umri huu...

Inamaana baba pia alifikia hatu ya kukubaka..

daahhh naanza kuamini wanaume wote ni sawa..

inamaana ndugu wa mume wanaweza vuruga maisha ya watu kiasi hicho..

Mbona naanza kuiogopa ndoa sasa jamani mama...

"hapana ndoa ni njema endapo utafanya uchaguzi uliokuwa sahihi kabla ya kuingia kwenye mahusiano...

mama wewe unaongea tu..
unadhani mama hakufanya uchaguzi sahihi hadi haya yote kumkuta.???

mwanangu kwa hapo mimi sitaki kuchangia ila ndoa ni nzuri sana....

kikubwa uwe na imani na utafute mcha Mungu tu utakuwa salama kabisa hajra mwanangu...

"Hivi mama unakumbuka kuhusu yule dada nyumba ya pili alie gombana na mume wake kisa mume kumficha kuwa alikuwa na mtoto wa njee na mke wa njee..

mama hawa wanaume hawatabiriki na jinsi wanavyokujaga huwa hawaeleweki kabisa..

unaweza dhani mcha Mungu kweli kumbeee...

Mama acha tu.. yule kaka wa jirani unaweza mdhania kama alimdanganya mke wake..??

haya msichana wa watu na mimba yake ya pili alafu analetewa mtoto wa mume wake na kuambiwa mume wake alitelekeza mke dar...

Mama ujue haya mambo yanachekesha sana...

japo inauma lakini basi tu...

Mama UJUE KWA MSIMAMO NILIO NAO NAWEZA NIKAFA NA BIKIRA YANGU...

"weehh Hajra acha ujinga wako.

Mama huu ujinga nikiendelea kuona naweza nisitamani mahusiano wala kuolewa tena...

nikaishi maisha yangu tu mwenyewe tena yenye amani kabisa.....

Mama ungejua magumu nayopitia chuo..
mambo ninayo yaona..
vitu nilivyo viona humu nyumbani wakati wewe upo kijijini...
watu hawana huruma wanatoa mimba ovyo tu na kutupa utadhani kaenda chooni kunya...

"Hahhaha hajra unavituko..

mahusiano na ngono zisizo salama ndio chanzo cha mimba za hovyo pia ni chanzo cha kuharibu maisha ya wengi.....

Tunza bikira hadi uolewe mwanangu...

unaweza pewa mimba ukazalishwa na bado ukaachwa tu uishi maisha yako kwenu..

Fanya uchaguzi sahihi na uolewe sehemu sahihi utakuwa na amani mwanangu..

sawa mama yangu nakupenda sana Shostito...

Mimi pia nakupenda Shost... twende zetu tukalale kwangu basi siunajua baba yako kasafiri...

'Sawa mama.. (niliitikia na kumwangalia kwa tabasam kisha kwenda chumbani kwake)

ITAENDLEA..






No comments: