SIMULIZI: NITAKUFA NA BIKIRA YANGU EP..... 06





SONGA NAYO...
"Huna lolote...
 unajidai mpolee kumbe kicheche tu Hostel nzima inakujua..
(aliongea Brenda na wote wakacheka)

Niliingiza vitu vyangu vyote na mwishoe nikachukua godoro langu kwasababu kitanda kilichobaki ndani kwa akina Monica hapakuwa na godoro..

Nilifuta vumbi na kutandika kitanda kisha kuoga na kupanda kulala.

kiasi fulani amani ya moyo wangu ilikuwa imerudi.

***

Asubuhi nilioga kisha kwenda darasani mimi na Monika...

Monika alikuwa akiniheshimu sana, alipenda  kampani yangu kwasababu ya ustaarabu nilio nao,
nilishukuru kumpata rafiki wa namna ile..

Tulishirikiana kusoma kila siku mimi na monica,
ushirikiano wetu ulitufanya tuwe imara sana kwa masomo darasani,

siku zilienda,
wiki iliisha na hatimae miezi hadi kufikia mtihani wa mwisho wa muhula wa pili...

ufaulu wangu ulipanda kwa kiasi fulani tofauti na mwanzo...

Baada ya mwaka wa kwanza kuisha na kwenda likizo ilikuwa ni nafasi ya pekee kuhama chumba cha mbali zaidi...

Nilishakuwa na rafiki wa shida na raha ambaye ni Monica hivyo sikuwaza sana...

Nilikwenda nyumbani kwa amani zote na kuanza likizo ndefu

***

Siku kadhaa zilipita nikiwa likizo nyumbani..
Mama pia alirudi kutoka kwao kumuuguza mama yake..
alinipenda sana mama yangu wa kambo..

Nilikuwa nikiishi kwa amani sana nikiwa nae,..
hata kumuomba baba hela za pedi haikuwa ngumu nilikuwa nikimwagiza tu mama....

Sababu pia kubwa ya mama kunipenda ilikuwa ni ufundi wangu wa kusuka..

 alinitegemea sana kumsuka na karibia staili zote za nywele nilikuwa nasuka.

Sikupenda kuonyesha hicho kipaji chuo nikihofia usumbufu..

Jioni ya siku moja baba akiwa kwenye safari zake za kikazi nilikuwa na mama tunaangalia mchezo kwenye TV...

"Hajra rafikiangu..
hivi unajua sababu za mama yako kuondoka hapa.?.

mmmhhh hapana shost'
(nilizoea kumuita mke wa baba shost kwasababu alikuwa ni rafiki tu kwangu...

Upo tayari nikusimulie.?
hautochukia.??
 na jee hauto nichukia mimi pia.??

" hapana mama siwezi chukia...
kwani kwajinsi navyoishi na wewe sioni dosari yeyote..
hapa tunapiga story tu...
(niliongea nakutabasam kidogo)

***

hajra mimi nilikuwa ni kama msichana wa kazi hapa kwenu mara tu baada ya wewe kuzaliwa...
nyumbani kwetu ni kijiji kimoja na mama yako hivyo alikuja kwetu kuniomba niwe msichana wake wa kazi hapa mjini nyumbani kwenu...

Nilihamia na kuishi hapa hadi mama yako kuondoka..

Nakumbuka siku kadhaa kabla mama yako kuondoka ilikuwa hiviii

MIAKA 18 NYUMA....

Walikuja wageni kama wanne kutoka kigoma ni ndugu wa baba yako.. walikuwemo shangazi zako wawili na bibi yako...

Siku hiyo hapakuwa na mtu mwingine nyumbani zaidi yangu...

Niliwapokea na kuwapa chumba cha wageni.

"Dada Husein yupo wapi.?
(aliongea bibi yako)

Ametoka na mke wake na mtoto ni kawaida yao siku za jumamosi kama hizi kutoka na wanarudi saa tano au sita za usiku...

" yule mama aliniangalia kwa muda kidogo na kuguna kisha kurudi chumbani....

Baada ya dakika kadhaa alikuja shangazi yako mmoja...

" eti dada kaka ametoka saangapi na mke wakeee.?

Ni muda kidogo kwani vipi.?

"huyu mwanamke anamuharibu sana kaka kwa starehe zake..
yaani kaka hakai na hela zake.
pale tu amemloga kama hujui shogaangu..
lakini usimwambie mtu..
mwanamke yule mchawi kama nini...

mmmhhh niliguna na kutulia nikimwangalia yule dada..

baada ya kuonasijamjibu kitu aliamua kurudi ndani...

Usiku uliingia zaidi na saa sita kweli walirudi na mimi ndio niliwafungulia geti..

Walisalimiana pale na kumbeba mjukuu wao ambae ni wewe na baadae kwenda kulala..

Yale maneno ya shangazi yako yaliniumiza sana na vile namfaham vyema mama yako kuanzia watoto alafu baadae mtu katoka alikotoka na kumuita mchawi..

***

Asubuhi baba yako huwa ananaondoka saa moja kasoro kwenda karizi.
hivyo ndugu zako walishaamka kumsalimia..

mama yako alikuwa bado kalala..

"kaka hii ni mara ya tatu tunakwambia kuwa maradhi ya kifua ya mama yanaletwa na huyu mkeo...

sasa changanya akili yako mwenyewe.. kama unampenda mwanamke au mama yako.??

'daaahhh.. baba yako alivuta pumzi na kuwaambia wataongea baadae...

" sawa kaka wewe dharau vitu,
siku mama yako anakufia hapa ndio utatambua

Baba yako alipanda gari na kuondoka...

Nakumbuka sikuhiyo mama yako kaamka hakuna anae msemesha...

nyumba ilikuwa kimya sana...

"mama yako akanifuata jikoni..

" eti dada kuna nn kinaendekea humu ndani.?

"sijui dada kwakweli..
lakini si salama sana kwako..

" baada ya mama yako kusikia vile aliondoka kurudi ndani....

Siku zilizidi kwenda na wiki kadhaa baadae bibi yako alipata homa kali sana akiwa morogoro..

Mazimbu kuna mbu wakali sana na kuna malaria mbaya sana...
bila kumeza dawa ya maleria kila baada ya miezi hata sita inakuwa mbaya kwa afya ukiwa maeneo ya Mazimbu..

Bibi yako aliugua siku kadhaa na kufariki dunia....

ilikuwa ni majonzi makubwa sana...

Nakumbuka ndio ilikuwa siku namuona baba yako akichukia...

alimfukuza mama yako kama Mbwa..
 hakutaka kumuona kabisa na wala hakutaka kukuona wewe.....

ITAENDELEA....






No comments: