MREMBO WA WA KIJIJI SEHEMU YA KUMI NA NNE-14



MREMBO WA WA KIJIJI


     SEHEMU YA KUMI NA NNE-14

Mzee Mligo alipokwisha kusema hayo alipanda baiskeli yake akaendelea na safari  kuelekea kijiji cha pili. Upande wa pili huku kijijini kwao nyumbani kwa mzee J hatimaye Chitemo hali yake iliimarika kiasi kwamba aliweza kutamka neno lolote lile. Kitendo hicho kilimfurahisha sana mzee J, kwa sauti ya upole akamuuliza kijana wake balaa gani alilo kumbana nalo kabla ya kupoteza fahamu.

"Chitemo hembu nambie mwanangu ni nani aliyekufanya hivi?.."

 "Baba wewe acha tu, bibi Pili ndio kanifanya hivi. Na laiti kama baba mdogo asingefika mapema basi mwanao nimgekufa"  Alijibu Chitemo akianza kwa kushusha pumzi ndefu.

"Pole sana mwanangu ila usijali, muhimu umeshaniambia basi nitajua cha kufanya"

Chitemo aliposikia maneno hayo akatabasamu kidogo halafu akajibu "Nakuaminia baba fanya kweli ili heshima itawale kwenye familia yako"

"Aha hahaha!.." Alicheka mzee J kisha akasema "Ndio maana mimi huwa sipendi dharau"  Alipokwisha kusema hayo, punde mzee Bidobido alifika. Naye alijikuta akiacha tabasamu baada kumuona Chitemo hali yake imeimarika.

 Bidobido alimtazama Chitemo na kusema "Chitemo baba uko vizuri?.."

Chitemo akatabasamu kwanza kisha akasema "Kama unavyoniona bamdogo, aamh nashukuru sana kwa msaada wako. Maana kama usingelikuwa wewe  Chitemo ningeitwa marehemu mpaka muda huu"

"Aha hahahah" Alicheka mzee Bidobido kisha akaongeza kusema "Usijali wewe ni mwananetu kwahiyo hatutokubali kuona ukinyanyaswa na vipakashumi vya kijiji hiki"

"Ni kweli kabisa" Alidakia mzee J. Hapo Chitemo alinyanyuka kutoka kwenye kilago alichokuwa amelalia akaawachia uwanja baba zake ili waendeleze zogo. Mzee J alimgeukia mdogo wake na akasema "Unajua mdogo wangu vita hii sasa imeshakuwa patashika?.."

 Bidobido alishtuka kusikia maneno hayo. Akakaa vizuri kisha akahoji "Enhee kwanini unasema hivyo?.."

"Kwa sababu ukiachilia mbali mpango huu wa kumuadabisha mzee Nhomo. Kuna kibwengo kingine kimejitokeza" Alisema mzee J.

 "Mmh ni nani huyo?.." Bidobido akarudia kuuliza.

"Bibi Pili, huyo mzee naye sio wa kubeza"

"Ni kweli kibasa kaka, tena kama ndio huyo niliyemkuta na Chitemo basi ni moto wa kuotea mbali. Makombora yake ni yakukata na shoka, abadani hatowezekanika kama hatutojipanga" Alijibu mzee Bidobido.

"Mmh bwana weeeh!.." Alishangaa mzee J kisha akasema
"Lakini mdogo wangu hatupaswi kuogopa, mimi mwanaume na wewe ni mwanaume kwahiyo kinacho takiwa tushikamane ili tuweze kuukata mzizi wa fitina"

"Hapo wala hakuna tatizo" Aliunga mkono mzee Bidobido, baada ya hapo aliaga kwamba anaelekea shambani kuendelea na shughuli. Kipindi hicho nyani na ngedere walikuwa wakivamia shambani na kisha kushambulia mazao,  mzee Bidobido alikwenda shamba kulinda. Lakini kabla mzee huyo hajafika mbali arudi, akamwambia mzee J kuhusu suala la kijana Saidon kujiwekea mikakati ya kumtongoza Chaudele. "Mmh Chaudele huyu huyu mrembo wa kijiji?.." Alihoji mzee J kwa shauku ya hali ya juu.

"Ndio bwana mkubwa, ila usiwe na wasi wasi kwa sababu nilishaongea na babu yake. Nikamwambia amkanye mjukuu wake kuhusu Chaudele la sivyo kitampata kitu kibaya sana" Alisema mzee Bidobido. J akatabasamu ila kabla tabasamu lake hilo halijafikia tamati, Bidobido akaongeza kusema "Lakini sasa mzee Mligo baada kumwambia hivyo akaonyesha na yeye umwamba wake sababu nilipomwabia vile nilipotea ajabu na yeye akapotea. Kwahiyo inaashiria kuwa na yeye yupo vizuri, umakini unahitajika katika hili bwana mkubwa"

"Doh! Hakika kijiji hiki tayari kimegubikwa na laana, hiki ni kijiji cha wachawi sio siri. Inamaana hapa kijijini kila mmoja ni mchawi sema wengine hawataki kujionyesha, yani mpaka Mligo naye!?.." Alisema mzee J huku akionekana kushangazwa na yale yanayo tokea kijijini Ndaulaike. Kumbe  wakati wazee hao walipokuwa wakiteta jambo, Chitemo aliyasikia yote mwanzo mpaka mwisho. Hivyo alishangaa baada kusikia kuna mtu kajitokeza anamtaka Chaudele.

" Inamaana huyu mtu ni mgeni hapa kijijini?.." Alijiuliza Chitemo.

"Sasa ngoja nitamnyoosha" Aliongeza kujisemea hayo kijana Chitemo huku moyo wake ukiwa umefura hasira zisizo na mfano.
  Kwingeneko sasa, alionekana mrembo Chaudele akiwa nyumbani kwao akimsaidia mama yake kazi mbali mbali za nyumbani. Lakini licha ya Chaudele kufanya hivyo, mawazo yake yote yalikuwa kwa kijana kutoka mjini. Naye si mwingine ni Saidon. Ukweli Chaudele alitokea kumpenda sana Saidon tangu mara ya kwanza alipomuona akiwa na babu yake walipokuja nyumbani kwao kununua nyama. Kutokana na hali hiyo, Chaudele alijikuta akifanya kazi huku moyo wake ukiwa na furaha isiyo kifani. Furaha iliyompelekea kutabasamu muda wote huku ikifikia mahala kucheka mwenyewe. Hali hiyo iliendelea kutawala machoni mwake, na mwishowe mama yake akamgundua ambapo aliweza kumuuliza "Chaudele nini tena? Mbona unacheka peke yako?.."

Swali hilo la mama Chaudele kwa binti yake lilimfanya kuzidi kuangaua kicheko na mwishowe akajibu "Hapana mama wala usiwaze, kuna kitu nimekumbuka kwahiyo kimenichekesha" Alijibu Chaudele, jibu ambalo halikuweza kumlidhisha mama yake, zaidi aliishia kuguna tu huku moyoni akihisi jambo.

  Usiku ulipoingia, nyumbani kwa mzee Nhomo mama Chaudele alimwambia ile hali harisi iliyotokea mchana wa siku hiyo. Mzee Nhomo alishangaa sana kisha akasema "Lakini mke wangu, ukiona mtoto wa kike anacheka hivyo ni dalili ya nini?.."

"Baba Chaudele inamaana unataka kusema tumuozeshe tu Chaudele kwa Chitemo?.." Alihoji mama Chaudele. Mzee Nhomo akajibu "Lah sina maana hiyo ila.."

"Ila nini mume wangu? Maana yako ni kwamba kujichekelesha kwa Chaudele ni kutaka mwanaume wa kuishi naye.."  Alidakia mama Chaudele, akiongea kwa hamaki kubwa mno.

"Kwahiyo binti akijichekelesha basi anahitaji mwanaume?.." Alihoji mzee Nhomo. Hapo mama Chaudele akajibu kwa ufupi tu "Kwenda zako huko niache nilale, kama umeshindwa kupambana na J bora useme tu mapema" 

"Mimi? Sio rahisi kihivyo mama Chaudele, tena unako elekea utaniudhi. Na ukishaniudhi kifuatacho unakijua. Shauri yako" Alisema mzee Nhomo kisha akavuta shuka tayari kwa safari ya kuusaka usingizi ili baadaye aamke kwa niaba ya kumkabili mzee J. Usiku wa balaa kijijini Ndaulaike.
   Usiku wa manane ulipo wadia, usiku wa mbalamwezi ukiwa umemulika kijiji kizima huku sauti za ndege na wadudu zikisikika kwa mbali kijijini hapo. Mara ghafla angani ilioneakana miale ya moto isiyopungua kumi na mitano, na punde si punde kundi kubwa la wachawi lilitua nyumbani kwa mzee J. Baada ya muda mchache mzee J akatoka ndani akiwa tayari katika mavazi ya kichawi huku mkononi akiwa amekumbatia kibuyu alichoambiwa akajaze damu itakayo msaidia pindi atakapo kuwa katika mapigano dhidi ya maadui zake.

Bada ya salamu na mambo kadhaa kuhusu uchawi, mzee J kama kiongozi wa kundi hilo aliawasa wenzake kuwa anahitaji damu ili kushinda vita yao. "Na mahala pakuipata damu hii itakayo tufanya kushinda vita hii ni nyumbani kwa mzee Mligo. Pale kuna kijana yule mgeni tuliyekuwa tunataka kumjaribu  ikashindikana, kwahiyo safari hii hatuwezi kushindwa kwa sababu nimejizatiti vya kutosha" Alisema mzee J.

"Hahahahah" Waliangua vicheko wachawi waliokuwepo hapo, kila mmoja alifurahishwa na taarifa hiyo mpya, muda mfupi baadaye walipanda nyungo zao kisha wakaanza safari kwa kasi ya ajabu kuelekea kwa mzee Mligo kwa dhumuni la kumfyonza damu kijana bishoo mgeni wa kijiji kutoka jiji la bandari. Saidon. Kumbe wakati  timu ya mzee J ilipokuwa angani ikielekea kwa mzee Mligo, Mligo naye alikuwa chumbani muda huo huo akiwatazama kupitia jungu lake kukuu lenye mkojo wa mama mjamzito. Mkojo mahususi uliotumika kutazamia kile kinacho endelea ulimwengu wa pili.

"Ahahaha hahaha" Mligo aliangua kicheko. Cheko la dharau kabisa baada kuwaona wachawi hao wakija kwa kasi ya ajabu na mbwembwe za hapa na pale, alipo hitimisha cheko lake akasema "Naona wameamuwa kulianzisha, sasa acha mimi nimalize ili wajue kuwa kuna tofauti kati ya uchawi na ugolo kama ilivyo utofauti wa tobo na shimo" Alimaliza kwa kiguno huku akijiandaa kikazi, kwingineko nyumbani kwa bibi Pili ilitua timu nyingine ya wachawi kwa uchu na utashi!

JE, WANA AGENDA GANI? NA VIPI MZEE MLIGO NA KUNDI LA MZEE J.. SAIDON ATAFYOZWA?
   HAYO NA MENGINE MENGI TUKUTANE SEHEMU IJAYO..
     SHEA MARA NYINGI ILI NIKUTUMIE MUENDELEZO FASTA KABLA HAIJAPOA..



No comments: