MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA KUMI NA SABA-17
WA WA KIJIJI
SEHEMU YA KUMI NA SABA-17
Kitendo kile cha Mwenyekiti kupotea katika mazingira ya kutatanisha kiliwashtua sana wanakijiji, wote wakajikuta wakipigwa na bumbuwazi. Mtaalamu ambaye aliletwa kwa dhumuni la kuwaumbua wachawi wa ndani ya kijiji akasema "Nafikilri tayati mmeshaanza kuona wenyewe kwa macho yenu, yani mpaka kiongozi anayewaongoza naye ni mchawi. Je, kwa wingine itakuaje?.."
"Mtaalamu nadhani hapa hakuna cha mswalie mtume, kilichobaki ni kuchoma moto kila nyumba itakayo julikana inamchawi" Alidakia mwanakijiji mmoja akimuasa mtaalamu. Hoja yake hiyo iliungwa mkono na kundi lote la wanakijiji, punde si punde mzee mmoja akawasha kibiliti lakini kabla uamuzi wa kuchoma nyumba ya Mwenyekiti haujatekelezwa mtaalamu alisema "Hapana hili sio jambo jema hata kidogo, sababu mtakuwa hamjapunguza kitu chochote. Hivi kati yenu ni nani anawafahamu wadudu aina ya kunguni?.."
"Wote mtaalamu tunawafahamu" Alijibu mwanakijiji. Mtaalamu baada kusikia jibu hilo akakohoa kidogo kisha akaongeza kusema "Vizuri kama mnawafahamu. Je, unaweza kuwateketeza ukawamaliza kunguni kwa kuwamwagia maji ya moto?.." Wanakijiji wote walikaa kimya wakati huo mtaalamu akiwatazama akisubiri jibu kutoka kwao. Mara baada kuona wameshindwa kujibu ndipo akawambia "Abadani kunguni huwezi kuwateketeza ndani kwa kutumia maji ya moto, bali watapoa ila baadae wataendelea kuzaliana. Hivyo basi ndugu zangu naomba mnielewe, hawa watu hamtowaondoa hapa kjijij kwa mtindo huo wa kuchoma nyumba zao. Tambueni watu hawa wanatembea na hirizi zao viunoni na mabegani kwahiyo njia pekee ambayo tutaweza kuwakomesha ni kuwakamata na kisha kuniachia mimi majukumu yangu, nitajua cha kufanya mpaka waachane na haya mambo ya ajabu ajabu " Alisema mtaalamu. Maneno hayo yaliwafanya wanakijiji kutuliza munkali, wote kwa pamoja wakapoa huku minong'ono ya chini chini ikisikika." Yani badala watu kuwaza maendeleo ya kijiji chetu, wao wanawaza kuhusu uchawi..."
"Ndio maana maendeleo hatuna, tutapaje maendeleo hali ya kuwa watu ambao wangeleta maendeleo ndio hao hao wachawi?.."
"Hakika huyu Mwenyekiti kuanzia leo hatufai, kwa vyovyote vile cha mtema kuni atakiona" Walisikika wanakiji hao baadhi kwa sauti ya chini kabisa wakimuongelea Mwenyekiti wao. Wakati minong'ono hiyo ikiendelea kusikika, muda huo mtaalamu alikuwa akinynyuzia dawa kwenye mlango wa nyumba ya Mwenyekiti. Zoezi hilo alilifanya kwa muda wa dakika kadhaa kisha akawamuru wanakijiji wasambalitike kila mmoja akaendelea na majukumu yake.
Upande wa pili nyumbani kwa mzee J, mpaka asubuhi mkewe alikuwa bado hajarudi. J aliwaza sana jambo, lakini kipindi anafikiria kipi afanye, ghafla alikuja swahiba wake mzee mwenzake. Mzee huyo aliitwa Magambo. "Jaruo kulikoni mzee mwenzangu mbona umeshika tamaa, huna hili wala lile. Hivi unahabari yoyote kuhusu mkeo?.." Alisema mzee Magambo akimwambia mzee J. Ambapo naye mzee J aliposikia sauti hiyo alikurupuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo, kwa sauti ya haraka akahoji" Eeh unasema?.. "
" Mmmh punguza papara basi bwana Jaruo, hebu kaa chini kwanza..." Mzee J alipoambiwa hivyo alitekeleza, akakaa chini. Hapo ndipo mzee Magambo akaendelea kusema" Enhee kwanza habari za siku mbili hizi, maana Jaruo umepotea sana. Hata kilingeni kwa sasa huji, yani natesa tu kwenye bao kwa sababu hakuna mtu anayenipa changamoto "
" Mmh ndugu yangu we acha tu, yani kwa sasa nipo bize sana kiukweli, si unajua pilika za hapa na pale istoshe Kipindi hiki ni chamavuno kwahiyo najikuta nakosa hata ule muda wa kwenda kilingeni. Enhee tuachane na hayo bwana, nambie unahabari gani kuhusu mke wangu?.. "
" Mkeo yuko kisimani kalala miguu inaning'inia ndani kichwa nje" Alijibu mzee Magambo. J akashtushwa na taarifa hiyo, ndani ya nafsi yake akajisemea" Alah kumbe? Sawa Sawa "
" Unajua matukio kama haya sasa yanakidhili hapa kijijini, na nilicho Kuja kugundua kijiji hiki kimejaza wachawi sio bure " Aliongeza kusema mzee Magambo kwa taharuki kubwa.
" Ni kweli mzee mwenzangu wala hujakosea " Aliunga mkono mzee J, muda huo huo ilisikika sauti ya mwanamke ikiwasabahi. Kwa pamoja wazee hao walitikia, kisha mwanamke yule akaongeza kisema " Hivi mnahabari?.. "
"Hbari gani tena?.. "Magambo akahoji.
" Mwenyekiti wetu hafai huyu mtu hata kidogo " Alisema mwanamke yule, mzee J na Magambo wakatazamana kisha J akamtaka mama huyo azungumze kwanini amenena maneno hayo ya kumuhusu Mwenyekiti wao. Mwanamke huyo kabla hajasema alitazama kwanza kulia na kushoto hakuona mtu kisha akasema" Ni mchawi " Mzee J na mzee Magambo wa kashtuka kwa mara nyingine tena wakatazamana, punde J akamgeukia mwanamke huyo kisha akamuuliza" Umejuaje?.. " Swali hilo la mzee J lilimfanya yule mwanamke kuongea mambo yote yaliyotokea nyumbani kwa Mwenyekiti mpaka pale mwenyekiti alipoamua kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
" Oophho tumekwisha mzee mwenzangu "Alisema mzee Magambo baada kuyasikia maneno ya yule mwanamke. Lakini wakati mzee Magambo anasema hayo, huku mzee J akili yake ilikuwa inafikiria mbali mno. Akili yake ilikuwa ikimfikiria mtaalamu aliyethubutu kujitoa muhanga kwa niaba ya kuwaumbua wachawi wa kijijini kwake.
"Doh hapa nisipokuwa makini nitaumbuka" Alijisemea hivyo kimoyomoyo mzee J hapo ni mara baada kuwaza kwa kina zaidi. Muda mchache baadaye alinyanyuka akaambatana na mzee Magambo, ila walipofika mbali kidogo na nyumbani kwa mzee J waliachana. Mzee Magambo akaelekea nyumbani kwake, ilihali mzee J akaelekea kisimani kumfuata mkewe ambapo mbele kidogo alipotea akaibukia kisimani. Hapo napo hakutaka kupoteza muda, alimnyanyua mkewe kisha akatoweka naye. Alipo mfikisha nyumbani akammwagia baadhi ya dawa, mama Chitemo akawa amerudi katika hali yake.
"Sasa ngoja nikaonane na wakuuu wangu ili niwashe moto rasmi, na kabla yoyote nitaanza na huyu kiherehere anayetaka kuvuruga mipango" Alisema mzee J huku akazisuka vilivyo hirizi zake. Sasa hasira zote akazipeleka kwa mtaalamu aliye jitosa kulivalia njugu suala la kuwaumbua wachawi wa kijiji cha Ndaulaike.
Kwingeneko kijana Maige alionekana akakikimbia kuelekea nyumbani kwa mzee Mligo. Alipofika alimkuta rafiki yake yupo nje anaota jua la asubuhi. "Saidon.." Aliita Maige.
Saidon aliposikia sauti ya rafiki yake akageuka kisha akaitika.
"Rfiki yangu unajua ukisikia siku ya kutafuta sifa mbele ya warembo wa kijiji hiki basi ni leo"
"Hahahaha ah kwanini Maige?.." Saidon alihoji.
"Sababu katika vijiji ambayo mabinti hupenda soka na hiki kijiji chetu kimo.. Hasa ukiwa mcheza mpira mzuri mbona utawakimbia wewe?.."Alijibu Maige. Saidon ndani ya nafsi yake akajisemea" Naweza kucheza soka vizuri lakini mpira ni michezo wa ajabu sana. Nisije nikajinasibu mbele ya Maige halafu uwanjani nikaja kuonekana kituko. Hebu ngoja ninyamanze tu, maana kama ni mrembo tayari Chaudele ameshaonyesha tas ya kijani kwahiyo ananitosha. Na hata box lile la kondom nitafanya mpango nilichome moto tu hakuna namna. Isitoshe kijiji chenyewe sikielewi kabisa "
"Mbona umeduwaa? Soka limekupita kushoto?? "Maige alimuuliza Saidon baada kumuona kazubaa, asijue kuwa muda huo Saidon kuna mambo alikuwa akiyaweka Sawa akilini mwake.
" Daah ni kweli ndugu yangu, mpira nacheza ila sio saana kawaida tu. Unajua hayo ni kama mazoezi tu ya kukimbia " Maige aliposikia maneno ya Saidon aliangua kicheko kisha akasema "Ndugu yangu kwa mwendo huo, usitegemee kama utampata Chaudele. Hivi unajua kuwa yule jamaa niliyekwambia anamtaka Chaudele ni fundi wa kuchezea mpira na kucheka na nyavu?.."
"Yupi yule mtoto wa mchawi?.." Saidon aliuliza.
Maige akajibu "Huyo huyo. Ni moto wa kuotea mbali, Chitemo mpaka kijiji cha pili wanamuelewa vizuri. Na hivi leo ni kombe la ng'ombe basi tutegemee maajabu kutoka kwake. Kwaheri ngoja nikafanye shughuli zangu mapema ili niwahi uwanjani" Alipokwisha kusema hayo akaondoka zake. Punde mzee Mligo akatoka ndani akiwa na ngoma ndogo iliyowambwa ngozi kwa ustadi wa hali ya juu. "Saidon haya kumekucha sasa, ngoja nikatoe taarifa kijijini juu ya michezo wa leo ili wanakijiji wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao" Alisema mzee Mligo akimwambia mjukuu wake. Saidon alishangaa sana ila hakujaji, zaidi alimtakia babu yake kila raheri.
"Sawa viazi vimo na karanga kwahiyo kazi kwako" Aliongeza kusema mzee Mligo kwa sauti ya mbali.
Baada mzee Mligo kuondoka zake, ghafla Chaudele akaja ambapo alikuja kwa style ya kunyata alipomfikia Saidon akamziba macho. Saidon alihaha ila mwishowe Chaudele akavitoa viganja vyake kwenye uso wa Saidon kisha akaungua kicheko ambapo Saidon naye alicheka kisha akasema "Tabia yako sio nzuri bwana"
"Kwanini Saidon jamani, au hupendi utani?.." Mrembo Chaudele alihoji.
"Aah mimi tena? Mmh ila cha muhimu na wewe upende utani. Sio nakutania unakasirika" Alijibu Saidon., Chaudele akaongeza kusema "Sawa wala Usijali. Nina haraka Saidon, nimetoroka nyumbani nimekuja kukujulia hali kwanza. Lakini pia nimekuja kukuuliza vipi unajua kucheza mpira?.." Swali hilo la Chaudele lilimfanya Saidon kunywea kidogo wakati huo akijisemea "Loh sijui nimjibu nini? Nikimwambia sijui nitaonekana tikiti maji. Nikisema najua mwisho wa siku mpira ukanikataa nitaonekana hata kwenye mahusiano nitakuwa muongo. Daah ila potelea kote bora nionekane tikiti maji tu"
"Aah hapana mimi sijui ila nacheza ingawa sio mchezaji wa kutumainiwa kama wengine" Alijibu Saidon.
"Sawa lakini naomba tuwe wote uwanjani wakati tu naangalia mpira" Alisema Chaudele, Saidon akacheka kidogo halafu akajibu "Sawa Usijali".
Baadaye jioni umati wa wanakijiji wapenda soka walikusanyika uwanjani kwa tiketi za kulipia sababu uwanja ulikuwa umejengwa uzio kwa makuti. Ndelemo na vificho vilitanda kila mahali huku wakisubiri muda ufike ili kabubu lichezwe. Na hatimaye muda ule uliokokuwa ukisubiliwa kwa shauku kubwa ulifika, mpira ulichezwa kijiji cha Ndaulaike na kijiji cha pili. Mpaka dakika arobaini na tano za kwanza zinamlizika kijiji cha pili lilikuwa kinaongoza kwa magoli mawili huku kijiji cha Ndaulaike kikiwa bado hakijapata goli. Simanzi ilitanda upande wa kina Chaudele na wenzake, sababu siku hiyo hata Chitemo mchezaji walikuwa wakimtumaini wala hakuwa mchezoni. Alicheza hovyo kabisa kiasi kwamba timu yao ilielemewa.
Mpaka dakika ya themanini, matokeo bado yalikuwa ni yale yale goli mbili kwa sifuri, punde si punde mchezaji wa Ndagu star timu ya kijiji cha Ndaulaike aliumia kwahiyo alihatajika kuingia mtu mwingine ili kuziba nafasi wakati huo wachezaji wa akiba alibaki mmoja ambaye naye alilalama kuumwa tumbo hali iliyowapelekea viongozi wa timu kutafuta walau kijana mwenye uwezo wa kucheza mpira ili achukue nafasi ya yule mchezaji aliyeumia.
"Kumuiteni yulee kijana, mwambieni babu yake anamuita" Alisema mzee Mligo alimuhitaji Saidon aingie uwanjani kusakata kabumbu. Saidon aliposikia wito huo alimwambia Chaudele "Nisubiri nakuja, babu ameniita mara moja" Alipofika kwa babu yake, mzee Mligo hakusema neno lolote zaidi alimrushia jezi. Saidon akashangazwa na kitendo hicho wakati huo tayari Ndagu star imeshaongezwa goli la tatu dakika ya themanini na tano. Mashabiki wa timu ile Ndagu star iliyopo chini ya mkufunzi mzee Mligo walinyong'onyea, walikata tamaa kabisa hali iliyo wapelekea kutanda na majonzi ikiwa upande wa wapinzani wao ilikuwa ni shangwe kubwa kubwa mno.
"Hizi sio dakika za kuanika meno, unaingia uwanjani sitaki maneno Saidoni " Mzee Mligo aliongea kwa msisitizo huku uso wake ukiwa umejaa hasira. Saidon hakuona haja ya kuendelea kujaji, upesi alivaa jezi na kuomba refa ampe ruhusa ya kuingia. Mashabiki karibia wote wa Ndagu Star wakiwemo na wachezaji wakiongozwa na Chitemo walilaumu sana mabadilko hayo, waliamini uongozi wao umechemka sanjari na wengine kuchukuwa uamuzi wa kuondoka uwanjani hapo.
Lakini punde baada kuingia, alipigwa pasi ya chini kutoka kwa beki wa kulia, pasi hiyo mujarabu aliipokea kwa kuutuliza mpira kwa madaha na mbwembwe kisha kukimbia nao kwenye chaki. Ajabu sana, alimpiga chenga mtu wa kwanza wa pili na wa tatu kisha akatoa pasi kwa mchezaji mwenzake, apesi akarudishiwa. Alipo ipokea kwa mara nyingine tena kutokea kwa kiungo namba nane, alikimbia nao na kufanikiwa kuwapiga chenga mabaki mpaka kipa, kwa utashi na ujuzi wa hali ya juu akafunga goli matata.
Shangwe zikalipuka, Ndagu Star wakamshangilia Saidoni kwa furaha huku akidiliki kuwaacha midomo wazi wanakijiji ambao walimzarau na kumbeza, hali ya kuwa hata wale waliokuwa wameondoka walirudi upesi kushuhudia kandanda safi kutoka kwa Saidoni.
Hatimaye dakika tisini zilikamilika, muamuzi wa akiba aliongeza dakika ya nne za nyongeza.
Dakika ya pili kati ya zile za nyongeza, Ndagu star walipata penart baada Saidon kuchezea mazambi eneo la hatari alipokuwa akiwahadaa mabeki ili acheze na nyavu kwa mara nyingine tena. Goli hilo la penart alilofunga Chitemo likatosha kusawazisha, ubao ukasoma moja moja. Dakika moja kabla ya nyongeza kumalizika ili waingie kwenye matuta, Ndagu star wakapata kona baada kufanya shambulizi kali la kushtukiza.
Kona hiyo aliipiga Saidoni ambapo ilipelekea mpira kujaa nyavu I moja kwa moja. Hakika ilikuwa ni furaha kubwa yenye historia yake kijijini Ndaulaike, mrembo Chaudele alilia kwa furaha achilia mbali Maige ambaye alipigwa na bumbuwazi kwa uwezo mkubwa alio uonyeshe rafiki yake.
Shujaa wa mchezo huo akawa Saidon, taarifa kila kona ya kijiji ikiwa inamzungumzia Saidon tu hata mzee Nhomo naye alidiliki kumsifu lakini jambo hilo likamkwaza sana Chitemo. Licha ya timu yake kuchukuwa mnyama ng'ombe "Kwanini asifiwe Saidon tu? Hapana lazima niongee na mzee wangu mapema ampoteze huyu jamaa la sivyo nitamkosa Chaudele wangu!" Alijisemea Chitemo wakati huo akirudi nyumbani kwao baada mchezo kumalizika.
Baada ya hayo kupita, hatimaye usiku mnene, nyumbani kwa bibi Pili michakato mzito ikazungumzwa, palikuwa na mkutano mdogo wa wachawi wa kundi hilo. Kiongozi wa kundi alisimama na kisha akasema "Jamani tayari mambo yameenda mlama, mchana wa leo nisingepotea mbele ya umati ule basi mngenikosa kiongozi wenu"
"Kwanini mkuu? Kuna balaa gani?" Aliuliza mchawi mmoja aliyeonekana kuwa na shauku kutaka kujua chanzo cha mkuu wake kunena maneno hayo..

No comments: