Nawashwa Chini 10





SIMULIZI - Nawashwa uku
SEHEMU - 10
ILIPOISHIA..
Tuliishia pale ambapo chemchem ya chuki ilipoanzia baada ya jackrine kumtoa nje mari nakumuuliza kuhusu jeff lakini pia muda huo huo akawafumania mama yao hatukujua kama alifanikiwa kuyanasa yale marumbano yao,
ENDELEA NAYO.
"NYIE KUNA NINI HAPA MBONA MNASUKUMANA SUKUMANA" boss lady aliuliza huku akimtazama kila mtu machoni kubaini kama kuna kitu wanachomficha "NYIE SINAWAULIZA MBONA MMEKAA KIMYAA??" bado boss lady aliwauliza huku akizidi kuwakagua machoni mwao ambapo kila mtu alikuwa ameinamisha kichwa chini tu. "mama maria" kabla jackrine hajaropoka maria alimdakia njiani ili asiendelee kuongea kisha maria akasema huku akimtizama boss lady "mama ni hivi huyu jackrine alinikopesha kahela kidogo sa nimekwama nimemwambia ukinipa mshahara nitamlipa lakini kawa mkari kweli" maria ilibidi atumie uongo kupotezea mada. "shingapi??" boss lady alimuuliza maria "elfu hamsini" maria alimjibu "weee ni elfu hamsini tu??" jackrine nae alijifanya kumdai kweli kuzidi kumpoteza maboya boss "ni shingapi? sasa?" maria aliuliza "na ile elfu ishirini nyingine ya juzi kati hapa??" kweli walitumia drama bomba iliompoteza kabisa boss lady na hakujua kilichokuwa kikiendelea pale hivyo aliuliza "kwo nishingapi jumla unayomdai?" alimuuliza swali jackrine "Elfu sabini mama" jackrine alijibu haraka huku wote wawili wakimuangalia boss lady akitoa hela kwenye kipochi chake kisha akamkabidhi jackrine "wewe maria mshahara wako mwezi huu nakupa nusu, alafu nije nisikie tena makelele yakudaiana hapa kama unashida we maria nifate uniombe mimi sio kupigizana mikelele tu hapa" alisema boss lady susan bila kujua ile pesa anayoitoa ilikuwa ni sadaka hakuna deni wala nini, alikamkabidhi jackrine kisha akahakikisha kila mtu anatoka pale na kurudi kwenye chumba chake baada ya hapo waliongozana na mume wake wakapanga gari lao V8 nakuteleza kuelekea kazini,
***************************
usiku wake walirudi wakiwa wamelewa kweli jambo ambalo lilinishtua kwani yapata mwezi nikiwa katika nyumbani ile sikuwahi kumuona hata siku moja boss akiwa amelewa leo ilikuwa ajabu kwangu tofauti na jackrine,morine pamoja na mari wao walishazoea ile hali.kama kawaida ya pombe huwa haina adabu boss lady alijikuta akianza kuongea maneno ya ajabu yaliyochochewa na pombe alioinywa kupita kiasi "jeff mpenzi wangu hivi mimi naweza kweli kuchafuliwa na wewe upo?? sema nikupe shingapi ili tu usiniache?? we tu ni wewe tu ndio..!!" kabla hajaendelea kuropoka alianguka chini na kupoteza fahamu lakini ajabu nilipomtizama mume wake alikuwa hajalewa hivyo alikili ya haraka ikaniingia "anha!! nimeshaujua mchezo jamaa kamlewesha mke wake kimakusudi akijua pombe hainaga siri akishalewa atatoboa siri, na ndivyo amemshinda ila hapa amekwama mi ndio master plan akitaka kucheza namimi ataumia mi sichezagi tumichezo tudogo tudogo hutu" jeff aliendelea kujisemea kimoyo moyo huku akimtizama big boss alivypkuwa anaogiza kama amelewa, akiwa anamnyanyua boss lady jicho baya aliendelea kumwangalia jeff lakini jeff nae hakukapua macho wala kugeuza shingo alizidi kumkazia macho vile vile. pale alipokaa jackrine nae alijisemea kimoyo moyo "Anha!! ukweli nimeanza kuunasa najua mama amelewa yale anayoyasema itakuwa ni pombe lakini nazidi kuupta ukweli wakwanza kwenye huu mchezo ni huyu jeff anamchezesha mama na maria fala huyu nikiujua ukweli???" alisema jackrine huku akimuangalia jeff kwa jicho baya, haisaidi kwani jeff ni genius anauwezo wa kuwala familia nzima na wote wasijue kama wanaliwa na mtu mmoja,
**************************
asubuhi sana na mapema niliamka nakufanya mazoezi yangu ya kawaida na baada ya kumaliza mazoezi nilianza kwa kulisafisha banda la kuku huku nikiwabadilishia vyakula, kisha nikaenda garden kulisafisha nikiwa naendelea na usafi sijui hili wala lile big boss aliamka siku hiyo asubuhi nakuja moja kwa moja mpka pale garden akiwa amekunja ndita hatari akaniuliza "ULIMSIKIA BOSS WAKO ALICHOKISEMA?" kwa taratibu nikamjibu "kipi boss wangu?" "HIVI WE FALA NI WAKULALA NA MKE WANGU??" boss aliuliza huku akinitizama kwa jicho la uchu kama simba mwenye njaa akiwa mawindoni kumkamata swala "hapana mbona sielewi unachokizungumzia boss wangu?" bado niliendelea kuwa mpole nikimpa nafasi atambe tu kwani hata akipiga kelele zake ni bure kama tunda nishalila tayari hivyo nilikuwa mpole tu "ANHAA!!! HAYA DOGO NITAJUA TU UKWELI HAKUNA SIRI HAPA, CHINI YA JUA" alisema boss yule nakuondoka kwa hasira alichokipanga kukipata hajakipata zaidi liliondoka likiongea lenyewe huku linaingia ndani,lioia
baada ya kupambazuka, jua kukua na kila mtu katika nyumba ile kuamka kila mtu alikuwa mezani akiwa amechukua nafasi yake kupa kifungua kinywa kama ilivyo ada kwa muandaaji kumpakulia kila mtu lakini siku hiyo hiyo kazi niliifanya mimi kwanzia maandalizi ya chai mpaka kupakua, wote tukiwa mezani morine, jackrine,maria big boss, na boss lady akiwa tayari hangover imeisha. nilipakua sahani zote nilipofika kwa maria baada ya kumpakulia alisema "ahsante mume" aliongea kwa makusudi huku akimtizama jackrine lakini jackrine aliuchuna tu lile neno lilimuuma boss lady alijisahau kabisa kama kuna mume wake pale alijikuta aking'aka "NINI???" "kila mtu akashtuka na kumtazama boss lady baada ya kujishtukia alikaa "mke wangu kwani kuna tatizo maria kumuita huyu kijana mume??" big boss aliuliza kinafiki lakini boss lady kabla hajanyanyua kinywa kujibu chochote gafla alianza kuhisi kichefu chefu nakutoka haraka kukimbilia nje na alipofika nje alitapika kweli huku akishuhudiwa na watu wote akiwepo na big boss, "Hii sio mimba kweri????" morine aliuliza kwa mshangao,
JE KWELI BOSS LADY KASHIKA MIMBA?? na kama kashika mimba unafikiri nini kitamkumba jeff ikigundulika?? sehemu ya kumi na moja ndio itatoa majibu



No comments: